Masha Lawrence asema CCM inaonyesha kushuka hadhi

Mkiliman

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
983
340
Akiwa kwenye Jenerali on Monday Channel ten, anamsifia Mkapa, anaona maziko ya CCM yapo njiani.
 
Hivi ni mna wagombea wangapi wanaotarajia kugombea urais 2015 - ulimwengu
 
Naye ni mtuhumiwa hana moral authority ya kuongelea mipasuko ndani ya chama.
 
Vijembe vya hapa na pale vitatufikisha popote - mpiga simu kutoka makambako
 
Nini kilimsukuma kuingia kwenye siasa,
nini msimamo wake kutokana na ccm kutokuwa na msimamo, inasubiri wapinzani ndio iige, mfano mkutano wa jangwani walioiga kwa chadema - mpiga simu
 
Ushabiki uondolewe, tuongelee hoja za msingi za kitaifa. MASHA
 
Kwanza yeye baada ya kushindwa ubunge alienda kuchukua furniture zote za ofisi ya mbunge kisa alinunua yeye Masha mtu wa visasi
 
Akiwa kwenye Jenerali on Monday Channel ten, anamsifia Mkapa, anaona maziko ya CCM yapo njiani.

Yeye ni mmoja wao aliyeisababishia CCM kushuka NGAZI; alipokuwa Madarakani alikuwa MBOGO; kama VILE

Atatawala MILELE; hakujuwa PEOPLE's POWER...
 
bora yeye kasema ukweli, maana dalili ya mvua ni mawingu, ukiona wapinzani wanawindwa na wanaharakati kutishiwa ni dalili za kwisha
 
Amesema mwanasiasa mzuri ni yule anayekubali kushindwa kama vile yeye alivyokubali kushindwa! Ni kweli hii?

Masha tangu mwanzo hakuwa tayari kushindwa. Angalia hapa:

1. Aliamrisha maafisa wa Uhamiaji (idara iliyokuwa chini ya wizara yake) wachunguze uraia wa mpinzani wake Wenje, na hatimaye Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mza (returning Officer) alimuondoa katika kinyang'anyiro baada ya kumwekea pingamizi. NEC ilimrudisha Wenje. Habari pia zilizagaa kwamba Masha alimuofer Wenje Sh 350 milioni ili ajitoe.

2. Wakati wa kampeni kuna gari moja lililoibiwa Kenya lilikutwa Mwanza limebandikwa picha za Masha za kampeni. Sijui hii ishu iliishia vipi.

3.Ilimchukuwa Returning Officer siku mbili kutangaza matokeo, ucheleweshaji ambao ulitaka kuzua ghasia kubwa. Zilikuwa zinatafutwa namna ya kumpa ushindi asiostahili.






 
Anapenda misifa tu huyo. Juzi juzi tu alikuwa katika kipindi cha mikasi cha ITV akihojiwa na yule Salama wa Bongo Star Search akiongea vitu kama hivyo hivyo!
 
ulemavu wetu humu ni bias

Pwenti akitoa mtu wa itikadi nyingine hata iwe na maana gani tunarukia kwenye negative tu............ KAUGONJWA KABAYA KULIKO UKIMWI
 
Masha anatafuta namna ya kurudi kwenye siasa...anatafuta daraja. Angekaa kimya tungemheshimu. Huwa nawashangaa sana ccm wanapokuwa madarakani wanakuwa wanakula tu, wakitoka wanaanza kuzungumza kana kwamba wao ni wema sana!
 
Back
Top Bottom