Masaa 48 kabla ya SENSA, mhamasishe jirani yako na JF memba mwenzio

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,396
7,967
Baada ya kusubiri kwa miaka kumi hatimaye imebakia masaa 48 tu kuhesabiwa ili serikali ipate takwimu inazohitaji. Nikiwa kama raia mwema wa Tanzania nimejiandaa vya kutosha kuhesabiwa na ninao wajibu wa kuwahamasisha watanzania wenzangu wahesabiwe. Ewe mwana JF mwenzangu, ewe Mtanzania mwenzangu huu ni wakati muafaka kuhesabiwa. Its a once in ten years opportunity. Kwangu nimeandaa soda na keki kwa ajili ya karani na kiongozi wa mtaa kujiburudisha huku wananiuliza maswali mkuu wa kaya.
SENSA KWA MAENDELEO YA TAIFA...
 
Hesabiwa wewe na familia yako hapa haesabiwi mtu waje kitaa waone
 
Baada ya kusubiri kwa miaka kumi hatimaye imebakia masaa 48 tu kuhesabiwa ili serikali ipate takwimu inazohitaji. Nikiwa kama raia mwema wa Tanzania nimejiandaa vya kutosha kuhesabiwa na ninao wajibu wa kuwahamasisha watanzania wenzangu wahesabiwe. Ewe mwana JF mwenzangu, ewe Mtanzania mwenzangu huu ni wakati muafaka kuhesabiwa. Its a once in ten years opportunity. Kwangu nimeandaa soda na keki kwa ajili ya karani na kiongozi wa mtaa kujiburudisha huku wananiuliza maswali mkuu wa kaya.
SENSA KWA MAENDELEO YA TAIFA...
kwangu nimewataarishia mapokezi mazuri
 
amabo mko tayari kuhesabiwa hamasishaneni, tuliogoma nasi tuna hamasishana tuendelee na msimamo wetu.
All the best kwa pande zote.
 
mkuu wewe ni PR wa NBS?hakuna kuhesabiwa mtu hapa mpaka kipengele muhimu ktk culture yani DINI kiwepo
 
Kwangu watakuta bango mlangoni (mimi muislam sihesabiwi)chezea waislam wewe!
Kutokutii mamlaka ni dhambi kwa mujibu wa Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar. Tii mamlaka inayotawala. Muislam safi Alhaji Jakaya Mrisho Kikwete Khalfan atakuwa wa kwanza kuhesabiwa.
 
dah hebu tusubiri tuone maana mkuu wa kaya alisema asie hesabiwa anafungwa sijui hayo magereza yatatosha
 
kuna kijana kaniuliza swali la kusikitisha sana.
Je sensa iliyopita imesaidia vipi ustawi wa jamii yetu?
 
2002 tuliesabiwa lakini sijui kama serikali ilitumia takwimu kupanga maana matatizo bado pale pale.Tukimaliza sensa basi serikali ijikite kuamasisha swala rushwa kupita kila kaya na baada ya hapo turudi kwenye mapambano dhidi ya ufisadi kaya moja baada ya nyingine.
 
amabo mko tayari kuhesabiwa hamasishaneni, tuliogoma nasi tuna hamasishana tuendelee na msimamo wetu.
All the best kwa pande zote.
Tii mamlaka, tii sheria za nchi kujenga Tanzania moja yenye amani. Kama hata ukitoa hela kwenye ATM unazihesabu kuona kama ziko kamili, kwa nini serikali isihesabu watu wake kujua idadi yao??
 
kuna kijana kaniuliza swali la kusikitisha sana.
Je sensa iliyopita imesaidia vipi ustawi wa jamii yetu?
Mwambie ndio imesababisha serikali kujenga shule za kata baada ya takwimu kuonesha kuwa idadi kubwa ya vijana walio shule za msingi watakaohitaji kuanza sekondari. Pia ujenzi wa zahanati katika kata au vijiji hutegemea idadi ya watu, Isije tokea eneo mlilogomea sensa mkaonekana idadi yenu haitoshelezi kupatiwa dispensari au kituo cha afya halafu muanze kusingizia mfumo islamu au mfumo kristo
 
2002 tuliesabiwa lakini sijui kama serikali ilitumia takwimu kupanga maana matatizo bado pale pale.Tukimaliza sensa basi serikali ijikite kuamasisha swala rushwa kupita kila kaya na baada ya hapo turudi kwenye mapambano dhidi ya ufisadi kaya moja baada ya nyingine.
Hata chama chako unacho support kitahitaji kujua idadi ya watu ili kijua maeneo gani ya kutoa kipaumbele wakati wa kampeni
 
Baada ya kusubiri kwa miaka kumi hatimaye imebakia masaa 48 tu kuhesabiwa ili serikali ipate takwimu inazohitaji. Nikiwa kama raia mwema wa Tanzania nimejiandaa vya kutosha kuhesabiwa na ninao wajibu wa kuwahamasisha watanzania wenzangu wahesabiwe. Ewe mwana JF mwenzangu, ewe Mtanzania mwenzangu huu ni wakati muafaka kuhesabiwa. Its a once in ten years opportunity. Kwangu nimeandaa soda na keki kwa ajili ya karani na kiongozi wa mtaa kujiburudisha huku wananiuliza maswali mkuu wa kaya.
SENSA KWA MAENDELEO YA TAIFA...
Sensa kwa maendeleo ya nchi,mi niko njiani narudi kutoka mkoani ili nihesabiwe kijijini kwangu Likurufusi bila kukosa ,sensa kwangu ni tukio muhimu kama vile kupiga kura,mii naandaa kabisa supu ya kuku wa kienyeji na togwa kwa ajili ya karani wa sensa atakaye kuja nihesabu kwenye kaya yangu
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom