Marufuku kupeperusha bendera za chama Morogoro

Shembago

JF-Expert Member
Aug 20, 2011
332
50
Wakuu,

Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imetoa barua na kuzigawa katika vyama vya Siasa target yao ikiwa Chadema eti ni marufuku kwa bendera za vyama kupepea ndani ya Manispaa,sababu eti maeneo ni ya serikali na kuna wananchi hawana chama! Kama mtakumbuka nilieleza kasi ya Chadema katika kufungua matawi ndani ya Manispaa ilinashika kasi kubwa na hilo limewashtua magamba haswa haswa lilie la kata ya kichangani,ambapo Viongozi wa magamba walipita uck na kushusha bendera zote za chama cha chadema na wakati mwingine wanatoa hela kwa vijana wachovu ili kutekeleza hayo!

Leo tamko hilo limejibiwa na katibu wa chadema Wilaya na Ishallah this week nitatoa huma JF barua ya Manispaa na majibu ya chadema kwenda manispaa.

Hivi namna hii kweli tutafika? naomba magamba wasome alama za nyakati kwa uchaguzi wa juzi tu pale senegal.

Nawakilisha,
 
Wakati ule wa vijiwe vya wakereketwa kutandaza bendera za CCM kila kona manispaa ilikuwa na wakazi wa CCM tu, ila sasa CDM wanavyoongeza kasi basi ndiyo kuna mchanganyiko wa wakazi wenye itikadi mbalimbali na wasio na itikadi. Inapoelekea tutaambiwa tusivae magwanda sasa.
 
Naunga mkono hoja ya manispaa ya morogoro, unaweza kuweka bendera sehemu nyingi kama masokoni madukani na ofisi binafsi sio ofisi za serikali.
 
Mwambungu bado DC hapo?kama yes sitashangaa huwa simwamini yule kwa maamuzi yenye ueledi,thats nonsense kuhangaika na bendera
 
Hawa Magamba wananichekesha, wananikumbusha ya kule Tunduma ambapo DC usiku wa manane akiwa na pajama alikwenda KUIBA bendera za CDM eneo la sokoni, lengo ikiwa kumdanganya VP kwamba Tunduma hakuna CDM wakati MB wa Mbozi Mashariki ni wa CDM.

Dawa ya ujinga huu ni 2015 kuikabidhi manispaa ya Morogoro kwa CDM.
 
Jackson Michael wao wanamaana mpaka nyumbani kwako ni eneo la serikali,maana mpaka huko sokoni wamekataza,Hawa jamaa ni waajabu sana ofisi zote za magamba yalikuwa maeneo ya wazi wakabadili matumizi kwa maguvu,viwanja vya michezo jamhuri Stadium ikiwemo wananchi wote walichangia leo kiwamja ni cha magamba,hayo hawayaoni wanaona bendera za chadema!
 
yesu alipo zaliwa erode akauwa watoto wa kiume wote akidhani atamuua yesu kumbe hakuweza.sasa na hawa magamba wanadhani watamuua chadema kumbe hawataweza kufanya hivyo
 
Jackson Michael wao wanamaana mpaka nyumbani kwako ni eneo la serikali,maana mpaka huko sokoni wamekataza,Hawa jamaa ni waajabu sana ofisi zote za magamba yalikuwa maeneo ya wazi wakabadili matumizi kwa maguvu,viwanja vya michezo jamhuri Stadium ikiwemo wananchi wote walichangia leo kiwamja ni cha magamba,hayo hawayaoni wanaona bendera za chadema!

Huyo JM ni gamba
 
Huyo JM ni gamba

Hata alicho post sidhani kama anakielewa!JM itakua ni gamba sugu maana magamba ndio uwa wana tabia ya kukurupuka na kusupport chochote bila hata kuelewa,ili mradi tu kimesemwa na kiongoz wa c.c.m au wa serikali!ila kwa ili C.c.m wanachekesha,yaani wameishiwa mbinu kabisa,na tatizo hawaamini kama watu wa Moro wangegeuka ghafla hv na kusombwa na upepo wa chadema,ndio maana wamechanganyikiwa na wanakurupuka,Moro ilikua ngome ya c.c.m lakini sasa imegeuka,na hiyo amri yao haitatekelezeka,maana ina kinzana na uhuru wa kila raia ktk kujiamulia awe ni mwanachama wa chama gani cha siasa,mwenyewe nyumbani kwangu nina bendera ya cdm japo ni ndogo,na sitaitoa,nasubiri hao watu wa manispaa waje kuniingilia,naishi kolla hill
 
CCM watoe upumbavu wao, na kesho ntafata bendera ya CDM kongwa nije niifunge nyumbani basi ili tuone kama na nyumbani watasema sio wote wana CDM, CCM acheni upuuzi kama mnabisha kesho njoo mazimbu FK home mtaikuta bendera juu.
 
Naunga mkono hoja ya manispaa ya morogoro, unaweza kuweka bendera sehemu nyingi kama masokoni madukani na ofisi binafsi sio ofisi za serikali.
Ungeelewa mada kwanza ndipo ukurupuke kujibu. Imekatazwa kuweka bendera ndani ya manispaa ya morogoro na si ofisi za manispaa. Kwa lugha nyepesi kwa vilaza manispaa ni ndani ya mipaka yote ya manispaa from Kingolwila to mzumbe e.t.c. No parties flags (Du udikteta unaanza polepole!!!!!)
 
Just for CURIOSITY hivi zilizopigwa marufuku ni bendera za vyama tu? Au hata bendera za Simba na Yanga. Kama sababu ni kwamba kuna wananchi hawana chama, pia kuna wananchi ambao sio wapenzi/mashabiki wa Simba wala Yanga?!
 
Kwa mtindo huu basi na wapige marufuku kuuza kitimoto ndani ya manispaa maana kuna watu hawatumii hiyo kitu. Pia wasisahau kupiga marufuku bar maana watu wengine hawatumii kilevi. The list goes on and on and on.....
 
Back
Top Bottom