Mashahidi kesi ya ubunge Segerea wakiri makosa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2]04 APRIL 2012[/h][h=3]
[/h]

Na Anneth Kagenda
MASHAHIDI wa utetezi upande wa Jamuhuri wamekiri mbele ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kufanya kosa la kisheria kwa kutosaini fomu za matokeo katika vituo vyao.
Wakiongozwa na wakili wa Serikali Bw. Seth Mkemwa, mbele ya Jaji Profesa Ibrahim Juma, mmoja wa mashahidi hao, Bw. Omar Muhando (54), ambaye alikuwa Msimamizi wa Kituo cha Kombo namba 4A, Kata ya Vingunguti, alikiri kutosaini fomu yake.

Alidai hakusaini fomu hizo kwa sababu ya uzee ambapo kosa hilo ameligundua baada ya kuoneshwa fomu hiyo mahakamani hapo.

Alipoulizwa na wakili wa upande wa madai Bw. Peter Kibatala kuwa baada ya kumaliza uchaguzi na kukabidhi fomu kwa wahusika aliambiwa nini kuhusu fomu hiyo, Bw. Muhando alidai pamoja na kusahau, hakuambiwa kitu chchote.

Shahidi mwingine Bi. Yusta Ngoda (30), alidai mahakamani hapo kuwa wakati wa uchaguzi huo alikuwa Msimamizi Mkuu wa Kata ya Vingunguti, Kituo cha Usisede, ambayo naye alikiri kusahau kuweka sahihi na jina lake katia fomu hizo.

Akiongozwa na wakili Bw. Mkemwa, shahidi huyo alidai yeye haoni kama kutoweka sahihi ni kosa kwani fomu hiyo ina vielelezo vinavyoonesha imetoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

“Mheshimiwa kama nilikosea kusaini fomu, waakala wa CHADEMA angeweka sahihi au angesema fomu namba 16 si halali kama ingekuwa na kasoro hivyo sikuona kama inakosa,” alidai.

Alipoulizwa na wakili Bw. Kibatala kuwa wakati wa semina hakuambiwa kwamba kutosaini fomu hiyo ni kosa kisheria, Bi. Ngoda alijibu, “Niliambiwa lazima niisaini”.

Shahidi mwingine Bi. Alvera Laurence (46) ambaye alikuwa ni Msimamizi Kituo cha Hali ya Hewa C, namba 5, Kata ya Kiwalani, alikiri kufanya makosa tisa katika fomu hiyo ikiwemo kutoweka saini, jina, tarehe ya kufunga na kutojaza nafasi zingine na kudai kisheria alifanya makosa.

Alipoulizwa na wakili wa Serikali Bw. David Kakwaye, alikiri kufanya makosa hayo kutokana na uchovu, kuchelewa kuletewa gari na kuwaza jinsi atakavyobeba makasha yenye kura kichwani. Kesi imepangwa kuendelea leo.



 
Hao ndio tunaowabebesha dhamana za kura zetu, wazee, wavivu, wajinga wa makusudi. Inaleta hasira sana kwanini walipokea posho zilizotokana na kodi zetu? Hata Tume nayo wazembe!
 
Tatizo la Mwizi baada ya muda unasahau ulivyoiba... sasa wanawauliza hawajui na walikuwa na Masanduku Mkononi
 
Hao ndio tunaowabebesha dhamana za kura zetu, wazee, wavivu, wajinga wa makusudi. Inaleta hasira sana kwanini walipokea posho zilizotokana na kodi zetu? Hata Tume nayo wazembe!

Lububuva kastaafu kutokana na uzee wake lakini Rais akaona ni mtu pekee anayeweza kushika nafasi aliyonayo sasa, ninamchikia sana Mwenye kiti wa CCM
 

Alipoulizwa na wakili wa Serikali Bw. David Kakwaye, alikiri kufanya makosa hayo kutokana na uchovu, kuchelewa kuletewa gari na kuwaza jinsi atakavyobeba makasha yenye kura kichwani. Kesi imepangwa kuendelea leo.




Stranger than fiction.

Hii inaweza kutokea Tanzania tu...!!!
 
Nashangaa mtu akicheka mahakamani anahukumiwa hapohapo bila hata kujitetea, hawa wanaokiri makosa sijui hakimu anataka mtu mwingine aje ashtaki, "upelelezi ufanyike", alipwe sitting allowence, apate hongo ndio atoe hukumu! Period!!!
 
Hizo fomu walizowakilisha zitakuwa feki zenye kumbeba jamaa. na huo wanaoongea ni uongo tu.
 
Wakuu mnao jua sheria, hivi mpaka hapo kunasababu ya kusubiri mashahidi wengine, nahisi kama ni upotezaji wa muda hivi?
Anyway, kuna thead iliwahi kutupwa humu kusiana na ushauri alioutoa Bwana mkapa juu ya matokeo ya uchaguzi wa Arumeru, kwamba tume itangaze ccm imeshinda then Chadema wataenda mahakani na mahakama itaendelea kupiga tarehe tu; nadhani ndicho kinachotokea sasa.
 
Hao ndio tunaowabebesha dhamana za kura zetu, wazee, wavivu, wajinga wa makusudi. Inaleta hasira sana kwanini walipokea posho zilizotokana na kodi zetu? Hata Tume nayo wazembe!
Nepotism hiyo kiongoz, unakuta ndugu wa kiongoz anapewa mchongo wa kuwa msimamiz wa uchaguzi ilhali ni mjinga wa level hiyo kama walivyojipambanua wenyewe.
 
hivi hawa wote walifanya kosa linalofanana, yalabi jimbo twalila hiloooooo, hakuna cha mkono wa mtu au mguu wa paka, nilazima kieleweke.
 
Wakuu, nadhani kweli tunapoteza hela zetu za kodi kuendelea kufuatilia kesi ambayo tayari imeisha. Jimbo jingine ndani ya CDM
 
Hivi shahidi akikiri kufanya kosa tena la jinai mahakamani hatua gani inafuata?
 
Back
Top Bottom