Mashangingi ya CHADEMA!!

nazungumzia "consistency" ya chama kwenye mambo wanayoyapigania wakati wa kampeni. Kusema akili yangu mbovu hakuondoi ukweli kwamba hata hayo mashangingi ya chadema yananunuliwa na kwa kodi za wananchi. Wewe hujui kuna baadhi ya wabunge kabla ya kuwa wabunge hata baiskeli walikuwa hawana uwezo wa kununua.

Unajisahaulisha kwamba wabunge wote walipewa mkopo wa shilingi milioni 90 na ofisi ya bunge kwa ajili ya kununulia magari yao?

vipi huo mkopo wa milioni 90 analipa nani serikali au mbunge? Kama ni mbunge then ni pesa zake binafsi lakini kama ni serikali ndo inalipa huo mkopo then kodi zetu zinafanya kazi. Tofautisha hivi vitu viwili vitakusaidia wewe na wanao kufanya jug.
 
Dr Slaa na Josephine wakiwa Arusha wanapewa posho ya malazi sh. 250,000/- kila mmoja wakati wanalala chumba kimoja
 
Ni vema watu tukatoa hoja sio kashfa na matusi.
Mtoa mada ametoa mada inayojadilika, iwapo m2 anajinadi kwa tabia fulani, sisi waangaliaji hu-judge kwa kuangalia matendo yake tukilinganisha na anachokisema.
Ni kawaida ya wanasiasa kuturubuni kwa maneno matamu, wakishika nafasi tu wanasahau yale waliyoahidi kwa wananchi.
NI MJADALA KUHUSU MUSTAKABARI WA TAIFA LETU WAJAMENI!!?
 
Dr Slaa na Josephine wakiwa Arusha wanapewa posho ya malazi sh. 250,000/- kila mmoja wakati wanalala chumba kimoja

kwanzia lini umekua msemaji wa chadema? Kama sio msemaji wa chadema leta source hapa umbea hatutaki.
 
Kuna wakati wana jf mna point lakini jinsi mnavyoandika inakera kweli. Nitatoa mfano, nilisoma katika shule moja ya kanisa. Katika shule hiyo, kama ulibainika kutoroka wakati wa usiku basi wewe hapakuwa na njia nyingine isipokuwa kufukuzwa. Siku moja, mimi na rafiki yangu tulisingiziwa na mlinzi kwamba tulikuwa tumetoroka, lakini kumbe tulikuwa tumetumwa na mlezi mmojawapo wa shule. Usiku ilipigwa kengele na wanafunzi wote walikusanyika na sisi hatukuwepo. Kesho asubuhi tulitafutwa mapema sana na tulianza kuulizwa kwa nini hatukuwepo shuleni wakati wa kuitisha majina. Kwa vile rafiki yangu alikuwa na kisa na mlinzi alifikiri kwamba huu ndiyo ulikuwa mda mwafaka wa kuchamba mlinzi. Hivyo malinzi aliposema hawa walitoroka mlezi, rafiki yangu alisema wazi wazi, "Wewe mzee ni mwongo sana wewe! Sisi hatujatoroka. Na unatabia ya kutufuatilia sana!" Mimi nilimwambia usiseme hivyo. Mlezi alinipa nafasi nijieleze na nilisema hivi, "Nashukuru sana mlezi, kwa kweli nikisema kwamba huyu mzee anachosema ni uongo nitakuwa namkosea adabu, lakini kweli anachosema si kweli kwani sisi tulitumwa na mlezi fulani." Kweli rafiki yangu alisimamishwa masomo kwa mda wa wiki mbili, hii ni kutokana na matumizi ya lugha mbaya.
Jambo la msingi hapa ambalo mleta mada ameleta ni: Je kweli viongozi wa CDM wanatumia magari haya ambayo walipiga kelele kwamba yanatumia mafuta mengi, gharama yake ya kununua ni kubwa na mambo kadha wa kadha? Kimsingi kama wanatumia magari haya naona hii si haki na ni kukosa msimamo. Je wakati wanasema hayo hawakuwa wamefanya research ya kutosha, kwamba magari gani yanaweza kutumika badala ya haya? Au ndiyo ule msemo usema, "Nyani hucheka **** la mwinzie, kumbe lake ni jekundu zaidi," Tunapoweka sera, lazima tuwe na dhamira za kweli, tunapotoa msimamo wetu lazima tuusimamie, na si kutoa matamko bila utafiti wa kutosha. Kama utafiti haujafanyika hakuna haki ya kuongea.
Mtoa mada jifunze jinsi ya kufanya utafiti. Pia wana jf jifunzeni kujibu hoja si matusi, hayasaidii. Hawa CDM tusipowajadili leo kesho wanaingia madarakani, tutaendelea hivyo na mwisho wake ni kuvuna mabua.
 
UKIDHANI WEWE SI fisadi PIMA KWANZA UHUSIANO WAKO NA mafisadi!!
 
Gari wanazo tumia viongozi wa CHADEMA NI V8? labuda mleta maada weke na picha kabisa ili tuweze kuchangia vizuri
 
Mkuu Kingarama.

Una hoja ya msingi sana usijali kebehi wala majibu ya kashfa.Kama CDM walisimamia hoja ya matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwa serekali kuacha manunuzi ya magari ya kifahari V8 na nk lakini wakati huo huo chama kinatumia fedha zake kununua magari aina ya v8 Toyota huo ni usani mbaya sana CDM lazima watupatie maelezo ya kina ni kwanini hawaishi sawa sawa na kauli zao.
 
Mbona husemi wanatumia Helicopter au umesahau....... CCM bana wana akili fupi sana.

Ila nature inafanya selection, kwa nini wengi waliobakia CCM uwezo wao wa kufikiria unakuwa mdogo?... mfano Lusinde etc wanashindwa kabisa kuchambua mambo na kjua waTZ kwa sasa wanahitaji nini?
 
Hata hao CCM hizo v8 wananunua kwa pesa zao sio kodi za wananchi na kama mkisema ni za kifisadi basi hata CHADEMA mafisadi wamepataje hayo magari v8
 
chadema wanatumia mavx ya mtumba,moja halizidi 40000000,mbowe ni mfanya biashara anaweza kumiliki hata gari ya 500000000.
hoja ni magari ya serikali yanayonunuliwa na ccm.
kama waliweza kununua rada kwa bei ya kutupwa ambayo chenchi yakeinatosha bajeti ya wizara unategemea nini kwenye mashangingi?
 
Wenye wivu wajinyonge! Tofautisha kati ya mali ya umma na mali ya mtu binafsi. Zungumzia mali ya umma tu!
 
Mkuu Kingarama.

Una hoja ya msingi sana usijali kebehi wala majibu ya kashfa.Kama CDM walisimamia hoja ya matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwa serekali kuacha manunuzi ya magari ya kifahari V8 na nk lakini wakati huo huo chama kinatumia fedha zake kununua magari aina ya v8 Toyota huo ni usani mbaya sana CDM lazima watupatie maelezo ya kina ni kwanini hawaishi sawa sawa na kauli zao.

ngongo habari yako bana?hivi unajua tofauti ya hizo gari unazoongelea?
chadema hakuna v8 hata moja,kumbe arusha kuna wanafiki?mi nilifikiri ni mji wa wajanja tu.
 
MBOWE anatumia gari la kiongozi wa upinzani bungeni (KU) aina ya Land cruser V8 alilotangaza kurudisha bungeni na kweli alirudisha lakini kalichukua kimya kimya bila kutuambia ameamua kulichukua......siasa bana.


Dk. Slaa anadaiwa kulipwa mshahara zadi ya milioni 7 kwa mwezi ambao unazidi mshahara wa mbunge.


Tukipata maelezo yao dhidi ya tuhuma hizi itapendeza.
Mama porojo aka mama G.Lwa... Naona CDM inakuchoma SANA. Acha ufisadi kuwa mzalendo utaipenda sana CDM, tatizo lako unaogopa kuishi kihalali unataka dark market for ur existance. SHAME ON U A MLAANIWA
 
HILI LA CHIKU ABWAO NI MTUMBA (NI KAMA $30,000)

DSCF0307.JPG


HILI LA MAREHEMU REGIA MTEMA (KAMA LA CHIKU ILA RANGI TOFAUTI)

Regia-Mtema-Car.jpg


HAYA YA SERIKALI NDIO V8 YA TZS 200,000,000

UJAMBAZI+2.JPG
 
Wakuu mie naulizia Shangingi V8 la Lema kaisharudisha bungeni?
 
Nazungumzia "consistency" ya chama kwenye mambo wanayoyapigania wakati wa Kampeni. Kusema akili yangu mbovu hakuondoi ukweli kwamba hata hayo mashangingi ya CHADEMA yananunuliwa na kwa kodi za wananchi. Wewe hujui kuna baadhi ya wabunge kabla ya kuwa wabunge hata Baiskeli walikuwa hawana uwezo wa kununua.

Unajisahaulisha kwamba wabunge wote walipewa mkopo wa shilingi Milioni 90 na ofisi ya Bunge kwa ajili ya kununulia magari yao?

Kweli wewe kiazi, hayo mashangingi ni yao binafsi siyo chama. mbona una kichwa kigumu wewe? Sera ya chama haiingilii uhuru wa mtu binafsi
 
Back
Top Bottom