Mashine ya Kukamua mafuta ya alizeti

Funge

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
581
165
Wana JF naomba msaada wenu. Ninahitaji kununua mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti. Ningependa kujua ni wapi naweza kupata mashine hiyo, pamoja na bei yake. Ninaishi Morogoro.
Natanguliza shukurani.
 
mkuu hiyo nenda temdo arusha njiro unapata kwa m tano lkn unasahau habari ya matengenezo kwani ile ni chuma tupu all the best
 
Wana JF naomba msaada wenu. Ninahitaji kununua mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti. Ningependa kujua ni wapi naweza kupata mashine hiyo, pamoja na bei yake. Ninaishi Morogoro.
Natanguliza shukurani.

Mkuu kama walivyo kuambia, ila kwenye hizi mashine kuna Tatizo moja.

1. Mashine nyingi zinazo zalishwa Tanzania ni nzuri kwa uimara ila kwenye kukamua mafuta hazina uwezo wa kukamua kwa 100% zinakamua 50% hadi 70% yaani hazimalizi mafuta kwenye alizeti

2. Mashine za India ndo inasemekana zina presing kubwa ya angalau kukamua kwa 90% hadi 100%

NDO MAANA VIWANDA VYOTE ZAIDI YA 50 VYA KUKAMUA MAFUTA BABATI HAKUNA KINACHO KAMUA KWA 100% NA YALE MASHUDU HUWA YANANUNULIWA NA MHINDI MMOJA ANAITWA MOUNT MERU HUYU HUKAMUA KWA MARA YA PILI YALE MASHUDU NA KUPATA MAFUTA, YEYE ANA MASHINE Z
A KUKAMUA KWA 100%
 
Mkuu hapo kwenye bei nadhan wadau wameshakusaidia, hivyo nitakaa kimya. Lakini ninakushauri katika mahesabu yako uongeze na gharama ya PURIFIER, kwan bila kufanya hivyo mafuta hayatakuwa na ubora unaostahili
 
Mtoa maada na waliokujibu wote siwasikii mkiongela kuhusu viwango...........ama uwezo wa mashine husika ziwe za hapa nchini ma zanje
 
Mkuu kama walivyo kuambia, ila kwenye hizi mashine kuna Tatizo moja.

1. Mashine nyingi zinazo zalishwa Tanzania ni nzuri kwa uimara ila kwenye kukamua mafuta hazina uwezo wa kukamua kwa 100% zinakamua 50% hadi 70% yaani hazimalizi mafuta kwenye alizeti

2. Mashine za India ndo inasemekana zina presing kubwa ya angalau kukamua kwa 90% hadi 100%

NDO MAANA VIWANDA VYOTE ZAIDI YA 50 VYA KUKAMUA MAFUTA BABATI HAKUNA KINACHO KAMUA KWA 100% NA YALE MASHUDU HUWA YANANUNULIWA NA MHINDI MMOJA ANAITWA MOUNT MERU HUYU HUKAMUA KWA MARA YA PILI YALE MASHUDU NA KUPATA MAFUTA, YEYE ANA MASHINE Z
A KUKAMUA KWA 100%

mkuu asante sana kwa elimu ya mashine nilikuwa sijalifahamu hilo, mimi ninafahamu zile machine za mkono zinazofanana na za kubangua karanga na mbaya zaidi unapokwenda kununua machine label zake huwa hazioneshi efficiency ya ukamuaji. Hizo machine za india bei yake roughly inafika ngapi?
 
Mkuu hapo kwenye bei nadhan wadau wameshakusaidia, hivyo nitakaa kimya. Lakini ninakushauri katika mahesabu yako uongeze na gharama ya PURIFIER, kwan bila kufanya hivyo mafuta hayatakuwa na ubora unaostahili

purifier bei inafika ngapi mkuu? nafahamu ile natural purification ya kuchemsha mafuta na maji kwa moto mkali ili kuondoa harufu ya alizeti
 
mkuu asante sana kwa elimu ya mashine nilikuwa sijalifahamu hilo, mimi ninafahamu zile machine za mkono zinazofanana na za kubangua karanga na mbaya zaidi unapokwenda kununua machine label zake huwa hazioneshi efficiency ya ukamuaji. Hizo machine za india bei yake roughly inafika ngapi?

Mkuu ngoja nifanyie kazi nitakualifu
 
Back
Top Bottom