Marufuku, marufuku are we siriazi?

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170
1. 04-02-2006 - Mifuko ya plastiki marufuku

Source Bofya hapa
Serikali imechukua hatua kali na za haraka kudhibiti uharibifu wa mazingira nchini. Katika hatua hizo, serikali imepiga marufuku utengenezaji, uagizaji, uuzaji, ununuzi na matumizi ya mifuko ya plastiki laini na ile ya kufungia maji ya kunywa na maji ya matunda.

2. 07 September 2007 - Wauza mifuko ya plastiki watupwa jela Dar

Source Bofya hapa

3. 18 -01- 2011 - Pinda apiga marufuku mifuko ya plastiki

Source Bofya hapa

My Take:

1. Ina maana ile marufuku ya Dr. Shein ilikuwa imefutika (haifanyi kazi?)

2. Marufuku (Ban) za serikali ni lini zitaanza kuheshimiwa, nakumbuka pia kuna marufuku kuingiza gari ya abiria ikiwa na abiria kituo cha mafuta Vp imetekelezeka?

3. Hawa wakuu hawaoni wanaingia katika mtego wa kutoaminiwa na wala kutokuchukuliwa kiumakini matamko yao? Maana inaonekana ni kusemasema tu?

4. Hizi marufuku huwa zina lengo la kumfurahisha nani?
 
Unategemea hizo amri zitekelezwe na nani wakati wanaozivunja ni hao hao, kwani hawamjui mwenye kiwanda hadi waje kukimbizana na vibaka kariakoo wenye mifuko mitano mkononi ya sh. 100.
 
I liked this one.
 
Kauli za huyu mtoto wa mkulim mwenzetu huyu, uchungu wake kutetea maisha yetu duni na uthabiti wa hatua anazozichukua mimi tayari naona mdororo mkuuuubwa!!

Tena anapokubali kutangaza mambo ambayo yanatuongezea machungu ya maisha kama Dowans ao kutokuwajibisha mtu yeyote kashfa ya Arusha hapo tena ndio mimi wala!!!!!!!!
 
1. 04-02-2006 - Mifuko ya plastiki marufuku

Source Bofya hapa
Serikali imechukua hatua kali na za haraka kudhibiti uharibifu wa mazingira nchini. Katika hatua hizo, serikali imepiga marufuku utengenezaji, uagizaji, uuzaji, ununuzi na matumizi ya mifuko ya plastiki laini na ile ya kufungia maji ya kunywa na maji ya matunda.

2. 07 September 2007 - Wauza mifuko ya plastiki watupwa jela Dar

Source Bofya hapa

3. 18 -01- 2011 - Pinda apiga marufuku mifuko ya plastiki

Source Bofya hapa

My Take:

1. Ina maana ile marufuku ya Dr. Shein ilikuwa imefutika (haifanyi kazi?)

2. Marufuku (Ban) za serikali ni lini zitaanza kuheshimiwa, nakumbuka pia kuna marufuku kuingiza gari ya abiria ikiwa na abiria kituo cha mafuta Vp imetekelezeka?

3. Hawa wakuu hawaoni wanaingia katika mtego wa kutoaminiwa na wala kutokuchukuliwa kiumakini matamko yao? Maana inaonekana ni kusemasema tu?

4. Hizi marufuku huwa zina lengo la kumfurahisha nani?

So analytical and critical,duh
 
Unategemea hizo amri zitekelezwe na nani wakati wanaozivunja ni hao hao, kwani hawamjui mwenye kiwanda hadi waje kukimbizana na vibaka kariakoo wenye mifuko mitano mkononi ya sh. 100.

nani atawachangia hela za kampeni zao wakifunga viwanda vyao?
 
mkuu... source inasema hivi.......

"WAZIRI Mkuu wa Mizengo Pinda amesema ipo haja ya kupiga vita matumizi ya mifuko ya plastiki nchini kwa kuwa inachangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira.
Waziri Pinda alisema hayo mjini Dodoma juzi wakati akifunga mkutano maalum wa taifa wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa Tanzania (ALAT) ulifanyika kwa siku tatu".

pia pinda hajatoa specs za mifuko inayopigwa marufuku.... kama vile opp.., pp..,pop pep..... na sizes in microns 3microns au
 
Ukweli ni kwamba TZ hatuko serious na lolote lile -ukitaka kujua tembelea nchi hata majirani zetu mabao wako serious utagundua wao wakishapitisha inabaki utekelezaji sio majadiliano na uchakachuaji : mfano Rwanda
- wamesema Mifuko ya plastick marufuku -hupiti mpakani ukiwa na mfuko na inatekelezwa hivyo
- Wanasema kama sisi mwendesha pikipiki yoyote avae helmet- hutoki barabarani bila helmet yako na abiria. Hapa Tz trafic police anapanda pikipiki bila helmet na yuko bize anenforce traffic law.

Kweli tunahitaji Tanzania Mpya itakayokuwa serious
 
Back
Top Bottom