Masha apewa live; wezi wako ofisini kwako!!!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, ametajiwa majina ya polisi wawili waliohusika katika mauaji ya watu 14 na kuwajeruhi wengine 18 kisiwani Ukerewe, mkoani Mwanza.

Watu hao waliuawa na majambazi katika kisiwa kidogo cha Izinga Januari 17, mwaka huu, walipokuwa wakijaribu kuzuia boti iliyotumiwa na majambazi waliovamia kisiwa hicho na kupora mali za wafanyabiashara.

Wananchi hao walimweleza Waziri Masha juzi wakati akiwahutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Bwisya kuwa kuna askari wawili, akiwemo aliyekuwa mkuu wa polisi wilayani Ukerewe na askari mmoja waliyemtaja kwa jina moja la Mrisho, kuwa walishiriki katika tukio hilo la uhalifu.

Wananchi hao walisema kuwa pamoja na kutuhumiwa askari hao hawakuchukuliwa hatua zozote, badala yake walihamishwa katika vituo vyao vya kazi tu.

Baada ya wananchi kumtajia majina ya polisi hao, Waziri Masha alisema serikali haitakubali kuharibiwa sifa na watu wachache wanaokiuka maadili ya kazi yao, na akawaagiza viongozi wote, ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na mkoani Mwanza, kufanya uchunguzi dhidi ya askari wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ujambazi.

Alisema kuwa askari wamaeajiriwa kwa ajili ya kulinda raia pamoja na mali zao na siyo kufanya vitendo vya uhalifu na kuonya kuwa askari yeyote atakayebainika kufanya vitendo hivyo, atawajibishwa kisheria ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.

“Viongozi wenzangu, nafikiri mmeyasikia. Siyo rahisi mtu huyo huyo anatajwa kila sehemu...hapa lazima kuna tatizo,” alisema na kuongeza: “Lazima mfuatilie na hatua zichukuliwe. Iko siku tutapigwa mawe na wananchi wakichoka.”

Masha aliwataka watu wanaoendesha vitendo vya uhalifu visiwani humo kujisalimisha mara moja na kuaacha kazi hiyo kwa kile alichoeleza kuwa serikali imejipanga vilivyo kukabiliana nao.

Pia aliwataka wananchi kutoa ushirikiano wa karibu kwa Jeshi la Polisi kwa kuwataja watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu katika maeneo yao.

Alisema kuwa serikali ilisikia kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Ukerewe kupitia kwa Mbunge wa jimbo hilo, Balozi Gerturude Mongella, cha kuimarisha ulinzi katika visiwa hivyo na kuamua kuunda wilaya ya kipolisi katika kisiwa cha Ukara ili wananchi waishi kwa amani na utulivu.

Akizungumza katika mkutano huo, Balozi Mongella aliishukuru serikali kwa uamuzi huo na kufafanua kuwa kama askari watakaopelekwa katika wilaya hiyo ya kipolisi watawajibika ipasavyo, watasaidia kwa kiasi kikubwa kukomesha vitendo vya uhalifu ambavyo vimekuwa kero ya muda mrefu kwa wakazi wa visiwa hivyo.

“Napenda kuishukuru serikali kupitia kwa Rais wetu na Waziri Mkuu na wewe mwenyewe (Masha) kwa kusikia kilio hiki cha wana-Ukerewe, kwa kweli nimefarijika sana na ninakuomba umfikishie salaam zangu Rais wetu,” alisema Mongella.

Hata hivyo, Mongella aliitaka serikali kuboresha maisha ya askari polisi pamoja na askari wa Jeshi la Magereza hususan kuwajengea nyumba bora ili wawe na maisha mazuri, hali itakayowapa moyo wa kufanya kazi na kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Katika hatua nyingine, Masha aliliagiza Jeshi la Polisi, Magereza na serikali wilayani Ukerewe kushirikiana kujenga kituo kikuu cha polisi katika wilaya ya kipolisi ya Ukara, badala ya kutegemea bajeti ya serikali.

Waziri Masha alitoa agizo hilo baada ya kukagua jengo la mahakama ya mwanzo katika katika kijiji cha Bwisya, ambalo linatumika kama kituo cha polisi.

Alisema mazingira aliyoyaona katika eneo hilo hayaridhishi kabisa kwa sababu jengo hilo ni bovu na chakavu na kuviagiza vyombo hivyo kushirikiana ili kujenga kituo hicho mapema iwezekanavyo.

Alisema mafundi katika ujenzi huo watatoka katika Jeshi la Magereza kwa lengo la kuharakisha ujenzi huo.

Alisema kuwa kituo hicho kilipangwa kujengwa kwa bajeti ya mwakani, lakini akasema hali aliyoishuhudia hairuhusu kusubiri bajeti ijayo. “Hatuwezi kuchezea maisha ya wananchi kwa kusubiri bajeti ya serikali, hivyo ninawaagiza Polisi, Magereza na uongozi wa wilaya kuhakikisha kituo hicho kinajengwa mara moja na serikali kuu itashiriki kikamilifu,” alisema.

Akisoma taarifa ya wilaya, Mkuu wa wilaya hiyo, Queen Mlozi, alisema katika tukio la mauwaji ya watu 14 katika kisiwa cha Izinga, tayari watu 40 wamekamatwa na kulipongeza Jeshi la Polisi kwa operesheni iliyofanywa katika kisiwa hicho.


CHANZO: NIPASHE
 
Ila jameni mi naona tatizo sio Masha as Masha, tatizo ni mfumo usiokua na uwajibikaji kwenye public office, kuna exploitation kubwa ya power on governments official kuanzia ngazi ya juu mpaka ya chini. Why hakuna uwajibikaji? mtu anapata kazi kwanza kwa kubebwa then akiharibu anabebwa na kuhamishwa kwingine wapi tunaenda? mapolisi wanaiba wanashirikiana na majambazi lakini wanafichiana siri, hivi wandugu naomba kuuliza kulikua na SABABU GANI za kimsingi kwa Prof. Mwakusya kwa mfano kubaki ofisini while under him mgonjwa wa mguu alichezewa ubongo (at the end of day alifariki RIP) na wa kichwa akachezewa mguu? mgonjwa wa akili kuweza kuwaua wagonjwa wenzake wodini which means hakuna uangalizi! aghhhhh jamani inachefua maana ukianza kufikiria HASIRA TUPU. Mie naendeleza my protest kesho ijumaa nawapiga kadi nyekundu na MUNGU atasikia tu kilio changu. RED FRIDAY PROTEST vaa red red on friday
 
I wish I could know what is in his mind.Ila najua ni mpenzi sana wa mpira, sijui Man U vile...angelipewa wizara ya michezo labda kama hii wizara imemzidi kimo.
 
Masha yupo likizo yakujiandaa na uchaguzi tangu mwaka jana mwezi wa march mwaka jana, kweli nakuambieni hafanyi kazi yoyote......kweli huyu jamaa ni legelege, aliepata madaraka ambayo hayawezi wala hana hadhi nayo.
Masha alistahili kupewa ukatibu kata labda angeweza kuendana na changamoto zake.
 
I wish I could know what is in his mind.Ila najua ni mpenzi sana wa mpira, sijui Man U vile...angelipewa wizara ya michezo labda kama hii wizara imemzidi kimo.

aisee wapenzi wa Man U wanafahamika na sidhani yeye ni mmoja wetu
 
Huyu jamaa anachukiwa sana sijui kwa nn?
Mwaka huu na ubunge itakuwa kazi kweli kweli kupita sijui ngoja tusubili.
 
Huyu jamaa anachukiwa sana sijui kwa nn?
Mwaka huu na ubunge itakuwa kazi kweli kweli kupita sijui ngoja tusubili.
mimi simchukii sana, ila sivutiwi na utendaji wake legelege, utendaji dhaifu , kiburi na kushiriki kwako kwenye kusign mikataba ilioiba fedha nyingi BOT akiwa ofisa wa IMA, Hii inamuondolea uzalendo, maana alishirikiana na wezi kuiaminisha serikali kuwa mikataba ya ilikua sahhihi.
Masha waziri asie na makali aliepewa kazi inayohitaji umakini na umahiri.
 
sekta hii ilifaa apewe magufuli tu atawanyoosha wote hawa nchi itakuwa shwariiiiiiii na tutalala milango wazi!maana yule ni mzee wa amri tu!
 
Uwezo wake mdogo madaraka makubwa..halafu naibu wake alipokua akijaribu kuziba mapengo akamjia juu na kumuambia yeye ndie top aache kujifanya mjuaji...wizara ikatumbukia katika likizo isiyoisha.
 
Uwezo wake mdogo madaraka makubwa..halafu naibu wake alipokua akijaribu kuziba mapengo akamjia juu na kumuambia yeye ndie top aache kujifanya mjuaji...wizara ikatumbukia katika likizo isiyoisha.

Mlevi wa 24/7 unategemea nini kutoka kwake!?
 
Mlevi wa 24/7 unategemea nini kutoka kwake!?


Huyu Jamaa kuna siku nilimkuta Rose Garden pale Mikocheni, was completely drunk, ilibidi walinzi wake binafsi wamsaidie kumpeleka kwenye gari!!!

Nilimdharau tangia siku hiyo! Hawezi kutofautisha alivyokuwa kabla pale IMMA na alivyo sasa pale Wizara ya Mambo ya Ndani!
 
Huyu Jamaa kuna siku nilimkuta Rose Garden pale Mikocheni, was completely drunk, ilibidi walinzi wake binafsi wamsaidie kumpeleka kwenye gari!!!

Nilimdharau since! Hawezi kutofautisha alivyokuwa kabla pale IMMA na alivyo sasa pale Wizara ya Mambo ya Ndani!
tatizo la Masha ni kujisahau na kujisahau ninini anapaswa kufanya, kweli.
kama elimu ni uongozi kijana kajitahidi kusoma, tatizo ni lile lile la kupeana madaraka kwa fadhila.
Masha anapewa Wizara nyeti sana, ikidaiwa ni asante kwa kusaidia upatikanaji wa mamilioni yaliyoibwa katika EPA na upuuzi mwingine.
Masha anashindwa hata kujitokeza hadharani kulaani mauaji ya Tarime, ajali barabarani na kila aina ya vurugu za kiusalama nnchi hii.
bado nashangaa....na nitashangaa nikiona JK anampa tena wadhifa wakiutendaji hata iwe ukuu wa wilaya.
kuna wakati nawashangaa hata wasaidizi wake , ni kama wanamuogopa kumueleza ukweli, nashangaa Kikwete ni kama anaogopa kumgusa ili asije kutoa siri......
 
Unadhani huyu m2 atawafanya nini? Hawezi lolote na si ajabu aliwatuma mwenyewe. Huyu jamaa ni miongoni mwa mawaziri walioshindwa kabisa katika wizara zao. Nashangaa bado K'wete amemng'ang'ania, ni afadhali hata afungiwe jiwe la kusagia azamishwe Kamanga kule kwao!
 
mimi sioni tatizo la masha liko wapi, tatizo ni mfumo wote wa utwala, km utendaji wa masha mbaya tuambieni ni utendaji wa kiongozi gani mzuri. pia hao polisi msiwalaumu sana maslahi duni ndo yanayowasukuma huko.
 
Huyu Jamaa kuna siku nilimkuta Rose Garden pale Mikocheni, was completely drunk, ilibidi walinzi wake binafsi wamsaidie kumpeleka kwenye gari!!!

Nilimdharau tangia siku hiyo! Hawezi kutofautisha alivyokuwa kabla pale IMMA na alivyo sasa pale Wizara ya Mambo ya Ndani!

mi nilimdharau siku nimepand nae ndege anarudi toka mwanza akawa aanaseviwa yeye tu mmh nikauliza jamaa yangu akaniambia yule mfanyakazi wa ndege ndio bibi yake mdogo...alimlewesha wakati tunatua naona wakampa nafasi ya kuanza kushuka kucheki kama yuko fit kutembea am lah hamad alifika salama ila hoi drunk

hawa ndio mawaziri watarajiwa 2011-15 wa bwana JK
NCHI IMEVAMIWA
 
Back
Top Bottom