Mashindano ya Mamiss na njaa za wabongo

Mgoyangi

Senior Member
Feb 6, 2008
184
9
Leo Asubuhi nilikuwa naangalia kipindi cha Tuongee nikaona mshiriki mmoja akikandia mashindano ya urembo.

Kwamba yanawazalilisha wanawake licha ya viongozi na wanaharakati kuyashabikia, lakini pia hayana maana kwa sababu anatafutwa mrembo wa Kitanzania kwa sifa za kizungu.

Pia kwamba waandaaji wanaganga njaa na kwamba kuna hila katika kutoa zawadi kwani kuna rushwa katika kutafuta mshindi na zawadi zinazotolewa sehemu yake hurudi kwa waratibu.

Kwamba hicho kinachodaiwa umiss utalii, hakitangazi utalii wa kitanzania kwa sababu hata nywele za washiriki huwa ni yale maplastiki ya kuvaa ili washiriki waonekana kama wazungu. Pia akasema Mwendo wa Nyau -- cat walk -- wapi na wapi kwa wadigo na kuhusu uwezo wa kuzungumza washiriki wanatumia kiswahili chenye rafudhi ya kizungu.

Kikubwa zaidi ni lile shairi lake ---

Na hebu waone, wakapite mbele ya kadamnasi,
wamekondeana kama vi bi Kikagula Mchawi
Na angalia midobo yao ilivyo miekundu,
Hii inanikumbusha hadith za alfu lela ulela
Juu ya Jini Makata mnyonya damu.

Mshiriki na mratibu wa Miss Utalii Bwana Chipungahelo, alikuwa akipinga haya yote.

Hivi ni vema kweli kuiga kila kitu? Kisa kimetoka kwa wazungu.
 
Back
Top Bottom