Mashehe wawataka madaktari kusitisha mgomo

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Wadai wana haki ya kuishi kama haki ya kibinadam, na wanadai kuwa iweje utumie haki ya mtu ya kuishi kudai haki yako?

Kwa hari hiyo madaktari hawawatendei haki watanzania na wanawataka warudi kazini na watumie njia ya mazungumzo kudai haki zao.

Source: TBC1 Habari, June 30, 2012 saa 2 usiku
 
Jopo hilo lililongozwa na katibu wa masheikh hao sheikh Matata wamesema swala la madaktari linazungumzika lakini maisha ya watanzania yanayoendelea kupotea nikuwakosea watu hao haki yao ya msingi yakuishi.
 
khalifa hamisi na idd simba sii masheikh,ni mafisadi wanaotumiwa na ccm kutugawa waislam!HILO SII TAMKO LA WAISLAM
 
Wadai wana haki ya kuishi kama haki ya kibinadam, na wanadai kuwa iweje utumie haki ya mtu ya kuishi kudai haki yako?

Kwa hari hiyo madaktari hawawatendei haki watanzania na wanawataka warudi kazini na watumie njia ya mazungumzo kudai haki zao.

Serikali si iwe na mazungumzo nao kwani wamekimbia?
 
UAMSHO vipi, wameshatulia, au madai yao hayazungumziki,? Sensa vipi wameikubali? mahakama ya kadhi vipi ahadi yao imetekelezwa kama ahadi yake JK? Waanze na mambo yanayo wahusu bana.
 
khalifa hamisi na idd simba sii masheikh,ni mafisadi wanaotumiwa na ccm kutugawa waislam!HILO SII TAMKO LA WAISLAM
Afadhali umenipa mwanga maana nilikuwa nataka kuporomosha tusi la karne! Serikali ndiyo ilaumiwe na wala si madaktari!!!
 
Serikali ya CCM sikivu , Mashehe jiulize mmedai mahakama ya Kadhi kwa muda gani.
Mara swala hili liko mahakamani ?si mngoje mahakama itoe shururi la kurudisha madaktari kazini , Kwa nini mnakuwa vuvuzela wa magamba
 
Wangetolea tamko swala la sensa kwanza, je wanatueleza nini sisi waumini. Tukubali kuhesabiwa ama tuendelee na maandamano siku hiyo. Pili huu mgogoro wa madaktari wangetoa tamko kwa pande zote mbili (serikali na madaktari) ingekuwa rahisi sisi kuwasikiliza na kuwaamini kuwa ni tamko lao halisi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom