Marin Hassan wa TBC jichunguze...

Wa mjengoni, kwanini unajitafutia maudhi? Why watch this TV station! Thank God mimi kwangu haipatikani!!
Ni TV Station yetu ingekuwa inazungumziwa ITV, hapo ungeweza kusema hivyo...kumbuka Marin ameajiriwa na watanzania siyo ya wana-CCM kama vipi CCM waanzishe TV station yao halafu wamwajiri huko au watuambie TBC ni mali ya CCM maana hawashindwi
 
Licha ya ujuaji wake,Marin amejaa dharau,na ubabe wa wazi wazi hadi kwa watangazaji wenzake yaani ni kichefuchefu hata kumuona anaongoza kipindi cha jambo :glasses-nerdy:
Acha woga wewe, mbona jamaa mshikaji tu. Sasa wewe kama umeenda halafu unaonesha kuchachawa hivyo ni kivyako. Lakini mshikaji yuko fresh tu na mi binafsi huwa nafagilia sana kipindi chake. Kama unajiamini na kile unachosema sidhani kama kunakuyumbishwa, ila kama wewe ni wakubumba ndo matokeo yake kayo hutakuwa na amani. Pole!
 
Tatizo la watu kama akina Marin ni kwamba wanalinda mifumo inayowakandamiza wao wenyewe. Huyu Mwandishi ukimuona kwenye kipindi utajua ameukata lakini ukimkuta anagombania daladala utadhani naye ni miongoni mwetu. Akipewa ziara tu ya kwenda na hao mafisadi yeye tayari meno nje.

Kama angekuwa mbwa angekuwa anabiligisha (kutikisatikisa) mkia kwa kwenda mbele

Au anapakatwa?
 
With time kama TBC kama Taasisi wanajirekebisha, leo tar 01/09/2010 niliweza kuona TBC ikicover hata wagombea wa vyama vya upinzani wanaotembea nyumba kwa nyumba.

Nashauri aliyeanzisha thread hii achukue hatua kuhusu matamshi ya Marin Hassan akitaja siku, tarehe na maneno ailyotamka na kwa kupeleka malalamiko hayo Baraza la Habari nakala TBC tuone kama hataacha kupayuka payuka
.

Hiyo ni haki ya wasikilizaji chini ya sheria zetu za habari.

JATROPHA,
Ni kweli wanaelekea kubadilika, lakini fikra na mitazamo yao ni duni. Binafsi niliangalia. Nilichoona ni kwamba mikutano ya Dr. Slaa hawataki kuonyesha umati wa watu, bali wanamuonyesha yeye tu na kijisehemu kidogo cha watu. Kama wana dhamira ya kweli kuwapa wagombea uwanja sawa, iweje JK anapewa coverage kubwa na wanajaribu ku-zoom zaidi umati wa watu.

Dr. Slaa alipokuwa Dodoma pale Kibaigwa walionyesha kipande tu kidogo cha watu na mbaya zaidi eneo waliokaa watoto.

Mimi nasema TBC1 ni mamliki wa CCM na hawajui walifanyalo.
 
Tuwekeeni picha ya huyo Marin na CV yake ili tumsome vizuri. Sisi ambao tuliacha kuangalia TBC siku nyingi hatumjui! Lakini kutokana na comment za wengi anaonekana ni **** fulani.
 
Siyo tu TBC1 walionyesha umati mdogo wa watu, vilevile walihakikisha kwenye coverage ya Kikwete, wanaunganisha na picha za ujenzi wa Barabara. Maoni yangu ni kuwa wamepewa amri kuwa kama ni lazima kufanya coverage ya Dk. Slaa basi negative elements zichomekwe na kwa upande wa Jk wahakikishe inapewa positive image. kama ulimsikiliza vizuri mtangazaji kabla ya kutupeleka maeneo husika ili reporters walete habari utaujua ubaya wa TBC1.

Tunataka fair coverage Lakini hata TBC1 msipoifanya naamini kuwa "IPO SIKU" mambo yatakuwa hadharani. OLe wenu mnaotumikishwa na Sisiemu na kuwasaliti watanzania.
 
Kwa Lipumba wanonyesha NGOMA! LOL!!! Tido Mhando nilikuheshimu sana ulipokuwa BBC! Lakini kwa sasa TBC1 imekuwa station ya watoto... Khaaaaa!!
 
ukikaa karibu na marine utapata harufu kali ya mdomo duh, hatari kweli kweli
 
Nakupongeza wa mjengoni kwa kuliona hilo, inavyoelekea kuna wandishi wanaoamini kuwa ccm itatawala daima na kwamba vyama vingine vyote ni haramu na havina haki ya kuungwa mkono. Hassan wa TBC ni kweli anahitaji kujichunguza zaidi na pia kupima kauli zake, inaeleweka wazi kuwa anachama anachokiunga mkono ila kwa aina ya kazi yake sio busara kuonyesha dhahiri kuwa ni mkereketwa wa chama fulani. Ile issue ya kunusurika kipigo pale jangwani siku ya uzinduzi wa kampeni za CHADEMA isimfanye aweke bifu la moja kwa moja.
 
Kwa Lipumba wanonyesha NGOMA! LOL!!! Tido Mhando nilikuheshimu sana ulipokuwa BBC! Lakini kwa sasa TBC1 imekuwa station ya watoto... Khaaaaa!!
hata watoto siku hizi hawaifagilii.....sababu kila wakati sisiem, sisiem sisiem......
 
With time kama TBC kama Taasisi wanajirekebisha, leo tar 01/09/2010 niliweza kuona TBC ikicover hata wagombea wa vyama vya upinzani wanaotembea nyumba kwa nyumba.

Nashauri aliyeanzisha thread hii achukue hatua kuhusu matamshi ya Marin Hassan akitaja siku, tarehe na maneno ailyotamka na kwa kupeleka malalamiko hayo Baraza la Habari nakala TBC tuone kama hataacha kupayuka payuka
.

Hiyo ni haki ya wasikilizaji chini ya sheria zetu za habari.

Naunga mkono.
 
Naona Marin Hassan AMENYWEA leo (3 Sept) nilikuwa namuangalia kwenye TBC1 wakati wa kusoma magazeti - hakutia neno hata moja uso umekuwa mwembamba kwa aibu. Siku CHADEMA ikishinda huyu inabidi akatangazie kule MCHAMBAWIMA.
 
Siku ile kwenye uzinduzi wa wa kampeni za Chadema walipo kata mitambo TBC1 nilimpa ya ugoko mpaka alilia huyu Hasan Marin bahati yake polisi waliniwahi
 
Naona Marin Hassan AMENYWEA leo (3 Sept) nilikuwa namuangalia kwenye TBC1 wakati wa kusoma magazeti - hakutia neno hata moja uso umekuwa mwembamba kwa aibu. Siku CHADEMA ikishinda huyu inabidi akatangazie kule MCHAMBAWIMA.

Ila ulimwona Agnes Mbapu alivyokuwa ankwepa mkusoma vichwa cya habari cya Chedema na Dk Slaa? Hadi nimeshangaa! magazeti karibu yote leo yana vichwa cya habari vikimhusidha Dk Slaa kumwambia Makamba akae kimya la sivyo atatoboa siri ya yeye kufukuzwa ualimu mkuu wa shule ya msingi....kismingi ni kuhusu ishu za ndoa ya Dt slaa

sasa cha ajabu mtangazaji akawa anakwepa main headlines anasome nyingine za ndani...nilikuwa najiuliza what is the point wakati kama unaangalia TV unaona kabisa!
 
Niliinyaka hiyo lakini mimi nilidhani wamezila (yaani wamewanunia CHADEMA).
 
Back
Top Bottom