Masahihisho Kwenye Umri Wangu.

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,720
Wadau, napenda kuuliza swali baada ya maelezo yafuatayo!

Mtoto anaanza uhai toka siku ya kwanza anatungwa mimba, hili bila shaka halina ubishi.

Anakua hadi umri wa miezi 9(with more or less) na kuzaliwa.
Kwanini akizaliwa tunafuta umri wake alioishi tumboni akiwa hai, na kuanza kuhesabu siku 1 nakuendelea?
Kwanini tusingeendeleza ile miezi tisa ili tuwe na umri sahihi wa mtu?

Unajua kwamba mtu yeyote anakuwa na umri aujuao yeye, plus miezi 9ambayo haisemwi?

Kwanini inafanyika hivi?
 
Pakajimmy leo umeenda mbali sana nadhani umeingia Nyuma ya ubongo..Mie sijui cha kusema..
Lakini Tofautisha mimba nakitu kilichoisha toka Tumboni tayari...
wanasayansi waje watufafanulie zaidi
 
Kwa sababu ndo siku ya kwanza anavuta pumnzi ya dunia ndo hapo hapo anaanza kuishi duniani asipo vuta pumnzi ya dunia anakufa hapo hapo anakuwa mfu huyo mtoto.
 
'Umri' unaanzia pale mtu anapozaliwa. Tukitaka kuanzia mimba ilipotungwa mbona kutakuwa na utata sana kwa sababu mara nyingi hatuwezi kujua kwa urahisi (katika accuracy ya siku au saa) siku/muda ambao mimba ilitunga.

In a Typical Pregnancy: For a woman with a regular period, conception typically occurs about 11-21 days after the first day of the last period. Most women do not know the exact date of conception, and their conception date is merely an estimate based on the first day of their last period.

Special Cases: Women who undergo special procedures such as artificial insemination or in vitro fertilization typically know the exact date of conception.
 
Ni jambo tata sana kusema umri uanze pale mimba inapotunga. Kuna watu wanakuwa na mimba siku kadhaa au hata miezi bila kujua ni wajawazito. Labda mtoa mada atupe kigezo kinachoweza kutumika kutambua siku na saa mimba inapotungwa.
 
Ni jambo tata sana kusema umri uanze pale mimba inapotunga. Kuna watu wanakuwa na mimba siku kadhaa au hata miezi bila kujua ni wajawazito. Labda mtoa mada atupe kigezo kinachoweza kutanbua siku ya kutunga kwa mimba.
Hiyo wala si ishu kama tutaamua kuhesabu icluding umri wa tumboni!
Itakuwa ni rahisi- yaani mtu anazaliwa, tayari ana miezi 9, then aendeleze kuanzia pale...!
 
pakajimmy mi nakuunga mkono hapo hususani ukirudi kwenye swala la kesi za mauaji ya wanawake wenye mimba iliyofika kama miezi 6 hivi,ujue huwa mimba hiyoo inahesabiwa kama ni mtu mzima au si hivyoo?
 
Hiyo wala si ishu kama tutaamua kuhesabu icluding umri wa tumboni!
Itakuwa ni rahisi- yaani mtu anazaliwa, tayari ana miezi 9, then aendeleze kuanzia pale...!
Issue ipo pale pale.............. kwamba hii ni miezi tisa.unaanza kuhesabu tota lini...??? maana wengine inaonekana wanazaliwa na miezi saba na wengine mpaka miezi 16............

By the way........... kwa nini hesabu za umri ziishie pale tu mtu anapokufa.........??? hivi wewe ambaye umefiwa na mzazi wako, may be alikufa akiwa na miaka .....say 40......... na wewe kwa sasa una umri wa mika 50 na bado upo hai...nani mkubwa...???
 
Mtoto akiwa tumboni mwa mama anakuwa bado ni sehemu ya mama, hata kama ni kiumbe hai, na ndo maana anaitwa "mimba" mpaka pale atakapozaliwa. Kuzaliwa ndiko kunamtenga yeye kama nafsi na mama yake. Kuanzia hapo ndipo tunaanza kuhesabu umri wake wa kuwa hapa duniani; ndo maana tunasema "nina miaka ya . . . ya kuzaliwa" na si "miaka . . . ya uwepo". Akiwa tumboni mwa mama yake bado hayupo duniani, bali tumboni mwa mama. Kube kuzaliwa ndo point of reference, na si kutungwa mimba.
 
pengine tuwapate physicians watusaidie katika hili
hii kitu ni ngumu sana kwa fikra za kawaida
hata hivyo barikiwa kwa mada hii.
tusubiri michango zaidi
 
Kama sikosei Korea wanaanza kuhesabu kuanzia mimba yani mtoto akizaliwa bas anakuwa na mwaka mmoja, ila kwetu hiyo hatuna!!
 
Wakianza kuhesabu kuanzia wakati wa kutungwa mimba itakuwa ngumu sana kupata exact time/day/date/hour ya mtoto huyo kutungwa mimba kwa vile wengine wanafanya tendo la ndoa mara kadhaa kwa siku au kwa usiku mmoja tena kwa intervals. Katika mazingira hayo si rahisi kusema mtoto ametungwa muda gani, hivyo kuweza kuanza kuhesabu umri wake. Itawezekana pale watu watakapoanza kufanya tendo la ndoa kwa mpango unaoeleweka na kuweka rekodi zao wazi. Tena hii itakuwa nzuri sana kwani wale vibaka wa mapenzi wanaotunga wake za watu mimba itakuwa rahisi kuwakamata au kuwadhibiti ili wasifanye uhuni huo tena.

Lakini kwa sasa ambapo waafrika wengi grafu ya tendo la ngono ilivyo juu hivi itakuwa ngumu kwa hakika kujua ni tendo lipi la saa ngapi kati ya matendo labda matano limetunga mimba hii. Kazi kwelikweli. Tukubali tu kuwa kuhesabu kuanzia kuzaliwa ndiyo njia nzuri na yenye uhakika kamili kwamba - tuseme - mtoto amezaliwa saa 5.59 za usiku wa tarehe 18.03.2010 na ndiyo tunaanza kuhesabu umri wake.
 
Hiyo wala si ishu kama tutaamua kuhesabu icluding umri wa tumboni!
Itakuwa ni rahisi- yaani mtu anazaliwa, tayari ana miezi 9, then aendeleze kuanzia pale...!

Na wanaochelewa kuzaliwa wanazaliwa na miezi 10 je? Na wale wanaozaliwa prematurely?
 
Wanauliza tarehe ya kuzaliwa. Hii huwa ni safi kwani wengine huzaliwa baada ya miezi 6, 7, 8 na wengine hadi 10. Sasa kipi kitumike kama standard?

Pia ingelikuwa hivyo, ingelibidi swali liwe "date of conceive". Tatizo hii tarehe kuwa wanawake wengi duniani huwa hawafahamu. Sasa utafahamu vipi kuwa ulitungwa mimba siku fulani kiasi kwamba una miezi tisa kweli na siyo miezi 8 na siku 23 na robo?
 
PJ swali lako ni zuri sana, ila uko kwenye hatari ya kubadilisha standard ambazo zinatufanya tuwe na system.

wa mfano nani aliyekuzuia wewe kusema una miaka X na miezi 9?? sioni tatizo wewe kufanya hivyo, swali lako ni kuwa unataka kubadilisha standard, then questions may continue

Nani aliyesema upande huu uitwe kusini, kaskazini , maksariki au magharibi?
Nani aliyetuamulia tuite leo jumatatu na leo jumamosi
Nani ........

Naona dalili ya mtoto mtukutu hapa!
 
Jimmy mbona unaanza unataka kutupeleka miezi tisa mbele bana...

Nimegundua kitu hapa...Watu wana hofu na umri!...huh!.............Kwanini tuogope kuonekana wa umri wetu sahhihi?...uNNECESSARILY skeptical of the truth!
 
kaka PJ mi hata sijaona kinachokusumbua akili............ lika kitu kina definition yake............... usijaribu kulazimisha definition fulani i-fit vitu unavyotaka wewe bali acha kila definition iangukie eneo lake..........

date of birth (DOB) ibaki date of birth na definition of age ibaki as defined accordingly.............. sasa ukianza kutaka tarhe ya kutungwa mimba, tengeneza definition nyingine alkini whenever you are asked your DOB please give your DOB or otherwise you will be regarded as cheating ............... u ll infact be in trouble................

these are demographics.............. consult the professional for more details..........................
 
Wanauliza tarehe ya kuzaliwa. Hii huwa ni safi kwani wengine huzaliwa baada ya miezi 6, 7, 8 na wengine hadi 10. Sasa kipi kitumike kama standard?

Pia ingelikuwa hivyo, ingelibidi swali liwe "date of conceive". Tatizo hii tarehe kuwa wanawake wengi duniani huwa hawafahamu. Sasa utafahamu vipi kuwa ulitungwa mimba siku fulani kiasi kwamba una miezi tisa kweli na siyo miezi 8 na siku 23 na robo?

mkuu umemaliza................ asiyetaka kujua shauri yake................
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom