Mashindano ya Uzuri: Tunakwenda wapi ? Yana faida kweli?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,442
54,993
tumefikia mahali kuna mashindano ya uzuri katika kila kitongoji za miji mikuu Tanzania? wakati Watanzania tunashindana kwa uzuri, wenzetu wana masindano ya ufundi/sayansi, lugha/insha/mashairi, hisabati n.k.

nimeshuhudia katika nchi za wenzetu mashindano[science shows, maths contenst, ROBOTICS, spelling bee, national geographic bees, poetry] hayo yapo katika kila mji. kila nchi nilipotembelea nimeona science shows kwa wanafunzi wa madaraja mbalimbali. mashindano hayo ni nafasi ya kukuza vipaji na kuchochea udadisi miongoni mwa wanafunzi wakiwa wangali wadogo.

jamani hii ni dunia ya Sayansi na Teknolojia, siyo dunia ya Uzuri na Urembo. Watanzania tujirekebisha.
 
Ni mashindano ya UREMBO, sio ya UZURI. Urembo ni sanaa na uzuri ni zawadi toka juu. Tunaweza kumzawadia anayeshamiri kwenye sanaa ya urembo, lakini sio sawa kumzawadia mwenye zawadi kubwa ya uzuri.

We must allow ourselves to be a beehive of activities. Kwenye nchi ya watu milioni 35, kuna nafasi ya mashindano ya Hisabati, Sayansi, Mpira, Riadha, Mavazi, Urembo, Kuimba. n.k.

Sanaa ya urembo ni sehemu ya Expressive Arts. Ina nafasi Tanzania.

Augustine Moshi
 
Augustino,Jasusi,Filgga,Richard,
haya mashindano ya urembo hayana faida ya muda mrefu[long term benefits] kwa nchi changa kama yetu.

hakuna taifa hata moja lililoendelea kwa kuweka kipaumbele katika mashindano ya urembo. kwa upande mwingine yako mataifa[japan,india,korea] yaliyopiga hatua kwa kuwekeza na kukuza vipaji vijana wao katika sayansi, teknolojia, hisabati,ufundi n.k.
 
Jokakuu,

Hakuna vile vile taifa ambalo limeendelea kwa kuweka kipaumbele kwenye mpira wa kikapu. Kwa hivyo tuache mpira wa kikapu?

Kukuza Expressive Arts, na Arts kwa ujumla, kuna faida kwa taifa. Ni muhimu lakini tuzingatie mashindano ya urembo na sio ya uzuri. Mashindanoya uzuri yanaweza kuwa morally objectionable.

Taifa huwa na mambo mengi, ikiwa na pamoja na expressive arts. We need not ban things unecessarily.
 
Augustino,
sijapendekeza kwamba mashindano ya urembo yafungiwe. mapendekezo yangu ni kwamba kuwe na variety katika kushindanisha na kukuza vipaji vya vijana wa Tanzania. tuendeleze na vipaji vingine haswa, ufundi, teknolojia,mahesabu, sayansi, lugha n.k.

tujaribu kuangalia dunia inaelekea wapi, na ni jinsi gani Watanzania tunawaandaa vijana wetu kuweza kuwa competitive kesho na keshokutwa.
 
Back
Top Bottom