Marufuku kuuza damu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
waziri%20wa%20afya%20mwinyi.jpg


Waziri Dk. Hussein Mwinyi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Serikali imewatahadharisha na kuwakemea wahudumu wa afya wote wenye tabia ya kuuza damu kwa wagonjwa kuwa hatua kali dhidi yao zitachukuliwa.


Aidha hospitali zote zimeagizwa kuweka mabango yanayoonyesha kuwa damu haiuzwi, na wananchi wametakiwa kutoa taarifa kwa viongozi pindi wanapoona wahudumu wanauza damu.


Tadhari hiyo ilitolewa jana na Waziri Dk. Hussein Mwinyi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakati akitoa tamko la wizara hiyo kuhusu maadhimisho ya siku ya wachangia damu salama duniani ambayo huadhimishwa kila Juni 14 ambapo kitaifa hafla hiyo itafanyika mjini Moshi mkoani Arusha.


"...wizara yangu inakemea na kulaani kitendo cha kuuza damu kwa wagonjwa wakati inapatikana bure kwenye kanda zetu..." alisema na kueleza kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni 'kila mchangia damu ni shujaa'.


Dk. Mwinyi alisema kuwa tangu kuanza kwa mpango wa damu salama nchini 2004, kumekuwa na mafanikio mbalimbali yakiwemo ya ongezeko la vituo vya kanda kutoka vinne mwaka 2006 hadi vinane mwaka 2007.


Mafanikio mengine ameyataja kuwa ni ongezeko la ukusanyaji wa damu kutoka chupa 52,000 mwaka 2005 hadi 140,000 mwaka jana ambapo mahitaji halisi kwa mwaka ni wastani wa kati ya chupa 350,000 na 400,000 ingawa malengo yaliyopo katika kipindi cha mwaka huu na mwaka ujao ni kati ya chupa 180,000 na 200,000.


Alisema mafanikio mengine ni kupungua kwa kiwango cha virusi vya Ukimwi kwenye damu inayokusanywa na vituo vya damu salama kutoka asilimia saba mwaka 2005 hadi asilimia moja mwaka jana na uanzishwaji wa mfumo mpya wa teknolojia ya habari na mawasiliano unaosimamia shughuli zote za upatikanaji wa damu salama.


Hata hivyo, alisema kumekuwepo na changamoto nyingi zikiwemo za mahitaji makubwa ya damu kuliko upatikanaji wake, uelewa mdogo wa jamii kuhusu suala la uchangiaji wa damu kwa hiari, uuzwaji damu usio halali, matumizi yasiyo sahihi ya damu katika hospitali na miundombinu hafifu hasa ya barabara.


Dk. Mwinyi aliziomba taasisi mbalimbali na viongozi wa serikali, siasa, dini na jamii kushirikiana na serikali katika jitihada hizi ili kunusuru maisha ya wahitaji wa damu.


Kuhusu maambukizi ya Ukimwi, alisema takwimu zinaonyesha kuwa asilimia kati ya tano na 10 ya maambukizi hayo husababishwa na mgonjwa kuongezewa damu yenye virusi vya ugonjwa huo ingawa yapo magonjwa mengine kama vile virusi vya homa ya ini na kaswende.


Maadhimisho hayo ambayo kidunia yanaadhimishwa mjini Seoul, Jamhuri ya Korea, madhumuni yake hasa ni kuwashukuru na kuwashawishi wachangiaji damu kujiheshimu ili waendelee kufanya hivyo, kuwatia moyo wasiochangia kufanya hivyo na kuwahimiza wafanyakazi wa huduma za damu kuwatambua wachangiaji.
CHANZO: NIPASHE
 
Mabango mabango.. yako ya USITOE RUSHWA, DAI RISITI, USIKOJOE HAPA, na sasa DAMU HAIUZWI.... Tanzania bana eti sheria zinatekelezwa na mabango
 
Serikali ilikuwa inaelewa siku nyingi hili suala la kuuza Damu wakati wananchi wake wanajitolea kutoa damu bure. Ninatoa pongezi kwa Waziri wa afya kwa hilo ajitahidi sio kuzungumza pasipo na Vitendo. wanaoumia Masikini wanaofaidika ni wachache wenye pesa mkuu............. Evarm
 
Last edited by a moderator:
hivi alishamalizaje kashfa ya mabomu gongo la mboto?
Kamuachia Rais wake huo mzigo wa mabomu mkuu Rais ndio anayejibu yeye hayopo tena Gongolamboto yupo muhimbili ukimuhitaji nenda huko hata hao waliokufa kwenye Mabomu ya gongolamboto wanakimbilia wapi kama sio muhimbili? ............. Janjaweed
 
Last edited by a moderator:
ngonjera tu hizi....
Mawaziri wa bingikwa iukemea kwenye vyombo vya habari hawajambo.....
Mkuu ni kweli lakini Wakati wa Uchaguzi tunawachaguwa hao hao tunao wasema kuwa ni wabaya Sisi Wa Tanzania tupo kwenye Usingizi Mzito tukisha pewa hongo wakati wa Uchaguzi basi tunasahau shida zetu na kuwachaguwa hao hao Viongozi mafisadi na wala rushwa tuamkeni Ndugu zangu Wa Tanzania kuwachaguwa viongozi imara wanaoipenda nchi yao na Walala hoi ...................... BADILI TABIA
 
Last edited by a moderator:
Wanaongea wakiwa wamekaa huko maofisini wakati wanajua kuwa hayatekelezeki......huwa inatangazwa damu bure lakini ukienda hospitali unalipishwa na vile mwenye shida ni wewe inabidi kulipia manake ukicheza atapoteza maisha ya mgonjwa wako........wao wanatibiwa india hawayajui haya.......haya ni yetu sie walala hoi MziziMkavu!
 
Last edited by a moderator:
hiki kitu ni kigumu sana chukulia mgonjwa wako anahitaji kuongezewa damu unaambiwa bank ya damu imeisha utafanyaje? na ukitoa kidogo unaona damu inapatika ukweli nchi yetu tumeshakosa utu, na uzalendo ndio maana haya yote yanatokea rushwa imekuwa ndio mhimili wa maisha ya binadamu na wala si kufanya kazi.
 
Mh.Dr. Mwinyi, suala hili la MABANGO ni kuwa yalishawekwa siku nyingi. Suala linalofuata; je, maagizo yenu yanafanya kazi? Au pengine Mabango ndo kitu cha kuwatia hofu madaktari humu nchini...! Nashauri maagizo yenu yasiwe yanaishia majukwaani bali fuatilieni kwa SIRI muyaone wenyewe yale mnayoagiza kama yanatekelezwa ama la.
 
Back
Top Bottom