Marufuku kukojoa hapa

aduwilly

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
1,176
305
Jamaa mmoja alikuwa ameshikwa na tumbo la kuhara, basi kwa bahati nzuri aliona uchochoro hivyo aliamua kwenda kujistahi, kufika pale akakuta kibao kimeandikwa 'marufuku kukojoa hapa'. Jamaa akaamua kushusha mzigo eneo lile kwani ingekuwa ngumu kwenda mbali baada ya mzigo kuwa ushawasha indiketa.
Basi vile anamalizia tu, mlinzi akatokea na maongezi yao yakawa kama ifuatavyo

Mlinzi: Zoa mzigo wako kwa mikono kisha lipa faini elfu 50.

Jamaa: Unajua kusoma?

Mlinzi: Ndiyo

Jamaa: Hebu soma hicho kibao hapo

Mlinzi: Marufuku kukojoa hapa

Jamaa: Umenikuta mimi nimefanyaje hapa?

Mlinzi: Umeachia haja kubwa

Jamaa: Sasa

Mlinzi: (Kimya)

Jamaa taratibu akasepa zake
 
Jamaa mmoja alikuwa
ameshikwa na tumbo la kuhara, basi kwa bahati nzuri aliona uchochoro
hivyo aliamua kwenda kujistahi, kufika pale akakuta kibao kimeandikwa
'marufuku kukojoa hapa'. Jamaa akaamua kushusha mzigo eneo lile kwani
ingekuwa ngumu kwenda mbali baada ya mzigo kuwa ushawasha indiketa.
Basi vile anamalizia tu, mlinzi akatokea na maongezi yao yakawa kama
ifuatavyo

Mlinzi: Zoa mzigo wako kwa mikono kisha lipa faini elfu 50.

Jamaa: Unajua kusoma?

Mlinzi: Ndiyo

Jamaa: Hebu soma hicho kibao hapo

Mlinzi: Marufuku kukojoa hapa

Jamaa: Umenikuta mimi nimefanyaje hapa?

Mlinzi: Umeachia haja kubwa

Jamaa: Sasa

Mlinzi: (Kimya)

Jamaa taratibu akasepa zake

wangeandika marufuku kujisaidia!
 
Hajakutana na mlinzi kichaa, anakugonga malungu ya kutosha halafu ndo anakwambia zoa uondoke na mzigo wako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom