Mashindano ya kunywa pombe yaua

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MKAZI wa kitongoji cha Sumbawanga ya Asili katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani hapa Moses Kayange (37) amefariki dunia baada ya kunywa paketi 25 za pombe kali aina ya 'Double punch' baada ya kuahidiwa zawadi ya fedha na wenzake.

Inadaiwa kuwa Kayange aliahidiwa na wenzake kuwa angepewa Sh 10,000 endapo angemaliza kunywa paketi 30 za pombe hiyo kali, inayotengenezwa kutokana na mananasi.

Paketi moja ya pombe hiyo kali inayotengezwa nchi jirani ya Zambia mjini Ndola, ina ujazo wa mililita 60 na asilimia 45 za kilevi na inauzwa Sh 250 kwa paketi kwa bei ya rejareja.

Tukio hilo lilitokea Jumatatu ya Pasaka mchana eneo la Mazwi mjini hapa ambapo Kayange na wenzake hao walikuwa wakinywa katika duka la kilevi wakisherehekea sikukuu ya Pasaka.

Kwa mujibu wa ndugu zake wa karibu, Kayange alikuwa ni kibarua wa kujaza mchanga kwenye magari makubwa.

Inadaiwa wakati wakinywa, Kayange aliwatambia wenzake kuwa yeye ni bingwa wa pombe kali na kwamba hakuna wa kumfikia mji mzima wa Sumbawanga kauli iliyowaudhi wenzake.

“Baada ya tambo hizo yalitokea mabishano makubwa kati yetu, tukaamua tuchangishane pesa ili apatikane bingwa, ndipo tulipopata pesa za kutosha tukanunua paketi 60 za Double punch na kubakiwa na Sh 10,000 ambazo tulizifanya zawadi kwa atakayeibuka kidedea.

“Hivyo tukaenda kushindania kwenye banda la kupumzikia abiria eneo la Uwanja wa michezo wa Mandela mbali kidogo na duka tulipokuwa awali,” alisema shuhuda ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Alisema kabla ya mashindano hayo, Kayange na wenzake walikuwa wameshakunywa pombe ya kienyeji iitwayo Msimamishe. Inadaiwa Kayange alipomaliza paketi 20 alianza kutokwa jasho jingi huku akishangiliwa na wenzake wakimhimiza aendelee kunywa … akajitutumua.

“Alijimiminia kwenye bilauri paketi zingine tano hivyo kuwa 25, alipomaliza tu kunywa ghafla akaanguka, akapoteza fahamu,” alisema shuhuda mwingine.

Inadaiwa kuwa wenzake walitaharuki na kupiga kelele kuomba msaada, umati ukakusanyika eneo la tukio na kujitokeza wasamaria waliokodi teksi na kumkimbiza nyumbani kwa wazazi wake eneo la Sumbawanga Asili.

Akizungumza na gazeti hili msibani hapo mdogo wa marehemu, Patrick Kayange, alikiri kuwa si mara ya kwanza kwa marehemu kujihusisha na mashindano ya unywaji.

“Siku ya tukio nilikuwa safarini hata wenzake waliponipigia wakiniomba niwape usafiri nilipuuza nikijua kuwa ni yale yale matatizo yake ya unywaji wa kupita kiasi ... we acha, kaka alikuwa anakunywa alikuwa anamaliza kreti ya bia peke yake ... tulimwekea vikao vya wanandugu mara kadhaa tukimkanya aache unywaji wa pombe kupita kiasi, lakini wapi alikaidi,” alisema Patrick.

Alisema kaka yake aliaga dunia juzi saa 11 jioni na maziko yake yalifanyika jana.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi unaendelea na hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa.
 
Shetani kavuna. Ulitaka iweje? Kiongozi wa dini wakati wa maziko aliwaambia wamwombee ili alazwe mahali pema peponi? Kama ndiyo, ni kipofu. Waebr9:27
 
Shetani kavuna. Ulitaka iweje? Kiongozi wa dini wakati wa maziko aliwaambia wamwombee ili alazwe mahali pema peponi? Kama ndiyo, ni kipofu. Waebr9:27
 
"Baada ya tambo hizo yalitokea mabishano makubwa kati yetu, tukaamua tuchangishane pesa ili apatikane bingwa, ndipo tulipopata pesa za kutosha tukanunua paketi 60 za Double punch na kubakiwa na Sh 10,000 ambazo tulizifanya zawadi kwa atakayeibuka kidedea.

Kweli shetani ni mbaya yaani badala ya kuwekeza hiyo pesa kwenye mambo muhimu ili aondokane na taabu ya kibarua cha kuchimba mchanga yeye anaitumia kununulia paketi za bia ambazo zinamletea mauti.

Kwakweli namshukuru Mungu sikuwahi kuwa mnywaji wa pombe na sitaitumia. Yaani mara nyingi huwa simshukuru Mungu ninavyotakiwa kwasababu wema na fadhili zake kwangu ni nyingi mno. kuna mambo mengi tuu aliyoniepusha nayo mfano nina ndugu zangu waliokubwa na kiu ya pombe kwakweli japokuwa wanadai wanaburudika wakinywa lakini kiukweli wanateseka yaani ni kama utumwa fulani hivi.

Sifa na utukufu ni wake Bwana kwakuwa yeye ndiyo taa ya miguu yangu, nitampa sifa siku zote za maisha yangu. Amen


"Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu."

Zaburi 119:105
 
Back
Top Bottom