Marehemu Nyaulawa, kuugua mpaka kufa kwake

he was great person by reading this thread...i didnt know him for sure!!! RIP
 
RIP Nyaulawa,

Nadiriki kusema kuwa yeye ndiye muasisi (indirectly) wa JF. Nadhani JF ni matokeo ya kufa kwa BCS baada ya discussions kule kuwa moto mno na hivyo kufungwa.


....so moto..tunaouona ukiunguza mafisadi leo hapa JF...ulianzia BCS iliyokuwa ikimilikiwa na NYAULAWA..thats good.....

MCHANGO WA NYAULAWA KUIBUA MAWAZO HURU HAUPINGIKI...IWE KUPITIA HIYO bcs, au MAJIRA ...gazeti la kwanza huru la kila siku tanzania.lilikuwa kikisambaza hadi copy 100,000 kwa siku na zikaisha zote..kuna wakati watu walikuwa wakilisubiri vituoni ili kupata mawazo huru yaliyokuwa hayaingiliwo na mmiliki.,.kuna wakati hata wana ccm walijiuliza kama mmiliki wa gazeti lile kweli alikuwa mwenzao?...wewe fikiria ...gazeti lililokuja baada ya ukiritimba wa uhuru ...na daily news..the only daily in tanzania by then.....waandishi waazilishi wa majira wengi leo wameendelea na kuwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari........wengine pia wametangulia mbele ya haki.....
 
Richard R.I.P

Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. sisiem walaaniwe kwa kifo chake kwani alidhaniwa ndio anafeed JF maana walidhani BCS ilikuwa seconded kwa invisible. will come back officially soon
 
RIP Nyaulawa.Jina la Bwana lihimidiwe.

Vikumbo sasa kwenye hilo jimbo,nafasi nyingine ya makamba na Mtikila
 
RIP Nyaulawa.Jina la Bwana lihimidiwe.

Vikumbo sasa kwenye hilo jimbo,nafasi nyingine ya makamba na Mtikila

Kuna sheria mpya hakuna by election ikibaki miaka miwili kufanyika uchaguzi mkuu.

Hivyo kiti hiki kitabaki wazi mpaka 2010
 
Lakini kama ilivyokawaida yetu, tunampa mtu sifa na heshima zake akiwa amefariki lakini akiwa hai huwa sifa hizo hatumpi. Why didn't we let the Tanzanians know about this before he died. That would be kind than what we are doing now.
 
``February 21, 1995

On the morning of Feb. 21, police arrived at the office of the independent daily Majira and arrested editor (Sam) Makila and publishers (Rashidi) Mbuguni and (Richard Saidi) Nyaulawa. The three were taken to the headquarters of the minister of internal affairs, where they were held for the day and interrogated as to their sources for a Feb. 19 article concerning a loan that the government was taking out in order to buy radar equipment, a loan for which it was allegedly using the Zimbabwe national gold reserve as collateral. They were warned that charges would be pressed if they did not reveal their sources, and on March 9 they were officially charged with sedition and disclosure of state secrets. The trial was postponed at least four times and is still pending. They face up to 10 years in prison if convicted. CPJ protested the charges on July 10.´´*

FEBRUARY 2, 1996

``Tanzanian authorities drop charges of sedition and withholding information against the former editor and publishers of the Kiswahili-language newspaper, Majira. The then-editor of Majira, Sam Makila, and the paper’s publishers, Rashidi Mbuguni and Richard Nyaulawa, were detained on February 22, 1995 before being charged in terms of the National Security Act. The police wanted Makila to reveal the source of a story Majira published three days previously exposing plans by the cash-strapped government to spend US$130 million on radar equipment. The court drops the charges because of a lack of evidence by the state.´´**

* Commitee to Protect Journalists, available at (press here)
** Freedom of Expression Institute, available at (press here)

______________________

Marehemu na wenzake walikuwa wa kwanza kuandika ufisadi wa radar. Sijui kama Bungeni aliwahi ku address ufisadi ule, pamoja na sheria za kidikteta za Sedition zilizomuweka kizuizini. I hope Business Times wata cover kikamilifu kazi za maisha ya marehemu, mchapishaji wao. Sidhani.

Nakumbuka vizuri Gazeti la Majira na magazeti dada yake ni miongoni mwa magazeti ya mwanzo yaliyokuwa yakiikosoa Serikali bila woga. Inasemekana Gazeti hili lilikuja kuwa tishio hadi serikali ikaona itafute namna ya kulimaliza. Yapo yanayosemwa serikali ilikuwa na mchango wake katika kuanzishwa kwa gazeti la Rai lililokuwa likimilikiwa na kina Jenerali Ulimwengu, Salva Rweyemamu, Gideon Shoo, Johnson Mbwambo, Shabaan Kanuwa na Marehemu John Homisdas Rutayisingwa. Ulimwengu na wenzake waliigeuka Serikali na kulifanya Rai kuwa ‘moto mkali’ kupita Majira. Mkapa aliwahi kuonyesha hasira zake hadharani akihoji Waandishi nao waeleze fedha za kuanzisha Vyombo vyao vya habari walizipata wapi! (Inasemekana hapa aliwalenga moja kwa moja akina Ulimwengu)

Gazeti la Majira liliendelea kupoteza umaarufu nadhani kuna mitego ambayo serikali ilitega na kufanikiwa kulinasa! Labda mojawapo ndio hii ya Muheshimiwa kujiingiza kwenye Siasa za chama tawala! Nani amelisahau gazeti la Sanifu? Wadadisi wa mambo wanajadili kuwa hata nguvu za ‘Mzee Puch’ pale UD zilimalizwa na Sanifu. Kwa kuwa‘mambo’ yote sasa yalikuwa yakianikwa hadharani Nchi nzima na sio kwenye kuta ‘chafu’ za UDSM. Ipo siku gazeti la Sanifu halikuzwa mitaani na taarifa za ndani zinasema mfanyabiashara mmoja anayemiliki pia vyombo vya habari ilibidi anunue nakala zote kuficha ‘ishu nzito’ iliyokuwa imechapishwa! Mtakumbuka huko Majira/Sanifu ndiko alipoibukia Masoud Kipanya! Mnakumbuka ule uchaguzi wa Temeke alivyokuwa akimchora Marehemu Brother Ditto! Nakumkumbuka uchaguzi ulipokwisha na Mrema kuibuka mshindi, Ditto alikwenda ofisi za Majira kumpa pongezi binafsi KP!

Mungu iweke Roho ya Marehemu Nyaulawa Mahala Pema Peponi. Binafsi nakumbuka nimewahi kukutana na Marehemu katika mafunzo mbali mbali ya Ujasiriamali yaliyokuwa yakiandaliwa na taasisi moja ya Uholanzi ijulikanayo kama IICD yeye akiwa kama mwelekezi. Hakuwa na makuu kabisa hasa pale nilipotaka ushauri katika fani ya vyombo vya habari aliyokuwa akishiriki kikamilifu.
 
Lakini kama ilivyokawaida yetu, tunampa mtu sifa na heshima zake akiwa amefariki lakini akiwa hai huwa sifa hizo hatumpi. Why didn't we let the Tanzanians know about this before he died. That would be kind than what we are doing now.

I suppose ukimpa sifa mtu kabla hajafa sifa nyingine hutazitoa.Its better baada ya kufa unazikusanya zote. Ila binadamu tuna tabia ya kuwasifu wafu hata kama walikua wabaya!! Mh. Nyaulawa alitenda mengi mazuri.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom