Ruge Opinion
JF-Expert Member
- Mar 22, 2006
- 1,838
- 701
Taarifa zilizosikika kwenye vyombo vya habari ni kwamba marekani imeanzisha mkakati wa kuingilia mgogoro wa Uganda na Lord's Resistance Army. Watu wengi, akiwemo rais Museveni wa Uganda, wamehoji ni kwa nini Marekani imengoja muda wote huo watu wameuawa na kuteseka sasa ndiyo wanaamua kuingilia. Wao wanasema wanataka kupambana na ugaidi popote duniani. Je hii ni kweli? Mimi nahisi uamuzi wa Marekani umatokana na mafuta kugunduliwa Uganda. Ni mkakati wa kujiingiza humo ili hatimaye wao ndiyo wawe na maamuzi makubwa juu ya raslimali ile. Uganda isipokuwa macho huu ni mwanzo wa nchi hiyo kuanza kuonja joto ya oil curse. Mnasemaje waungwana?