Edwin Mtei
Senior Member
- Dec 13, 2008
- 181
- 342
Katika mjadala unaoendelea wa marekebesho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuna malalamiko na lawama zinazoanzia Zanzibar kwamba mpangilio na utaratibu wa sasa umemshusha hadhi Rais wa Zanzibar na kumfanya Waziri wa kawaida tu ktk Cabinet ya Muungano. Malalamiko hayo yanaonyesha kutoridhika na utaratibu unaotambulika kikatiba kwamba mgombea wa kiti cha u-Rais akitokea Bara kuna mgombea mwenza atakayekuwa Mzanzibari, na wakishinda ndiye atakuwa Makamu wa Rais kama Makubaliano ya Muungano yalivyotamka awali mwaka wa 1964.
Lalamiko lingine ni kwamba kumekuwa na ma-Rais wanne wa JMT, lakini ni Rais mmoja tu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, aliyetokea Zanzibar. Licha ya kwamba Orodha ya Makubaliano ya 1964, hayakutamka hivyo, hawa Wazanzibari wanataka kuwe na zamu ya kupokezana uongozi mkuu wa JMT. Hawaridhiki na utaratibu wa kuwa na Mgombea mwenza ambao unahakikisha kwamba kama kiongozi mkuu akitokea Bara, makamu wake ni lazima atokee Zanzibar; na akitokea Zanzibar, makamu wake ni lazima atokee Bara.
Ni vizuri ifafanuliwe kwamba utaratibu wa kuwa na mgombea mwenza wa kiti cha u-Rais, sio tu unahakikisha Watanzania wote wanajumuishwa katika kumchagua Mkuu wa nchi yao pamoja na makamu wake, bali pia unaondoa uwezekano wa Makamu wa Rais kuwa ni mteule Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, kwa vile Bunge la JMT halidhibiti mashughuli ya Baraza hilo.
Aidha ieleweke kwamba katika mazingira ya vyama vingi vya siasa, inawezekana kabisa kwa chama cha siasa kinachoshinda ktk Uchaguzi wa Rais wa JMT, kisiwe kimeshinda pia na kupata u-Rais wa Zanzibar. Rais wa Zanzibar akiwa ni wa Chama kinachopingana kisiasa na kile kilichoshinda u-Rais wa JMT, haitawezekana yeye awe ni makamu wa Rais wa Mkuu wa nchi.
Kwa utaratibu wa sasa, mgombea mwenza Mzanzibari wa chama kishindi atakuwa ni Makamu wa Rais licha ya kwamba chama chake hakitakuwa kimeshinda na kuchukua Serikali ya Zanzibar. Rais wa Zanzibar akiwa tu ni Waziri wa kawaida anayehudhuria vikao vya Cabinet ya JMT kama Katiba ya sasa inavyosisitiza, hakutakuwa na matatizo.
Waumini wa demokrasia ya kweli wanaona kwamba mpangilio na utaratibu unaohakikisha kwamba sehemu ya Jamhuri ya Muungano ambayo jumla ya wakazi wake ni chini ya asilimia 5 ya Watanzania wote kuwa na uhakika (yaani Guarantee) ya kutoa Mkuu wa nchi au Makamu wake kila wakati, ni kujitolea tosha ili kuendeleza na kudumisha huo Muungano.
Katika nchi ambazo ni muungano wa dhati, hakuna taratibu za kuhakikisha sehemu fulani inashiriki katika uongozi, isipokuwa kuna uhakika wa haki sawa kwa kila raia na uongozi unatokana na uwezo binafsi anaouonyesha mgombea.
Matarajio yangu ni kwamba tutakapofikia lengo kuu la kuwa na Serikali moja ya JMT iliyochaguliwa bila kuwa na rushwa au ufisadi basi demokrasia ya kweli itakuwa imefikiwa.