Marufuku kubeba petroli kwenye vidumu

Hawana lolote hao, wao c wana uhakika wa mafuta ya bure, inamaaana nikipatwa na emergence nifanyeje? gari ni chombo cha moto, muda wowote chaweza kupata madhara...au kuishiwa mafuta..they should thnk b4 imposing they r stupid lawz.
 
Nafikiri wana lengo la kuwalinda wenye sheli ambao mara nyingi wamekuwa wakitupunja mafuta wanapojaza moja kwa moja kwenye gari. Sasa baada ya watu kugundua na kuamua kutumia vidumu, wameona wapitishe hiyo sheria. Kwa maneno mengine hiyo sheria inamnufaisha mwenye sheli zaidi

Pili hoja mojawapo waliyotoa kuwa ni kuzuia uchakachuaji, haina mashiko kabisa. mtu atachakachua vipi kidumu cha lita 5 au 20 alichonunua mwenyewe

Tatu, Matukio karibu yote ya mlipuko wa mafuta hapa kwetu yalitokana na ajali za magari yanayosafirisha mafuta hayo. Badala ya wao kudhibiti eneo hilo kuhusu usalama wa tanker zinazosafirisha mafuta, wao wanahangaika na vidumu, it is nonsense, labda kama wana sababu zingine.
 
Pump attendants wamepata ulaji. Itabidi wahongwe buku ili waweke mafuta katika vigaloni.
 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA), imepiga marufuku matumizi ya chupa za plastiki (vidumu) kuhifadhi au kubebea mafuta jamii ya petroli, kwa kuwa zina uwezo mkubwa wa kulipuka.

Pia imewataka wauzaji wa nishati hiyo katika vituo vyote vya mafuta nchini, kukataa kuhudumia wateja watakaohitaji petroli bila kuwa na magari yao vituoni kama njia ya kuwaelimisha juu ya athari za matumizi ya chupa au vidumu hivyo

Source: Habari leo


Maoni yangu

  1. Sisi tunaotumia magenereta kwenye biashara zetu na majumbani tufanye nini?
  2. Sheria hii inataka kutuaminisha kwamba mwenye gari akiishiwa mafuta ghafla basi ni mzembe. Tuchukulie mazingira kwamba umebakiwa na mafuta kidogo kwenye gari, lakini yanatosha kufika sheli iliyo umbali wa kama KM 25, then unafika na gari yako kwenye sheli hiyo, unakuta mafuta wameishiwa au hawa operate. The next sheli ni KM 25 zingine, uliskume gari mpaka huko?

Hawa wapuuzi kazi muhimu ya kudhibiti uchakachuaji na upandishaji bei holela imewashinda kwa kuwa mabosi wao ndiyo culprits, sasa ili waonekane wanafanya kazi wanageukia watumiaji (consumers). Tanzania kweli ni nchi ya ki "authoritarian", badala ya kufanya kampeni kwa umma kwenye TV na matangaza ili kuwaelimisha wawe makini na matumizi ya highly flamable petroleum products, wao kwa uvivu wa kufikiri wanakuja na marufuku what a rubbish!.

Ni nani asiyejua hali za watanzania kiumasikini na je gari likizimika katikati ya balabala kwa fault ya gauge kusoma wrong kuhusu mafuta huku yameisha likae hapohapo kusubiri breakdown hata kama kituo cha mafuta kipo metre 200?. Hii marufuku imeletwa ili kuwapanulia wigo wa rushwa watendaji wa Ewura ili wawapige fine wenye vituo vya uchochoroni kwa kuuza mafuta kwenye vidumu wakati vituo vya vigogo vikipeta. Tanzania tunahija Tsunami kuliko ile ya Japan ili kuisafisha system.
 
Bila kuogopa naweza kusema kwamba waliotoa tamko ni wapumbavu na hawana uhalisia wa hali ya mtanzania wa kawaida.... itabidi sasa majenereta tuyabebe kwenye bajaji kuyapeleka petrol stations

hivi hawa watu wanafikiria kwa kutumia nini?

akili zao ni jinga kabisa.
Wanakurupuka tu.
Khaa!
 
Hawa jamaa si ndio wanalipiwa 200USD per month kwenye gym?..kwa hela wanazopata kwa wafanyabiashara wa petroleum products! Watz hatujafikia huko...na yale majerican wamezuia?
 
Nawashauri EWURA watoe elimu ya kutosha kwa wadau kuhusu madhara waliyoyaona ili majanga ya milipuko ya mafuta yasitokee na sio kukaa tu ofisini na kutoa miongozo yenye utata kama hii. Pia nawashauri EWURA wafanye ziara za kushtukiza mara kwa mara kwenye vituo ili kudhibiti vipimo sahihi vya mafuta kwa wateja na kupelekea kupunguza idadi ya vudumu kwenye vituo vya mafuta.
 
Kutokana na kauli ya ewura ya kwamba, kwa yeyote yule kwenda na kidumu kununua mafuta sheli asiuziwe na badala yake mashine husika ndo iwekewe iwapo sheli. Je inamaana watu waende na majenereta kununua mafuta.?
 
tanesko wat2tese na mgao ununue jenereta yako kwa shida unataka kuweka lita 2 usukume cku unaambiwa uende nayo sheli inamana utafute pesa ya taxi na hapo wakuibie na kalita 1 mana ukiweka kwenye dumu ngumu kuibiwa kweli 2tafika je sio njama za wenye sheli na eura
 
dira ya kigari chako cha mkopo haifanyi kazi, gari inakuzimikia kisa mafuta hakuna, unafungua buti, unatoa kidumu cha rita 5 haraka unaenda kituoni ili ununue mafuta safari iendelee, ghafla muuza mafuta anakwambia ni marukufu kuja na vidumu hapa, unamueleza hali ulitonayo kuwa gari imekuzimikia hivyo huna jinsi HATAKI KATUKATU. ghafla linakuja daldala limejaZa watu pomoni. anakuacha wewe pale unashangaa anakwenda kumuhudumia konda wa daladala. WANA JF nisaidieni hivi ile sheria ya kujaza mafuta huku gari likiwa na abiria imefutwa.....? NA HII YA KUTONUNUA MAFUTA KTK VIDUMU NDIO MBADALAAAAA..........?
 
Tatizo la viongozi wasio na akili kuwaza kwa kuzunguka na kiti ofisini bila kujua mazingira ya Mtanzania hawajui wapo wanaotumia jenereta kupata maji hasa kwa wale wanaotumia pump kwa ajili ya kuvuta maji.Hiyo sheria waliyoipitisha nnaipinga mwanzo mwisho hata kwa nguvu ikibidi
 
unajua wanaopitsha haya ni mafisadi hivyo ugumu wa maisha hawaujui,wao wakienda sheli ni full tank,sasa akina sisi wenye hela ya kuunga unga ndio inakuwa balaa!
 
  • Thanks
Reactions: Obe
na kale kamashine kangu ka kusaga pale nyumbani nikitaka mafuta lazma nikabebe niende nacho sheli!!?
 
huyu aliyetoa hilo wazo la kutokwenda na kigalon ni mpumbavu sana.......narudia......ni punguwani wa kutosha......mtu mzima huwezi fikiria upumbavu wa namna hiyo.......badala ya kutumia ubongo anatumia......nanihii (nimeihifadhi}.....$#^@@@*
 
dira ya kigari chako cha mkopo haifanyi kazi, gari inakuzimikia kisa mafuta hakuna, unafungua buti, unatoa kidumu cha rita 5 haraka unaenda kituoni ili ununue mafuta safari iendelee, ghafla muuza mafuta anakwambia ni marukufu kuja na vidumu hapa, unamueleza hali ulitonayo kuwa gari imekuzimikia hivyo huna jinsi HATAKI KATUKATU. ghafla linakuja daldala limejaZa watu pomoni. anakuacha wewe pale unashangaa anakwenda kumuhudumia konda wa daladala. WANA JF nisaidieni hivi ile sheria ya kujaza mafuta huku gari likiwa na abiria imefutwa.....? NA HII YA KUTONUNUA MAFUTA KTK VIDUMU NDIO MBADALAAAAA..........?

Huelewei sababu ya kutokuuziwa mafuta kwenye vidumu? Pumps nyingi sana zimechakachuliwa na hazitoi mafuta kama meter inavyosoma. Sasa ukinunua mafuta kwenye kidumu utagundua mchezo wao. Meter inasema umenunua lita tano lakini kidumu kimeingiza lita tatu na nusu. Ndio maana wengi wa mataxi drivers hununua mafuta yao kupitia vidumu.
 
huyu aliyetoa hilo wazo la kutokwenda na kigalon ni mpumbavu sana.......narudia......ni punguwani wa kutosha......mtu mzima huwezi fikiria upumbavu wa namna hiyo.......badala ya kutumia ubongo anatumia......nanihii (nimeihifadhi}.....$#^@@@*

Preta tusimlaumu sana huyu aliyetoa wazo, yeye alikuwa anatekeleza maagizo. Muasisi wa hii issue ni CCM na serikali yake, baada ya kuona yanayotokea Middleast na maandamano ya CDM basi wakaona kuwa vijana wanaweza kuanza kutengeneza mabomu ya Petrol na njia pekee ya kudhibiti upatikanani wa Petrol ni kuwataka wauzaji kuuza kwa wenye magari tu, swali likaja how?, wakaona waweke kisingizio cha usalama wa raia na kuwataka wasimuwekee mtu asiyekuwa na gari( kwenye kidumu), na kwa kuwa wauza mafuta wengi ni wezi wakubwa yaani lita kumi unawekewa saba na kwa kuwa huwezi kuona kwenye Tank kuna nini wameipokea kwa shangwe amri hii kwani inawahakikishia muendelezo wa utapeli. Huu wote ni uoga wa kiinteligensia wasitudanganye kuwa ni kwa ajili ya Public safety wakati wanatoa vibali vya vituo vya mafuta kujengwa kwenye makazi ya watu.
 
sasa kama nataka kusafiri safari ndefu na inanilazimu nibebe mafuta ya ziada ndio nafanyaje?
 
Back
Top Bottom