Imany John
JF-Expert Member
- Jul 30, 2011
- 2,930
- 1,165
Kwanza nikuulize. Hivi usingeweza kujenga hoja yako ya kuipinga hoja yangu bila ya kuandika hilo neno nililoli-bold?
Wengi wa walioipinga hoja yangu wameongea kama vile mimi sielewi nani anakusanya kodi na serikali inatumiaje kodi inayokusanya. Kiuhalisia serikali kukusanya kodi na kuigawanya kwa matumizi ya serikali ni mambo mawili tofauti. Kodi inayotumika kulipa wafanyakazi wa kufagia maofisi ya serikali ndiyo hiyo hiyo inayotumika katika kulipa posho wabunge na mawaziri wa serikali. Hakuna Kodi inayokusanywa maalum kwa ajili kuwalipa wabunge marupurupu yao.
Hoja yangu hapa ni ya kimaadili. Mtu mkweli utamtambua kwa matendo yake, ndiyo maana nasema nguruwe akiuzwa uswahilini au super market wote ni nguruwe na bado watakuwa ni haramu kwa waislamu na wasabato. Kama wao CHADEMA walisema matumizi ya mashangingi ni hasara kwa serikali basi wangeonyesha kwa vitendo kwa.
Nimetoa mfano wa baadhi ya wabunge ambao kwa hakika walikuwa hawana hata uwezo wa kununua Baiskeli lakini leo wanamiliki VX kama vyombo vyao vya usafiri. Makadirio ya kuwapa wabunge mafuta yanatokana na aina ya magari ambayo wabunge wengi wanatumia. kama wabunge wengi wa CHADEMA wangekuwa na magari mdogo yanayotumia mafuta kidogo ni pesa ngapi za walipa kodi zingeokolewa kwa wabunge hao kutumia magari ya "kawaida"?
Sisi ambao tunafika kwenye viwanja vya bunge mara kwa mara tunajua siyo tu wabunge wa CCM hata wabunge CHADEMA nao huwa hawaji na magari yao DODOMA lakini bado tu wanachukua na posho ya kuyahudumia magari yao wakiwa DODOMA.
Chadema haina serikali magari wanapewa tu na bunge.
So ku put blame on them ni ujinga.