Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,272
Marxism–Leninism ni mfumo wa siasa au uliojulikana duniani kama Marxism na Leninism, lengo lilikua kuanzisha serikali za kijamaa na kuziendeleza zaidi. Marxist–Leninists walihodhi mfumo huu na waliusambaza pembe zote za dunia kutokana na uelewa wa sehemu ile, lakini kipaumbele cha mfumo huu ilikua chama kimoja cha kisiasa kitakacho endesha serikali ambayo itasimami uchumi, maswala ya kimataifa, elimu, afya, jeshi, na maswala mengine yote. Hii ilikuwa tofauti na siasa za kibepari ambayo kuna tabaka la mabwana ambao walimiliki uchumi wa nchi. Siasa hii imebakia katika serikali za China, Cuba, Laos na Vietnam na huu ndio ulikua mfumo wa Communist Party of the Soviet Union (CPSU) na nchi nyingine za ulaya Mashariki (Eastern Block).
Marxism-Leninism kwanza walianza filosofa hii kwa mawazo yaliyofanana katika Muungano wa Kisoviet mnamo miaka ya 1920, wakati Joseph Stalin na wengine waliomuunga mkono kuchukua madaraka ya Chama Cha Kikomunist cha Urusi (bolsheviks). Kilikataa wazo hili la Umoja la Marxists wakati dunia ikiwa kwenye mapinduzi umuhimu wa siasa za ujamaa (siasa mkusanyo wa mapato) na baadae kuhama kutoka ubepari mpaka kufikia Taifa la kijamaa. Mwisho walikuja na mpango wa miaka mitano. Kimataifa pia mpango huu ulianza kutangazwa na kuanza kusaidia mapinduzi ya nchi nyingine ili ziunge mkono mfumo huu wa siasa.
Vladimir Lenin
Malengo ya Marxism-Leninism yaliendeleza taifa kuelekea kwenye jamhuri ya kisoshalist kupitia uongozi wa kimapinduzi, tabaka la watawaliwa ambao walianza kuona maonevu kutokana na nafasi yao katika jamii. Serikali ya kisoshalist inapinga ukandamizwaji wa tabaka la watu wa chini na chama tawala kinasimamia uongozi wa kidemokrasia unaoongoza nchi nzima kitu ambacho Vladimir Lenin alielezea kama "tunagawanyika katika mijadala lakini tunaungana kwa vitendo". Usoshalist ulilenga ujamaa ambao ni mfumo usio na matabaka, hakuna mmiliki wa mali na vitega uchumi vyote vimilikiwe na serikali na raia wote wawe na haki sawa katika jamii.
Kijamii.
Marxism–Leninism ilihakikisha huduma zote za jamii kutolewa bure bila ubaguzi. Uboreshaji wa huduma za afya, elimu, malezi ya watoto na huduma zote za jamii zigharamiwe na serikali. Soko la kazi na ajira kupanuliwa na watu waletewe maendeleo kutokana na makusanyo ya serikali. Watu wapewe elimu kuhusu uchumi na mipango ya nchi kwa njia ya elimu kwa wote bila ya matabaka.
Uchumi.
Serikali kuwa mmiliki na mwangalizi wa secta ya uzalishaji kupitia umilikaji wa jamii.Kwa kuzingatia uzalishaji bora na kupunguza hasara tekinologia ya sayansi ifuatwe bila kuangalia ufundi wa masoko na unafuu wa bei na nguvu ya nchi kufanya manunuzi kwa pamoja kufute nguvu ya soko huria na usawa kati ya uzalishaji uuzaji na ununuaji ufikiwe kutokana na utafiti wa kisayansi.
Marxi
Kisiasa.
Marxism-Leninism waliunga mkono mfumo wa chama kimoja cha siasa kwa nchi nzima, chama hicho kitafuta sera za ujamaa na kuleta usoshalist katika jamii ya kijamaa. Nguvu na maamuzi ya chama yatawakilisha wengi kupitia kupitia uchaguzi wa kidemokrasia na utawala wa vitongoji mpaka taifa.