Mashimo barabara za Dar es Salaam

Mutwale

Member
Oct 20, 2010
67
19
Ukipita Barabara ya Uhuru ambayo hapo awali ilitumika kupitisha viongozi wakitafa, nakumbuka Mzee Mandela, Walter Sisulu, Papa John Paul(Mwenyeheri) na wengine wengine wengi; utakutana na mahandaki kuanzia Buguruni pale Kiomboi Kisiriri, polisi, Rozana ndo balaa maana kuna mshimo wa kina kirefu kwani pia umejaa maji! Malapa, Bungoni, kisha Kariakoo Shule ya Uhuru karibu na Round about ya Msimbazi rd., Kisha kwenye mataa ya makutano ya Uhuru na Bibi Titi! Shimo lingine liko pale Mtaa wa Jamuhuri na Azikiwe, mbele kabisa ya NMB House, pembeni mwa Benjamini Mkapa Tower! Mashimo yote haya yako katika kati ya Jiji la Dar es Salaam, aibu iliyoje?

Je manispaa zinazo husika hazioni uozo huu? na kama barabara za katikati ya Jiji, (Tanzania) je barabara za Kisukuru, Mwitongo, Rubya, Litumbadyosi, Kiwele, au Kifyulilo ambazo hazionekani mbele ya macho ya watawala atazijenga nani!

Je ile kodi ya Road License inakwenda wapi? je kuna sababu gani ya kulipa Road License na ilihali asilimia 95 linapopita gari lenye stika hiyo ni mashimo matupu?

Chonde chonde wanasi hasa, acheni longo longo, za kujivua Magamba fanyeni kazi, kujivua gamba kwa ukweli ni kutumia kodi zetu kwa malengo kusudiwa na si kuzunguka nchi na kujitambulisha, kwani hakutatusaidia.

Ingefaa misafara ya rais irejeshwe tena kupitia barabara ya uhuru! pengine itasaidia, pia Rais anapowaambia watendaji wake watoke maofisini, ingefaa naye siku moja afanye ziara ya ghafla maeneo ya mitaa ya Sinza kwa wajanja na viunga vyake ajionee, hapo atajua kama kweli wamejivua gamba, au wanapaswa kujiua gamba! watanzania wa leo tumechoka siasa, kwani hazitusaidii bali walio karibu na hao wakuu wa Kaya.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Mungu kaamua kuimbua CCM mwaka huu maovu yote yataonekana, serikali haina pesa, mvua zimekuja kwa wingi ili kuharibu barabara za jiji na kwa kuwa serikali haina pesa hawataweza kukarabati barabara.Tunamshukuru sana Mungu kwa kuleta janga, ili madhambi ya CCM yajidhihirishe mbele ya macho ya walipa kodi.CCM mnalo
 
Kaa tayari kuna kodi ya makazi zinakuja kwa waheshimiwa wa halmashauri za Dar es Salaam. Kuna handaki kubwa limechimbwa kwenye makutano ya barabara ya Tunisia na Ali Hassan Mwinyi kiasi cha kuzuia matumizi ya makutano hayo. Mashimo kadhaa waliyoyachimba kwenye barabara nyingine bado hawajayafukia vizuri, mtu anaenda kuweka kifusi cha udongo kuziba shimo kwenye barabara ya lami. Mifano ipo mingi, kuanzia bara ya zamani ya Bagamoyo karibu na daraja la Mlalakuwa, Buguruni, Mchepuko wa barabara ya Morogoro kwenda ya Shekilango, n.k

Halmahsauri zetu hizi ni mtihani kweli kweli
 
Hayo mashimo wanayaita 'ng'ombe wa maziwa' ni mradi wa manispaa na jiji...
 
Hivi kwenye serikali hii ni katika sekta ipi ambapo unaweza ukasema inafanya vizuri japo kwa 50%???
 
Back
Top Bottom