Mashairi ya CCM yamemponza Cheyo?

Inasikitisha kuona mtu kama Mh. Cheyo na Msomi Bagenda wanasimama na kuanza kuhutubia umati wa wasomi bila kuhusianisisha na maada iliyo kuwa inaongelewa. Wakati wenzao wanachambua Mwasada wa katiba kipengele kwa kipengele wenyewe wanaleta propaganda zilianza kutukifu wananchi za amani na utlivu. Nawapongeza vijana wa Mlimani kwa kukataa muda wao kuchezewa na hawa wazee wanaodhani vyeo na ulaji ndo mwisho wa kila kitu.
 
everyone knows Cheyo Mapesa si mwanamapinduzi wa kweli, na inaonekana dhahiri ni kibaraka wa CCM.No doubt about that.Amevuna alichopanda, kuzomewa ni halali yake.MOMOSE ALIPASWA KUELEWA KUWA PALE UDSM si mahali pa propaganda, bali ni mahali pa kuchambua mambo based on available facts. Yeye alianza hoja za propaganda, vijana wakamkarisha chini. that is very excellent.
 
Ukweli swala la katiba ni swala gumu sana, serikali ilikuwa haijajiandaa nalo kilichofanyika ni kupora hoja ili kuzima moto. Hawakujua kuwa litakuwa kubwa hivi ndio maana wanajaribu kutumia kila mbinu kulipindisha lkn kwa sasa watashindwa ni vizuri waliache lifanyike kulingana wananchi wanavyotaka otherwise linaweza kuzua vitu vingine!!!
 
Serikali ya JK iwe makini na maamuzi yake, kama haina nia ya Katiba mpya ni bora iseme mapema kuliko kuwatia hamasa wananchi na mwishowe wakaamua kudai katiba ya kweli! Na yeyote atakayesimama kutetea usanii katika suala la katiba mpya atakumbana na wananchi ambao ndiyo wenye nchi!

Uliyoyasema hapo ni ya kweli ila viongozi wa serikali ni sijui ni viburi vimewajaaa kichani au vurugu tu za kung'ang'ania madaraka?

Sijui ni nani anae wapa kiburi hicho kwani hawahofiikabisa kwa mifano hai ya huko Arab world eg Libya,Yemen,Syria. na nchi kama Tanzania ni nchi haina makuu na ni rahisi kuitawala sasa siwaelewi hawa viongozi wa CCM wao ni mbumbumbuu au hata elimu ya ngumbaru hawakuitilia maanani? unajua unafika mahali unajiuliza rais yeye hataki nini kama yeye anatetea AMANI huku akijua HAKI haitendeki simwelewi kabisa sijui ana kugugumizi gani au nchi inawenyewe huko Ulaya au twajiendesha sisi kama wananchi wa Tanzania jamani khaaaa.

 
Nilifuatilia kwa makini mjadala wa katiba ulioendeshwa mlimani siku ya jumamosi, mjadala ulikuwa mzuri lakini kati ya mambo ya kukumbukwa na kutosahaulika ni mzee mapesa kushushwa jukwaani na wasikilizaji ambao hawakuridhishwa na maneno na mwelekeo wa mzee Cheyo. inawezekana kuna sababu nyingi zilizowafanya wananchi kumpigia makofi ya kuondoka hata baada ya Dr Kitila Mkumbo kuwasihi wamsikilize amalizie anglau neno la mwisho, lakini moja ya mawazo niliyonayo mimi ni kwamba alianza kuimba mashairi yaliyozoeleka na yanayotumika kukandamiza haki za watu.

Mashairi haya moja ya hilo ni huu ubeti wa amani na utulivu, ubeti huu umekuwa ukitumika kuwanyamazisha watu wasidai haki zao katika nyanja mbalimbali. wakati wachangiaji wengi walikuwa wakikosoa muswada na kupendekeza marekebisho, yeye alijikita kwenye utetezi na msisitizo kwenye "amani na utulivu"

Nafikiri hii ni wake up call kwa wanasiasa wengine watafute namna ya ku - rephrase hii slogan la sivyo wananchi washatambua kwamba mashairi haya ya amani na utulivu bila haki ni upuuzi mtupu.

Naomba kuwasilisha wana JF

Hilo ndio tatizo la Watanzania mpaka wagonge ukuta ndio wajuwe walikuwa vipofu!
Naungana na mtangazaji mmoja aliekuwa akitowa maoni yake kuwa anawaheshimu sana wasomi lakini wasomi wanapogeuka kuwa wanasiasa basi joho la usomi linaondoka na kuwa kundi moja na wanasiasa waliozoelea kuona hoja zao hata zikiwa za kipuuzi basi ziwe hivyo hivyo. Wapenzi wa CHADEMA sasa weako sawasawa na wale waCUF wakati fullani waliokuwa wakiambiwa walale barabarani!
 
Yes nakumbuka hata Prince Bagenda alichemsha na wasomi walikuwa wanawashusha kistaarabu kwa kukupigia makofi bila kuchoka
Mchemsho wa Bagenda uko wapi? Kusema kuwa Taifa lazima liwe na mfumo utakaokubaliwa na kila ajae katika madaraka, hilo ni mchemsho? Hivyo unataka tuwe na Katiba ya Chama fulani katika madaraka na kikija chengine ibadilishwe. Sijuwi lakini kama wasomi walimzomea Bagenda kwa kuwa alituwa na CCM angalau inanipa faraja lakini kama walimzomea kwa alichokisema mungu atusaidie kama uel;ewa wa wasomi wetu uko kiwango hicho.
 
Cheyo baada ya kukiona cha moto pindi nyumba yake Masaki ilipotaka kupingwa mnada.......CCM waka mwokoa........toka wakati huo Cheyo kwishinyenee......yeye na CCM damu damu,Bwan mapesa amekuwa Bwana omba omba kwa CCM.....Kazi kushinda Q Bar tu...kuangalia machangu...
 
Cheyo huyu hapa Bungeni Dodoma.Hana tabasamu lake la kawaida.Amenywea mno.UD bwana......kweli Chuo Kikuu!
 
Back
Top Bottom