sasa kama nataka kusafiri safari ndefu na inanilazimu nibebe mafuta ya ziada ndio nafanyaje?
Hapo ndipo tunapoona kuwa nchi haina viongozi wanaofikiria beyond their own interests. Ningekuwa mimi ni muhusika ningesema mtu asiuziwe mafuta kwenye kidumu mpaka aoneshe kadi ya gari au aje na gari kituoni au aoneshe leseni au risiti ya kumiliki chombo kinachotumia mafuta ambacho hakiondosheki. Ukweli ni kwamba sheria hii ya kijinga inatekelezwa na wenye vituo kwa sababu inawapatia mwanya wa kuwaibia wananchi through faulty pumps. Kamaa ingekuwa inawabana wasingeitekeleza asilani. Nafikiri wahusika wanatakiwa kuja na tamko jipya kuhusu huu upuuzi. Maamuzi ya kukurupuka ni mabaya sana, walitakiwa kufanya utafiti kwanza wa kwa nini wtu hutumia vidumu?. Je kuna petrol stations za kutosha kwenye barabara kuu?, halafu wajiulize je kuna usalama katika barabara kuu kwa mtu kutembea na kiasi kikubwa cha pesa ili kununulia mafuta?, majibu yote haya ndiyo yangepelekea kuana na maamuzi sahihi.