Mashine tatu za kusafisha damu Muhimbili zaharibika

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
[h=2][/h]







Mashine tatu za kusafisha damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam, zimeharibika.

Hata hivyo, uongozi wa hospitali hiyo umewataka wananchi wenye matatizo ya kibofu cha mkojo, kutokuwa na hofu ya kusitishwa kwa utoaji wa huduma kutokana na kuharibika kwa mashine hizo.

Afisa Habari wa Hospitali hiyo, Aminiel Eligaesha, alisema kitengo cha kutoa huduma kwa wenye matatizo ya kibofu kinaendelea kufanya kazi kama kawaida na hakuna haja ya kuwa na hofu hiyo.

Eligaesha alitoa kauli hiyo kufuatia kuwepo kwa taarifa kusambaa hospitalini hapo kuwa huduma ya usafishaji damu

katika kitengo hicho imesimamishwa kutokana na kuharibika kwa mashine hizo.

Alisema mpaka sasa kitengo hicho kinatoa huduma kwa kutumia mashine nne kati ya saba zilizokuwa zikitoa huduma awali.

Alisema licha ya kuharibika mashine tatu kazi ya kuwahudumia wagonjwa haijatetereka kutokana na kuchukua hatua za haraka za kuweka zamu kwa wagonjwa wanaotakiwa kupatiwa huduma hiyo.

Eligaesha alieleza hatua nyingine waliyochukua ni pamoja na kuwaelekeza wagonjwa wenye kadi za Bima ya Afya

kwenda katika hospitali nyingine zinazotoa matibabu ya aina hiyo ili pasiwepo na mrundikano wa wagonjwa.

Aidha, Muuguzi Mkuu wa Kitengo hicho, Morris Ngonyani alisema kwa ujumla kitengo hicho hupokea wagonjwa 10 kila siku na mpaka sasa hakuna mgonjwa aliyekosa matibabu.

Ngonyani alisema mashine zilizoharibika zinafanyiwa uchunguzi na wataalamu wa kizalendo waliopelekwa nje kujifunza jinsi ya utunzaji wa mashine hizo.




CHANZO: NIPASHE

Hata Hospitali ya muhimbili kuna Mafisadi wa kuharibu mashine ya kusafishia Damu ? Kazi kweli Wagonjwa watakufa wengi basi kasheshe bongo yetu



 
Back
Top Bottom