Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashangingi yaitafuna serikali Tanzania

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Lunyungu, Apr 18, 2007.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2007
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 9,908
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Mashangingi yaitafuna serikali Tanzania

  *Yatumia Sh33bilioni kwa mwaka

  Na Ramadhan Semtawa

  WAKATI matumizi ya Serikali yakiwa yamezidi bajeti kwa Sh 900 bilioni, imebainika gharama kubwa za kuendesha magari ya kifahari maarufu kama mashangingi ni moja ya chanzo kinachochangia hali hiyo.

  Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba, mashangingi yanayotumiwa na viongozi wa serikali yapo 800 yanatumia zaidi ya Sh33 bilioni kwa mwaka ikiwa ni matumizi ya mafuta na gharama za kuyafanyia mategenezo.

  Kwa mujibu wa takwimu zilizopatikana, magari hayo yanatumia wastani wa lita 300 kila moja kwa wiki, hivyo hutumia lita za mafuta 240,000 kwa kipindi hicho kwa magari yote hayo. Kwa wastani bei ya sasa ya mafuta ya diseli ni sh 1200 kwa lita hivyo magari hayo yanatumia Sh1.152 bilioni kwa mwezi. Uchunguzi umegundua kuwa gharama za kulifanyia mategenezo kwa mwezi ni Sh2 milioni kila gari hivyo gharama za kuhudumia magari hayo kwa mwezi ni Sh1.6 bilioni.

  Ukijumlisha gharama za mafuta na mategenezo kwa mwezi ni Sh 2.752 bilioni na kwa mwaka ni kiasi cha Sh33 bilioni. Kiasi hicho cha matumizi kingepungua iwapo baadhi ya viongozi ukiachia rais, waziri mkuu na makamu wa rais wangetumia magari ya kawaida.

  Kati ya magari hayo, 540 ni ya viongozi wa Serikali Kuu wakiwamo ofisi ya rais, ofisi ya waziri mkuu, makamu wa rais, mawaziri, manaibu mawaziri, makatibu wakuu. Orodha hiyo ya serikali kuu imezingatia, makatibu wakuu 27, manaibu wao 27, maafisa utumishi (Ma Dap) 27, na wakurugenzi wanne kila wizara na sehemu nyingine wakurugenzi wasaidizi, huku Ikulu, ofisi ya makamu wa rais na ya waziri mkuu, kwa pamoja zikiwa na magri hayo yasiyopungua 40.

  Mengine hutumiwa na watendaji wakuu wa mashirika na taasisi za serikali, wakati kwa upande wa Tamisemi ni kuanzia wakuu wa mikoa 22, makatibu tawala wa mikoa 22, makatibu tawala wa wilaya, wakurugenzi watendaji wa wilaya na wakuu wa wilaya 104.

  Wakati gharama hizo zikionekana kuwa mzigo kwa walipa kodi, Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, ameliambia Mwananchi: "Tena naomba uninukuu vizuri, mawaziri wataendelea kutumia magari yanayoendana na hadhi yao, waziri hawezi kutembelea Vokswagen (Bito)".

  Uchunguzi umebaini kuwa gharama hizo zimekuwa zikiongezeka maradufu katika siku za hivi karibuni kutokana mawaziri, manaibu mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu tawala wa mikoa na wilaya kutotulia ofisini kutokana na ziara wanazofanya katika maeneo mbalimali.

  Pia imebainika kwamba, gharama za kuendesha magari hayo zimekuwa ni mzigo kwa walipa kodi kutokana na baadhi ya mawaziri kutofanya kazi vizuri huku baadhi ya magari yakionekana kuranda randa kwenye mabaa nyakati za usiku na mwisho wa wiki. Akizungumzia zaidi kuhusu magari hayo, Chenge alisema serikali haijafikia uamuzi wowote wa kupiga marufuku magari hayo ya kifahari ambayo yeye anayaita kuwa ni ya kawaida.

  "Kwanza si magari ya kifahari, wewe ndiye unayeyaita hivyo, ni kwa sababu ya umasikini wetu tu, lakini lazima waziri atembelee gari lenye hadhi yake," alisisitiza Chenge.

  Hata hivyo, aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo kabla ya Chenge, Basil Mramba aliwahi kukaririwa na gazeti hili kuwa mashangingi ni mzigo mkubwa kwa serikali na kwamba inafanya mipango ya kusitisha ununuzi wa magari hayo.

  Alipoulizwa haoni huo umasikini wa nchi yetu ndiyo ambao ulitupasa kuacha kununua magari hayo, alijibu, " kwanza, matumizi ya serikali hayawezi kuzidi kwa ajili ya magari haya", na kuhoji:

  "Hivi siku za nyuma katika serikali zilizopita mafuta yalikuwa yakitolewa lita 50 kwa wiki, nchi yetu ilipiga hatua gani kubwa katika nyanja za maendeleo?" Chenge alipoelezwa mfano, wa serikali ya Mwalimu Nyerere kwamba iliweza kujenga viwanda na mashirika makubwa ambavyo watawala wa sasa wanayauza ovyo, alijibu tena, " wewe sikia, haya mafuta ya magari hayawezi kukuza uchumi, cha msingi watu fanyeni kazi kwa bidii, tushirikiane kutekeleza ilani ya chama na mipango ya maendeleo ya serikali."

  Hata hivyo, Chenge alisema serikali itachukua hatua kwa wale watakaobainika kutumia magari hayo katika mabaa na nyakati zisizo za kazi.

  Wakati huo huo; Shirika la Fedha Duniani (IMF) limeishauri Serikali ya Tanzania kubana matumizi yake kwa kuyaelekeza fedha kwenye vipaumbele muhimu vya nchi kama afya, miundombinu, elimu na maji.

  Ushauri huo ulitolewa jana na Mwakilishi Mkazi Mwandamizi wa IMF nchini, Dk David Robinson, alipokuwa akijitambulisha kwa wanahabari jijini Dar es Salaam, katika ofisi ya shirika hilo.

  "Siwezi kulitolea maoni kwa undani kwani nahitaji muda wa kujifunza zaidi, lakini ni muhimu Serikali ikadhibiti matumizi yake ya fedha na kuzielekeza katika sekta muhimu kama afya, miundombinu, elimu na maji," alishauri Mwakilishi huyo wa IMF.

  Dk Robinson alisema hayo wakati akijibu hoja ya wanahabari juu ya ripoti ya IMF kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania, ambayo imeifagilia Serikali kuwa iko makini katika udhibiti wa fedha, wakati ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeonyesha kuwepo kwa mushkeli katika matumizi.

  Ripoti hiyo ya CAG ya hivi karibuni inaonesha kwamba Serikali imekuwa na matumizi makubwa kwa kutumia ziada ya sh900 bilioni miezi minne kabla ya kuisha kwa mwaka wa fedha. Taarifa ya CAG kwa mwaka 2005/06, inaonesha kuongezeka kwa matumizi ya kawaida kutoka Sh2,138,860,343,786 mwaka 2004/05 hadi Sh2,732,455,841,323 mwaka 2005/06.

  Taarifa hiyo inasema, fedha za matumizi ya miradi ya maendeleo zimepungua kutoka Sh850,533,139,955 mwaka 2004/05 hadi Sh844,103,204,420, huku deni la taifa la nje likikua hadi kutokaSh5,548,446,077 hadi Sh5,772,620,992 katika kipindi hicho na kumfanya Rais Jakaya Kikwete kuitisha mkutano na watendaji waandamizi wa serikali kuijadili katika kikao hicho kilichofanyika Dodoma, ambapo aliwatahadharisha watendaji watakaorudia makosa hayo watatimuliwa kazini.

  Takwimu zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Machi mwaka huu, zinaonesha tayari katika matumizi hayo kuna ongezeko la asilimia 5.6 ya pato la taifa, badala ya asilimia 5.1 ya pato la taifa kama ilivyokuwa imekadiriwa kwenye bajeti ya mwaka 2006/07.

  Kutokana na kuongezeka kwa matumizi hayo, taarifa ya hiyo ya BoT inaonyesha mpaka Februari mwaka huu, tayari kumekuwa na pengo la Sh978.8 bilioni.

  Akizungumza zaidi, Dk. Robinson alieleza kwamba kwa sasa jumuiya ya nchi wahisani imekuwa ikielekeza zaidi misaada yake ya fedha kwenye bajeti kuu za Serikali ili ziwe na uhuru wa kupanga vipaumbele vyake badala ya kuamuliwa.

  Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo ya Februari mwaka huu Bodi tendaji ya IMF imeridhia kuipa Tanzanai fedha zaidi baada ya kuridhishwa na inavyotekeleza Mkakati wake wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umasikini (MKUKUTA) katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita .

  Kwa hali hiyo Tanzania imefunzu kupewa dola za kimarekani 4.2 milioni kwa ajili ya kuendeleza jitihada hizo. Kiasi hivyo kinafanya jumla ya fedha ambazo Serikali ya Tanzania itazipata kwa ajili ya mpango huo kufikia dola za kimarekani 29.4 milioni.

  Lengo la wahisani hao ni kuona kwamba uchumi wa Tanzania unakuwa hasa katika kujenga uwezo wa matumizi bora ya fedha, kuimarisha mchango wa sekta ya fedha katika maendeleo, kuwa na sera za fedha zinazotekelezeka na mazingira bora ya biashara.

  Ripoti hiyo imeonesha kwamba katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Uchumi wa Tanzania umekuwa ukikuwa vizuri na kufanikiwa kushusha mfumko wa bei pamoja na kujiwekea hakiba kubwa ya fedha.
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Apr 19, 2007
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 8,090
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Priorities za serikali yetu hizo; kulipia gharama za elimu ya juu kwa raia wanaona kero lakini kulipia gharama za kuendesha mashangingi wanaona swafi.
   
 3. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2007
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Kwa mahesabau hayo...Shs Bil 33 ni sawa na USD Mil 33. Nikigawanya kwa magari/mashangingi 800: 33,000,000/800 = 41,250 USD

  Kila Shangingi moja linatumia wastani wa USD 41,250 kila mwaka..!!!


  Mungu Ibariki Tanzania.
   
 4. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2007
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,819
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kama mahesabu yako ni sawa,Je serikali ingefikiri kupunguza gharama kwa hilo angalau nusu yake kwa nunuu magari mbadala ,nusu iliyobaki kwa mwaka ineweza kusomesha watanzania wangapi tena bure na kama ni mkopo ingekopesha wangapi kwa kiwango cha asilimia 100.
  Kupanga ni kuchagua wao wamechagua kutoipa elimu kipau mbele ila kutoa kipaumbele ktk kugharimia usafiri wao.
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2007
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Kwa nchi yetu ilivyo mimi sioni magari mbadala wa haya mashangingi..!!

  Tatizo hapo ni jinsi hizo Bil 33/= zilivyotumika..siamini kama zote zimetumika kugharamia hayo magari. Magari yametumiwa kama kisingizio au kama ni kweli basi inaonyesha ni jinsi gani usimamizi mbaya wa hayo magari ulivyo.

  Kutumia USD 41,250 kwa mwaka kwenye gari inayogharimu Est USD 70,000 ni wizi wa mchana kweupe.

  Mungu Saidia Wadanganyika
   
 6. J

  Joo Wane JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2007
  Joined: Mar 14, 2007
  Messages: 343
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Wakati wa enzi ya Marehemu baba wa taifa serikali ilikuwa inatumia zaidi landrover 109 "mandolin" na baadaye Mzee wetu Mwinyi alipoanza serikali ilikuwa inatumia landrover 110. Gari zote hizo gharama yakuzinunua na kuziendesha ilikuwa sio ya kutisha. Kwa sasa serikali inaweza kabisa kuuza mashangingi (sio lazima wayauze yote wanaweza kubakisha machache sana) na kutafuta gari mbadala (sio lazima landrover sasa hivi kuna aina nyingi sana za magari) zenye gharama nafuu na zinazoweza kuhimili barabara zetu za mijini na vijijini. Viongozi wetu mara nyingi wakifanya kitu chochote (hasa kikiwa kibaya) wakiulizwa huwa wanajibu tumeiga kwa wenzetu na Tanzania sio kisiwa, kwa hiyo na hili suala la magari ya serikali wamuige Nkurunziza aliyeuza mashagingi yote. Serikali ikifanya hivyo itaokoa pesa nyingi na kuzitumia katika sekta nyingine kama elimu, afya n.k. Sio lazima waje WB, IMF waje watushauri kila kitu kinachohitajika ni uwezo tu wa kuthubutu.
   
 7. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #7
  Apr 19, 2007
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 9,908
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Watanzania na waafrika bwana . Ikifikia kwenye hili wanasema tumeshauriwa na WB na IMF mbona hao hao wakija na ushauri juu ya Zimbabwe na demkokrasia Afrika wanaikataa kwamba si kila jambo waambiwe ?Kwa nini kwenye matumizi tena mabaya ya kuangamiza Nchi wanawasiliza wazungu na kuiga kwa wenzetu wasi ige demokrasia na kuheshimu utawala na kutumia less money za walipa kodi ?
   
 8. J

  Joo Wane JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2007
  Joined: Mar 14, 2007
  Messages: 343
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ndugu yangu Lunyungu,

  Naomba nitoe ufafanuzi.
  Niliposema kuwa sio lazima waje IMF, WB waje watushauri kila kitu nilikuwa nina maana kuwa viongozi wetu hawawezi kusikiliza na kuufanyia kazi ushauri wowote unaotolewa na wananchi hata uwe wa maana kiasi gani, na hata hawaumizi vichwa kubuni mbinu za kupunguza matumizi ya serikali ambayo yanazidi kuongezeka kila siku. Na hata majibu ya Chenge yanaonyesha mwanzoni mwa habari hii. Lakini wakishauriwa na WB, IMF kitu chochote kile hata kikiwa hakina maana wanatekeleza haraka sana.
   
 9. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2007
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Hata waje watumie magari kutoka wapi ndugu yangu...iwapo spea ya Shs 100,000 inaandikwa kwenye vitabu imenunuliwa kwa Shs 1,000,000 gharama zitakuwa pale pale kwenye Bil 33/=. Magari wala sio tatizo...hizo tabia ya kuongeza 0 ndio tatizo na hilo dawa yake ni watu kumwaga unga. Lakini badala yake JK anawaita Dodoma na kuwaambia tabia hii ikome..!!
   
 10. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #10
  Apr 19, 2007
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 4,055
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Kama ni nyoka, umemgonga kichwani! That is a very good summary of our leaders' double standards!
   
 11. Nyangumi

  Nyangumi JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2007
  Joined: Jan 4, 2007
  Messages: 599
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lunyungu,ungelikuwa karibu ningelikununulia kimbo moja ya kangara upate kujiburudisha.Unatoa mifano ambayo inagonga kwenye utosi.
  Ningeongeza tu kwa kusema hwa viongozi wa Tanzania na Africa hawako kwa maslahi ya nchi zao. Hukataa ushauri wa WB au IMF ambao unaathiri maslahi yao mfano demokrasia, na hupokea ushauri ambao unawafaidisha wao binafsi, sio nchi.Wanapokuwa madarakani wanaiona nchi kama personal property na kuwa hakuna mwingine mwenye haki ya kutawala isipokuwa wao tu(wateule!!!!).
  Nakumbuka kikao cha kwanza cha 1995 cha bunge, hoja ya kwanza iliyoletwa na mbunge mmoja ni kulitaka mbunge kupitisha mswaada utakaowafanya wapigiwe Saluti, kuongezwa posho na kuweza kufikia kwenye hotel ya Five star kama wabunge wa Uingereza!!Wakati huo huo walitoa tamko la kuwalaani Madaktari waliokuwa wakidai nyongeza za mishahara. Huwezi sikia mbunge akisema tunataka mswaada utakaoifanya nchi i-practice demokrasia yenye uwazi kama ya Uingereza.
   
 12. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 3,483
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Haya ni mafuta mengi sana kwa wiki moja, lita 50 kwa siku moja - Ni biashara gani inafanyika? Au wamekuwa daladala siku hizi? Je ni kwa nini kiwango hicho kiliongezwa kwa asilimia 600 (600%)?

  Je tunahitaji VT mwingine aje kutoka South Korea?
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2007
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 12,127
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Yebo Yebo,
  Hapa Marekani ni Rais, Makamu rais, Waziri wa mambo ya nje na Waziri wa Ulinzi tu ndio wanaopewa magari maalumu. Mawaziri wengine wote pamoja na wabunge wanatumia magari ya binafsi. Wengine tunapigana nao vikumbo kwenye main roads wakijiendesha wenyewe kwenda kazini. Hamna cha petrol allowance au maintenance allowance. Na hawa wameendelea. Sembuse sisi ambao ni omba omba tu!
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Apr 19, 2007
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 8,090
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Niliwahi kufanya kazi kama fundi kwenye mojawapo ya viwanda vya pale Morogoro. Siku moja tukapeleka gari kwenye karakana ya binafsi ili ikabadilishewa kitu ambacho tusingeweza kubadilisha kwa nyezo tulizokuwa nazo kiwandani. Tukaambiwa gharama ilikuwa Shs240. Tuliporudi kwa mhandisi mitambo, yeye akaorganize na ile karakana binafsi ili invoice iandikwe kwa Shs 500. Baada ya kutayarisha LPO na kuipeleka kwa technical Manager, ikafanyiwa marekebisho na bei ikabadilishwa kuwa Shs 1000. Hata hivyo baada ya kuingia kwenye idara ya mahesabu, malipo ya mwisho yaliyofanyika yalikuwa ni Shs 2500; hiyo ilikuwa ni mwaka 1983. Kwa hiyo tabia hii ya ku-inflate malipo ilianza zamani sana, na ilitakiwa kwa sasa hivi serikali iwe na utaratibu wa kuidhibiti.
   
 15. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2007
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 1,297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  kichuguu,
  usitake ni cheke, unanikumbusha jinsi masesenger na masecretary wanavyo haribu photocopy machine ili wapeleke kazi mtaani.bongo ukisimuliwa mambo yake utafikiri hutani.ndio maana watu hawalalamiki hata kidogo kuhusu hali ngumu ya maisha,kila kukicha wanakwenda kazini na kurudi.utakuta mtu ni mesenger tu lakini ana nyumba zaidi ya moja.anasomesha watoto st mary na kwingineko lakini kipato chake ni tofauti na matumizi yake.
  Kutokana na hali hii ndio maana serikali imejenga kiburi na kufanya kila kitu kwa jinsi inavyojisikia.
   
 16. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #16
  Apr 19, 2007
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,819
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwahiyo kwako wewe Gari ni shangingi tu hata kama si cost effective katika ununuaji na uendeshaji wake.
  Tulichoelezwa hapa ni gharama za mafuta zinazosababishwa na magari hayo,kwahiyo tunasema wanunue magari mbadala ambayo yatapunguza utumiaji wa mafuta kwa kiwango kinachotugharimu sasa.hayo matatizo mengine uliyoyataja vile vile wanayoyasababishwa sheria ichukue mkondo wake.
   
 17. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #17
  Apr 19, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 3,483
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Picha kwa hisani - Michuzi Blog.

  Wahusika wa matatizo yanayoendelea Bongo kwa namna moja au nyingine, Je tuwafanyaje sasa?
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2007
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 12,127
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Dua,
  Hawa lazima tuwatafutie dawa. Sasa hivi ni kama they are getting away with murder.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 46,508
  Likes Received: 3,537
  Trophy Points: 280
  Ikulu sasa yaushtukia mzigo wa mashangingi

  *Yaagiza tathmini ya gharama zake ifanywe

  Na Ramadhan Semtawa

  BAADA ya kilio cha muda mrefu cha wananchi juu ya gharama kubwa za magari ya kifahari, maarufu kama Mashangingi, serikali sasa imeanza kuyageukia magari hayo kwa kujaribu kuyadhibiti ili kuokoa matumizi makubwa ya fedha za umma.

  Magari hayo ya kifahari yanayokadiriwa kufikia kiasi cha 800 serikalini, ikiwa ni yale ya Serikali Kuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) yanakadiriwa kutumia zaidi ya Sh33 bilioni kwa mwaka kama gharama za uendeshaji wake.

  Waziri wa Fedha, Zakia Meghji na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo, wamethibitisha kwa nyakati tofauti juu ya mpango huo wa Serikali wa kutekeleza agizo kutoka Ikulu juu ya udhibiti wa magari hayo.

  Awali chanzo cha habari kutoka serikalini, kilisema Ikulu imeagiza uhakiki wa magari hayo ufanyike kuanzia Serikali kuu na kwamba kazi hiyo ilikamilika Mei 11,mwaka huu ikiwa ni awamu ya kwanza iliyochukua wiki mbili.

  "Serikali imeanza kuchukua hatua za kudhibiti matumizi yake, ikiwa ni pamoja na kuangalia gharama za kuendesha mashangingi, agizo kutoka Ikulu limeelekeza kila wizara kufanya hivyo," kilisema chanzo hicho na kuongeza:

  "Jukumu hilo lipo chini ya Wizara ya Miundombinu, aliyekabidhiwa jukumu hilo ni Chambo (Omar, Naibu Katibu Mkuu)."

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, hata awamu ya pili ya uhakiki katika ngazi ya Serikali za Mitaa nayo imekamilika na kwamba magari yote ya kifahari yakiwamo ya wakurugenzi watendaji wa halmashauri yamehakikiwa.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, Serikali inaangalia pia namna itakavyoweza kupunguza idadi ya magari hayo yanayonunuliwa katika vipindi tofauti.

  Waziri wa Fedha, Zakia Meghji alikiri kuwapo kwa uhakiki wa mashangingi akisema :" mpango huo uko katika utekelezaji".

  "Suala hilo linafanyiwa kazi sasa hivi, subirini mtaona, " alijibu kwa kifupi Meghji, lakini akikiri suala hilo ni agizo kutoka Ikulu.

  Kwa upande wake, Chambo ambaye jukumu hilo liko chini yake, aliliambia Mwananchi kwamba tayari uhakiki wa magari hayo na gharama zake umekwishamalizika.

  "Kila kitu tayari, tulianza na wizara na tukaenda na upande wa Tamisemi ambako nako tayari," alithibitisha Chambo ofisini kwake juzi.

  Alithibitisha kwamba lengo la mpango huo ni sehemu ya mikakati ya serikalai kubana matumizi.

  Chambo alipoulizwa kama kuna uwezakano wa kuuza baadhi ya magari, alijibu, "halafu viongozi watembee na nanini, ni kweli tunaangalia jinsi ya kupunguza gharama lakini si kuuza, haijaamuliwa hivyo kwanza."

  Kuhusu kuwepo wakurugenzi wasaidizi wenye kutembelea magari hayo alijibu, " kwa kawaida hawa hawamo katika bajeti ya kupata magari hayo, hakuna bajeti inayoweza kuidhinishwa ya kutaka mkurugenzi masaidizi apate shangingi."

  Serikali ina magari ya kifahari yanayokadiriwa kufikia 800 ambayo yanatumiwa na mawaziri na naibu mawaziri, makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu, wakurugenzi wanne kila wizara, Ikulu (Ofisi ya Rais na Makamu), Ofisi ya Waziri Mkuu na hata wakurugenzi wasaidizi wa wizara.

  Wengine wenye magari hayo ni wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu tawala wa mikoa na wilaya, na wakurugenzi watendaji wa wilaya.

  Tathimini ya kiuchunguzi inaonyesha kuwa gharama za kufanyia matengezo gari moja kwa mwezi ni kati ya Sh1.5 hadi Sh2 milioni, huku mafuta ikiwa ni zaidi ya Sh2.5 milioni kwa kila gari.
   
 20. S

  Samvulachole JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2007
  Joined: Oct 22, 2006
  Messages: 731
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  unazungumzia IKULU hiyo hiyo ilyokataa kuwatambua hawa WAJUKUU WA NYERERE ambao wanaishi kama WAKIMBIZI huko UKRAINE au IKULU YA ZANZIBAR? au?