Marudio ya uchaguzi

KUCHI

Member
Dec 27, 2010
83
46
Wana JF naombeni mawazo yenu juu ya chaguzi za marudio. Kwa mujibu wa katiba ya sasa na sheria ya uchaguzi iliyopo , pindi ubunge unapobatilishwa na mahakama kama ilivyo kuwa arusha mjini na sasa igunga, tume ya uchaguzi inatakiwa mara moja kutangaza kuwa jimbo lipo huru na kisha kuanzisha mchakato wa uchaguzi. Maoni yangu ni kuwa kwakuwa kumbukumbu za tume ya uchaguzi zinaonyesha kuratibu uchaguzi katika jimbo moja inagharimu takribani zaidi ya shilingi Bilioni kumi , sasa wazo linakuja kwamba kwakua kila aliyeshindwa anayo haki ya kikatiba kupinga matokeo mahakamani na kwa hivyo upo uwezekano wa majimbo mengi kubatilishwa matokeo chini ya mwavuli wa mahakama je si bora katiba ikatamka kuwa iwapo mbunge aliyeko madarakani akiondolewa kwa amri ya mahakama basi badala ya kufanya uchaguzi mpya kwa gharama kubwa aliyemfuatia kwa wingi wa kura akapewa ubunge rasmi ?
 
Back
Top Bottom