Marehemu mzee omari suleiman (1910 - 2012) shujaa wa uhuru wa tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,912
30,253
MzeeOmar Suleiman (1910 - 2012) Mwasisi wa TANU Dodoma

MohamedSaid
Katika moja yamisiba mikubwa ya Tanzania ni kukosekana kuwapo kwa historia ya kweli yakupigania uhuru na kwa ajili hiyo kusababisha kutokuwapo kwa mashujaa wa taifa.Mzee Omar Suleiman ni mmoja wa waasisi wa TANU Dodoma na kwa ajili hii ni katiya mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika ambao si wengi wanamfahamu nakujua khasa nini ulikuwa mchango wake. Mara kwa mara hasa kwa siku hisi zamwisho wa maisha yake kila ilipotokea nafasi ya kutaja Mzee Omar Suleimankilichokuwa kikielezwa ni uhusiano wake na Julius Nyerere na kusema kuwaNyerere alikuwa akifikia nyumbani kwake basi. Nini ulikuwa mchango wake haukuwauanelezwa na sababu khasa ni kuwa hakuna aliyekuwa anaujua. Hata alipokufahakuna taazia yoyote iliyosmdikwa kumweleza Omar Suleiman alikuwa nani. Ili kumjuaOmar Suleiman ni lazima mtu arudi nyuma sana na kumtafuta Omar Suleima katikakundi la wazalendo wenzake aliokuwanao katika siasa wakati wa kuiunda TANUJimbo la Kati mwaka wa 1955.Kuipata pichaya siasa katika Tanganyika ya 1950 hatuna budi uitazama African Associationmtangulizi wa TANU.

African Association mjini Dodoma ilikuwa ikiongoza katikaharakati baada ya Vita Kuu ya Pili. Ilikuwa na wanasiasa wenye juhudi sana nawabunifu kuliko wanasiasa wengine wote waliopata kutokea katika historia yaTanganyika. Wanasiasa hawa walikuwa Ali Ponda, Mmanyema na Hassan Suleiman,Myao, rais na katibu wake. Mwaka 1945 Ali Ponda alitoa wito kwa Waafrika wotekuungana kama umma mmoja. Lakini kuanzia mwaka 1948 harakati za siasa mjiniDodoma zilififia, na TANU ilipoanzishwa mnamo Julai, 1954, tawi la TAA Dodomalilikuwa limedorora kiasi kwamba kilishindwa hata kupeleka mjumbe kwenyemkutano ule wa TAA wa kuundwa kwa TANU. Pamoja na ukweli kuwa mji wa Dodomakulikuwa na Kikuyu Secondary School (sasa Alliance Secondary School) ambakokulikuwa na walimu wa Kiafrika, wengi wao kutoka Makerere, ambao kama wasomi,wangechukua juhudi kuihuisha African Association.

Labda kwa kuhisi kuwahapakuwapo na ukinzani unaokwenda kinyume na maslahi yao katika mfumo wa kikoloni, walimu wale waliamua kujitenga nasiasa. Kwa hiyo basi, harakati dhidi ya serikali ya kikoloni ziliachwa kuwa mikononimwa wa Waislam wa mjini Dodoma, wengi wao wakiwa hawakujaliwa kupata elimu kaajili ya siasa za Waingereza walioacha elimu iwe mikononi mwa Wamishionari.
Historia yaMzee Omar Suleiman haiwezi kukamilika bila ya kumtaja rafiki yake shujaa wauhuru marehemu Haruna Taratibu. Mwaka wa 1953 Haruna alikuwa na umri wa miaka 23 na akifanya kazi Public Works Department (PWD) kamamwashi. Haruna Taratib alijaribu kuunda chama cha wafanyakazi kwa kuwahamasishana kuwakusanya vibarua walioajiriwa katika kazi za ujenzi. Kwa sababu yaharakati hizo za kutaka kuanzisha chama cha wafanyakazi, Taratibu alionekana nawakoloni kama mtu mkorofi na mzusha vurugu.

Hata hivyo Taratibu hakufanikiwakuanzisha chama hicho na matokeo yake akapewa uhamisho kwenda Singida kamaadhabu. Taratibu alivutiwa sana na harakati za Mau Mau nchini Kenya na alizoeakufuatilia matukio yake katika gazeti lake alilokuwa akilipenda sana, "Baraza,"gazeti la Kiswahili la kila wiki kutoka Kenya.
Ilikuwa katikaNovemba 1954 wakati Taratibu alipokuwa akipekuapekua gazeti hilo ndipo alioposomahabari kuhusu TANU. Taratibu aliuliza pale Singida mjini kama kuna tawi laTANU. Taratibu alifahamishwa kukuwepo kwa tawi la TANU pale mjini na katibu wake alikuwa mzee mmojakwa jina la Mzee Kinyozi. Taratibu alikata kadi yake toka kwa huyo mzee naakawa mwanachama wa chama cha siasa. Asubuhi iliyofuata Taratibu aliingiaofisini kwake na akaiweka kadi yakeya uanachama wa TANU yenye rangi nyeusi na kijani juu ya meza yake, kilamtu aione. Ofisa Mzungu wa PWD Singida hakuweza kuvumila ufedhuli kama ule,alishauri Taratibu apewe uhamisho kurudi Dodoma alikotoka, kabla hajaeneza sumu yake kwa Waafrika wengine. Hapo ndipoalipokuja kuungana na Mzee Omar Suleiman.Mwaka 1955wakati wimbi la utaifa wa Tanganyika lilipokuwa limepamba moto Tanganyika,Omari Suleiman alikuwa na umri wa miaka 43.

Omar Suleiman alikuwa fundicherahani akifanya shughuli zake katika nyumba moja katikati ya mji wa Dodoma.Mkabala na nyumba ambamo Suleiman alikuwa amepanga chumba kimoja ilikuwa nyumbaaliyopanga Taratibu. Mara baada ya kupewa uhamisho kutoka Singida, Taratibualimuuliza jirani yake, Suleiman, kama kuliwepo na tawi la TANU pale mjini.Suleiman alimwambia Taratibu kuwa hapakuwepo na tawi la TANU mjini Dodoma naalimjulisha kuwa kulikuwa na tetesi mjini kuwa Hassan Suleiman amemuahidi nakumhakikishia DC kuwa yeye, akiwa katibu wa Jimbo wa TAA, hatairuhusu TANUkusajiliwa katika Jimbo la Kati bila ya idhini yake. Lakini ukweli ulikuwaHassan Suleiman akitokea katika uongozi wa TAA alikuwa tayari ameisajili TANU lakinihakumfahamisha mtu yoyote wala kufanya juhudi yoyote kuitisha uchaguzi aukufanya mkutano.

Hassan Suleiman kama, Omar Suleiman alikuwa na umri wa miakaarobaini na tatu mwaka 1955. Tofauti na Omari Suleiman, Hassan Suleimanialikuwa ameelimika na alikuwa mwanasiasa mwenye uzoefu akiwa amekiongoza chamacha African Association kuanzia miaka ya 1940 na alikuwa amehudhuria mikutanoya African Association Tanganyika na Zanzibar.
HarunaTaratibu, Omari Suleimani na marafiki zake wachache waliunda kamati ndogo kishawakaandika barua kwenda makao makuu ya TANU Dar es Salaam kuomba ruhusa yakufungua tawi la TANU. Katibu mwenezi wa TANU, wakati ule Oscar Kambona,aliwaandikia kuwaeleza kuwa Hassan Suleiman tayari alikuwa ameshaisajili TANUna ikiwa uchaguzi wa viongozi haujafanyika basi waonanena na yeye pamoja na AliPonda. Omari Suleiman na Haruna Taratibu hawakuridhika na majibu kutoka makaomakuu ya TANU kwa hiyo walikwenda kutafuta ushauri kwa Edward Mwangosi,aliyekuwa mwanachama mkongwe wa African Association. Mwangosi aliishauri kamatiile iitishe mkutano Community Centre ili kujadili ufunguzi wa tawi la TANU, naHassan Suleiman na Ali Ponda waalikwe kuhudhuria. Kadhalika Mwangosi aliishaurikamati ile kuwaalika walimu waliokuwa wakifundisha Kikuyu Secondary School,wengi wao wasomi kutoka Makerere kuhudhuria mkutano huo. Mwangosi aliwaambia wajumbe wa kamati ilendogo kuwa wasomi wa Makerere walikuwa ni muhimu sana kwenye chama kwa kuwawangetoa uongozi uliokuwa unatakiwa.Karibu ya watuarobaini pamoja na wale wasomi wa Makerere, miongoni mwao Job Lusindewalihudhuria mkutano ule. (Lusinde alikuja kuwa waziri, na Amon Nsekela,alikuja kushika nyadhifa muhimu katika serikali na vilevile kuwa balozi waTanzania nchini Uingereza).

Hassan Suleiman na Ali Ponda hawakutokea mkutanoni.Wakati wanakusanyika kwa ajili ya mkutano, afisa wa Community Centre aliwaambiakuwa alikuwa amepokea amri kutoka kwa DC kuwa mkutano huo usifanyike. Kufuatiaamri ile watu walitawanyika mara moja. Alexander Kanyamara aliyekuwa Mwafrikatajiri mjini Dodoma na rafiki wa John Rupia, wakati ule makamu wa rais wa TANU,aliwataka kuahirisha mkutano huo kwa sababu ya kutokuwepo kwa viongozi wa juuwa TAA, Hassan Suleiman na Ali Ponda. Kutokana na sababu hii na vile vitisho vya DC, mkutano uliahirishwa bilakupanga tarehe ya mkutano mwingine. Asubuhi iliyofuata Taratibu alikamatwa napolisi na kupelekwa kwenye ofisi ya DC, (hivi sasa ofisi hiyo ni ofisi yaWaziri Mkuu). Taratibu alimkuta Hassan Suleiman pale ofisini akizungumza na DC,Bwana Smith. DC alianza kumsaili Taratibu kwa kumuuliza kama alikuwa akijuakuzungumza Kiingereza. Taratibu alijibu kuwa yeye hakusoma. AkizungumzaKiingereza Hassan Suleiman alimwambia DC kuwa yeye ndiye katibu wa TANU mjini Dodoma.DC, Bwana Smith, alimshutumu Taratibu kwa kuunda chama haramu na kwa kuitishamkutano usio na idhini ya serikali katika Community Centre jana yake ambaoulielekea kuvuruga amani.

Bila woga Taratibu alijibu kwamba yeye alikuwa namamlaka ya kuitisha mkutano kwa sababu alikuwa mwanachama wa chama cha siasakilichosajiliwa kihalali. Taratibu aliichomoa kadi yake ya TANU kutoka mfukonikwake yenye rangi nyeusi na kijani na kumwonyesha DC. Bwana Smith alimuulizaHassan Suleiman kama ikiwa na yeye pia alikuwa na kadi ya TANU. Hassan Suleimanhakuwa nayo. Hassan Suleiman na DC walizungumza Kiingereza kwa muda baada yahapo aliwataka wote wawili kuandika maelezo yao. Baada ya kuandika maelezo yakeTaratibu aliruhusiwa kurudi nyumbani. Inasadikiwa kuwa wakati ule mwanachamapekee wa TANU mjini Dodoma walikuwa Haruna Taratibu na Alexander Kanyamaraambae yeye alikata kadi yake Dar esSalaam.
Wasomi waMakerere, ambao Mwangosi aliwaamini sana katika kuunda TANU, walipopata habarikuhusu mkasa wa Taratibu na DC, Bwana Smith, waliogopa. Waliamua kujiweka mbalikabisa na TANU na mambo ya siasa nakuendelea na kazi yao ya kufundisha. Haruna Taratibu na Omari Suleiman sasawaliamua kugeuza mbinu, waliitisha mkutano wa siri usiku nyumbani kwa Swedi binAthumani.

Mkutano huu uliamua kuwa Taratibu lazima aende makao makuu ya TANUDar es Salaam akazungumze na Nyerere ana kwa ana kuhusu matatizo yaliyokuwayakiikabili TANU Dodoma. Mahdi Mwinchumualiyekuwa mwanachama wa TANU Dar es Salaam alijitolea kufuatana na Taratibu hadimakao makuu ya chama Dar es Salaam kwa kuwa alikuwa akijuana na viongozi waTANU. Said Mussa mjumbe mwingine wa ile kamati ya siri alijitolea vilevilekufuatana na Taratibu na Mwinchumu hadi Dar es Salaam. Siku ya kuondoka JobLusinde alikwenda stesheni ya gari moshi kuagana na ule ujumbe uliokuwaukielekea Dar es Salaam, makao makuu ya TANU. Lusinde aliuambia ule ujumbe kuwajamaa wa Makerere wanaunga mkono maamuzi yote yatakayoamuliwa na ile kamati yasiri.
Kwa bahatinzuri katika gari moshi lile lile ambamo Taratibu na wenzake walikuwawakisafiri kulikuwa na wajumbe wa TANU kutoka Kigoma, Bukoba na Mwanzawakisafiri kwenda Dar es Salaam kuhudhuria mkutano mkuu wa kwanza wa mwaka waTANU. Wahudumu ndani ya gari moshi walipofahamu kuwa walikuwa na wajumbe waTANU kwenye gari moshi lile, waliwafanyia heshima kubwa. Mmoja wa wahudumu walealijitolea kumpa malazi Salum Mussa nyumbani kwake Dar es Salaam. MahdiMwinchumu aliwapeleka Haruna Taratibu na Said Mussa makao makuu ya TANU NewStreet ambako walifanya mazungumzo na Nyerere pamoja na Rupia.

Uongozi wa makaomakuu ulielezwa kwa ufupi matatizo yaliyokuwa yakikabili Dodoma katika kufunguatawi la TANU. Papo hapo Nyerere alimwalika Taratibu kuhudhuria mkutano mkuuHindu Mandal Hall kama mjumbe wa Jimbo la Kati. Mkutano ule ulimchagua Taratibu kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa yaTANU. Taratibu na ujumbe wake walirudiDodoma washindi, walikwenda Dar es Salaam watu wasiojulikana na walirudinyumbani wakifuatana na mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa wa TANU, chombo cha juukabisa katika chama. Nyerere alimpa Taratibu dafari ya tasjili ya wanachama,kadi mia moja hamsini za uanachama wa TANU na nakala hamsini za "Billof Rights." Kazi ya kuwahamasisha na kuwaingiza watu TANU alipewa OmariSuleiman, na fundi cherahani mwingine aliyejulikana kwa jina la Abdu MohamedMkamba. Mara tu baba mwenye nyumba wake alipopata habari za kuwa mpangaji wake,Haruna Taratibu alikuwa mwanachama wa TANU, alimfukuza kutoka kwenye nyumbayake.
Baada ya kupatakikundi kidogo cha wanachama, Taratibu alipiga simu makao makuu ya TANU nakuzungumza na kaimu katibu, Elias Kissenge akaomba ruhusa ya kufanya uchaguzi.Kissenge hakuweza kutoa uamuzi wowote wa maana kuhusu tatizo la uongozi wa TANUDodoma. Taratibu alifanikiwa kumpata Kambona ambae aliidhinisha uchaguziufanyike kwa shuruti moja la kuwa Hassan Suleiman na Ali Ponda waruhusiwekushiriki na kugombea uongozi wa chama.

Kusisitiza kwa Kambona juu ya uongoziwa zamani wa TAA kuongoza chama kipya huenda kulishawishiwa na mafanikio yazamani ya uongozi wa Hassan Suleiman mbae alimfahamu huko Dodoma wakati Kambonaalipokuwa mwalimu akifundisha KikuyuSecondary School. Kwa bahati mbaya, wanachama wa TANU waliokuwa wanainukia nachama pale mjini Dodoma waliwaona Hassan Suleiman na Ali Ponda kama wasalitikutokana na kutokushirikiana na wenzao katika kuanzisha TANU.
Wakatiametatizwa na tatizo la uchaguzi wa TANU, Taratibu alijulishwa na makao makuukuwa makamo wa rais, John Rupia, atapita Dodoma kwa gari moshi akiwa njianikwenda Tabora kushughulikia mambo ya chama. Gari moshi liliposimama DodomaRupia alishangazwa kuona kundi la wananchama wa TANU wakimsubiri katika kituocha gari moshi wakimtaka avunje safari waende mjini kujadili na kutatua tatizola uchaguzi. Rupia aliwaeleza wanachama wa TANU wa Dodoma kuwa yeye hakuwa na idhini kutoka makao makuukufanya shughuli yoyote ya chama mjini Dodoma. Wanachama wa TANU hawakutakakusikia lolote na walimwambia Rupia kuwa wamechoshwa na makao makuu kwakushindwa kwake kutoa uamuzi wa tatizo la uchaguzi. Mizigo ya Rupia ilishushwachini kutoka kwenye gari moshi na Rupia akawa hana khiyari isipokuwa kuwafuatawale wanachama wa TANU hadi mjini.Ghafla mjimzima ukavuma tetesi kuwa makamu wa rais wa TANU, John Rupia, yupo mjinikufungua tawi la TANU.

Rupia alimwita Hassan Suleimna na akamtaka alete hati yatasjili ya TANU Hindu Mandal siku inayofuata, mahali ambako mkutano utafanyika.Hassan Suleiman hakutokea mkutanoni lakini alimtuma mtu apeleke ile hati. AliPonda alihudhuria mkutano ule. Rupia alikuwa mwenyekiti wa mkutano na TANUikafanya uchaguzi wake wa kwanza. Alexander Kanyamara alichaguliwa Rais; Haruna Taratibu Makamu wa Rais,Abdu Mohamed Mwamba, Katibu na Omari Suleiman Mweka Hazina. Miongoni mwawanachama waasisi alikuwa mwanamke mmoja wa Kimanyema, Binti Maftah Karenga;wengine walikuwa Bakari Yenga, Maalim Khalfan, mwanachuoni wa Kiislamualiyekuwa akiheshimiwa sana pale mjini, Idd Waziri na Said Suleiman. Walewasomi wa Makerere hata mmoja hakujitokeza kwenye mkutano huu wakuasisi TANU. Ali Ponda, mwanasiasa mkongwe alipuuzwa na hakuchaguliwa kushikawadhifa wowote. Walipoona hawakupewa wadhifa wowote katika TANU, Ali Ponda naHassan Suleiman walijiunga na UTP kuipinga TANU.
Baada yauchaguzi huo, wale mafundi cherahani wawili, Abdu Mohamed Mkamba na OmariSuleiman, walianza kuhamasisha wananchi waziwazi kujiunga na TANU ili wapiganieuhuru wa Tanganyika. Tawi la TANU la Dodoma baada ya kujizatiti pale mjini,lilituma wanaharakati kuwahamasisha watu wa Kondoa ili wafungue tawi la TANUkatika wilaya hiyo. Abdallah Jumbe alizipenyeza kadi za TANU na kuzipelekakwenye wilaya hiyo kwa siri akaanza kuandikisha watu. D.C. wa Singida alikuwajeuri sana kiasi kwamba ni baada ya Mkutano Mkuu wa Tabora wa mwaka 1958 ndipoAbdallah Jumbe aliweza kufanikiwa kufungua tawi mjini Singida. Wakati huo TANUilikuwa na nguvu sana ikiwa na wajumbe wake katka Baraza la Kutunga Sheria.

Kwaajili hii hakuna Mzungu aliyethubutu kuwa fedhuli kwa TANU na kuwabughudhiwanachama wake.
Hii kwamuhtasari ndiyo historia ya marehemu Omar Suleiman na wenzake waliopiganiauhuru wa Tanganyika historia ambayo si wengi wanaifahamu na kwa ajili hii ikawaimepotea hata historia ya wazalendo wengine aliokuwanao baga kwa bega katikakuitafutia Tanganyika heshima yake.

Mungu ailaze roho ya Mzee Omar Suleimanmahali pema peponi.

12 Februari 2012
 
asante mkuu....!inawezekana kabisa kuna dosari katika namna ya uhifadhi wa kumbukumbu mkuu....!hasa katika historia za mashujaa...

ila sasa ondoa dhana ya udini hapo.....!
 
MzeeOmar Suleiman (1910 - 2012) Mwasisi wa TANU Dodoma

MohamedSaid
Katika moja yamisiba mikubwa ya Tanzania ni kukosekana kuwapo kwa historia ya kweli yakupigania uhuru na kwa ajili hiyo kusababisha kutokuwapo kwa mashujaa wa taifa.Mzee Omar Suleiman ni mmoja wa waasisi wa TANU Dodoma na kwa ajili hii ni katiya mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika ambao si wengi wanamfahamu nakujua khasa nini ulikuwa mchango wake. Mara kwa mara hasa kwa siku hisi zamwisho wa maisha yake kila ilipotokea nafasi ya kutaja Mzee Omar Suleimankilichokuwa kikielezwa ni uhusiano wake na Julius Nyerere na kusema kuwaNyerere alikuwa akifikia nyumbani kwake basi. Nini ulikuwa mchango wake haukuwauanelezwa na sababu khasa ni kuwa hakuna aliyekuwa anaujua. Hata alipokufahakuna taazia yoyote iliyosmdikwa kumweleza Omar Suleiman alikuwa nani. Ili kumjuaOmar Suleiman ni lazima mtu arudi nyuma sana na kumtafuta Omar Suleima katikakundi la wazalendo wenzake aliokuwanao katika siasa wakati wa kuiunda TANUJimbo la Kati mwaka wa 1955.Kuipata pichaya siasa katika Tanganyika ya 1950 hatuna budi uitazama African Associationmtangulizi wa TANU. African Association mjini Dodoma ilikuwa ikiongoza katikaharakati baada ya Vita Kuu ya Pili. Ilikuwa na wanasiasa wenye juhudi sana nawabunifu kuliko wanasiasa wengine wote waliopata kutokea katika historia yaTanganyika. Wanasiasa hawa walikuwa Ali Ponda, Mmanyema na Hassan Suleiman,Myao, rais na katibu wake. Mwaka 1945 Ali Ponda alitoa wito kwa Waafrika wotekuungana kama umma mmoja. Lakini kuanzia mwaka 1948 harakati za siasa mjiniDodoma zilififia, na TANU ilipoanzishwa mnamo Julai, 1954, tawi la TAA Dodomalilikuwa limedorora kiasi kwamba kilishindwa hata kupeleka mjumbe kwenyemkutano ule wa TAA wa kuundwa kwa TANU. Pamoja na ukweli kuwa mji wa Dodomakulikuwa na Kikuyu Secondary School (sasa Alliance Secondary School) ambakokulikuwa na walimu wa Kiafrika, wengi wao kutoka Makerere, ambao kama wasomi,wangechukua juhudi kuihuisha African Association. Labda kwa kuhisi kuwahapakuwapo na ukinzani unaokwenda kinyume na maslahi yao katika mfumo wa kikoloni, walimu wale waliamua kujitenga nasiasa. Kwa hiyo basi, harakati dhidi ya serikali ya kikoloni ziliachwa kuwa mikononimwa wa Waislam wa mjini Dodoma, wengi wao wakiwa hawakujaliwa kupata elimu kaajili ya siasa za Waingereza walioacha elimu iwe mikononi mwa Wamishionari. Historia yaMzee Omar Suleiman haiwezi kukamilika bila ya kumtaja rafiki yake shujaa wauhuru marehemu Haruna Taratibu. Mwaka wa 1953 Haruna alikuwa na umri wa miaka 23 na akifanya kazi Public Works Department (PWD) kamamwashi. Haruna Taratib alijaribu kuunda chama cha wafanyakazi kwa kuwahamasishana kuwakusanya vibarua walioajiriwa katika kazi za ujenzi. Kwa sababu yaharakati hizo za kutaka kuanzisha chama cha wafanyakazi, Taratibu alionekana nawakoloni kama mtu mkorofi na mzusha vurugu. Hata hivyo Taratibu hakufanikiwakuanzisha chama hicho na matokeo yake akapewa uhamisho kwenda Singida kamaadhabu. Taratibu alivutiwa sana na harakati za Mau Mau nchini Kenya na alizoeakufuatilia matukio yake katika gazeti lake alilokuwa akilipenda sana, "Baraza,"gazeti la Kiswahili la kila wiki kutoka Kenya.Ilikuwa katikaNovemba 1954 wakati Taratibu alipokuwa akipekuapekua gazeti hilo ndipo alioposomahabari kuhusu TANU. Taratibu aliuliza pale Singida mjini kama kuna tawi laTANU. Taratibu alifahamishwa kukuwepo kwa tawi la TANU pale mjini na katibu wake alikuwa mzee mmojakwa jina la Mzee Kinyozi. Taratibu alikata kadi yake toka kwa huyo mzee naakawa mwanachama wa chama cha siasa. Asubuhi iliyofuata Taratibu aliingiaofisini kwake na akaiweka kadi yakeya uanachama wa TANU yenye rangi nyeusi na kijani juu ya meza yake, kilamtu aione. Ofisa Mzungu wa PWD Singida hakuweza kuvumila ufedhuli kama ule,alishauri Taratibu apewe uhamisho kurudi Dodoma alikotoka, kabla hajaeneza sumu yake kwa Waafrika wengine. Hapo ndipoalipokuja kuungana na Mzee Omar Suleiman.Mwaka 1955wakati wimbi la utaifa wa Tanganyika lilipokuwa limepamba moto Tanganyika,Omari Suleiman alikuwa na umri wa miaka 43. Omar Suleiman alikuwa fundicherahani akifanya shughuli zake katika nyumba moja katikati ya mji wa Dodoma.Mkabala na nyumba ambamo Suleiman alikuwa amepanga chumba kimoja ilikuwa nyumbaaliyopanga Taratibu. Mara baada ya kupewa uhamisho kutoka Singida, Taratibualimuuliza jirani yake, Suleiman, kama kuliwepo na tawi la TANU pale mjini.Suleiman alimwambia Taratibu kuwa hapakuwepo na tawi la TANU mjini Dodoma naalimjulisha kuwa kulikuwa na tetesi mjini kuwa Hassan Suleiman amemuahidi nakumhakikishia DC kuwa yeye, akiwa katibu wa Jimbo wa TAA, hatairuhusu TANUkusajiliwa katika Jimbo la Kati bila ya idhini yake. Lakini ukweli ulikuwaHassan Suleiman akitokea katika uongozi wa TAA alikuwa tayari ameisajili TANU lakinihakumfahamisha mtu yoyote wala kufanya juhudi yoyote kuitisha uchaguzi aukufanya mkutano. Hassan Suleiman kama, Omar Suleiman alikuwa na umri wa miakaarobaini na tatu mwaka 1955. Tofauti na Omari Suleiman, Hassan Suleimanialikuwa ameelimika na alikuwa mwanasiasa mwenye uzoefu akiwa amekiongoza chamacha African Association kuanzia miaka ya 1940 na alikuwa amehudhuria mikutanoya African Association Tanganyika na Zanzibar. HarunaTaratibu, Omari Suleimani na marafiki zake wachache waliunda kamati ndogo kishawakaandika barua kwenda makao makuu ya TANU Dar es Salaam kuomba ruhusa yakufungua tawi la TANU. Katibu mwenezi wa TANU, wakati ule Oscar Kambona,aliwaandikia kuwaeleza kuwa Hassan Suleiman tayari alikuwa ameshaisajili TANUna ikiwa uchaguzi wa viongozi haujafanyika basi waonanena na yeye pamoja na AliPonda. Omari Suleiman na Haruna Taratibu hawakuridhika na majibu kutoka makaomakuu ya TANU kwa hiyo walikwenda kutafuta ushauri kwa Edward Mwangosi,aliyekuwa mwanachama mkongwe wa African Association. Mwangosi aliishauri kamatiile iitishe mkutano Community Centre ili kujadili ufunguzi wa tawi la TANU, naHassan Suleiman na Ali Ponda waalikwe kuhudhuria. Kadhalika Mwangosi aliishaurikamati ile kuwaalika walimu waliokuwa wakifundisha Kikuyu Secondary School,wengi wao wasomi kutoka Makerere kuhudhuria mkutano huo. Mwangosi aliwaambia wajumbe wa kamati ilendogo kuwa wasomi wa Makerere walikuwa ni muhimu sana kwenye chama kwa kuwawangetoa uongozi uliokuwa unatakiwa.Karibu ya watuarobaini pamoja na wale wasomi wa Makerere, miongoni mwao Job Lusindewalihudhuria mkutano ule. (Lusinde alikuja kuwa waziri, na Amon Nsekela,alikuja kushika nyadhifa muhimu katika serikali na vilevile kuwa balozi waTanzania nchini Uingereza). Hassan Suleiman na Ali Ponda hawakutokea mkutanoni.Wakati wanakusanyika kwa ajili ya mkutano, afisa wa Community Centre aliwaambiakuwa alikuwa amepokea amri kutoka kwa DC kuwa mkutano huo usifanyike. Kufuatiaamri ile watu walitawanyika mara moja. Alexander Kanyamara aliyekuwa Mwafrikatajiri mjini Dodoma na rafiki wa John Rupia, wakati ule makamu wa rais wa TANU,aliwataka kuahirisha mkutano huo kwa sababu ya kutokuwepo kwa viongozi wa juuwa TAA, Hassan Suleiman na Ali Ponda. Kutokana na sababu hii na vile vitisho vya DC, mkutano uliahirishwa bilakupanga tarehe ya mkutano mwingine. Asubuhi iliyofuata Taratibu alikamatwa napolisi na kupelekwa kwenye ofisi ya DC, (hivi sasa ofisi hiyo ni ofisi yaWaziri Mkuu). Taratibu alimkuta Hassan Suleiman pale ofisini akizungumza na DC,Bwana Smith. DC alianza kumsaili Taratibu kwa kumuuliza kama alikuwa akijuakuzungumza Kiingereza. Taratibu alijibu kuwa yeye hakusoma. AkizungumzaKiingereza Hassan Suleiman alimwambia DC kuwa yeye ndiye katibu wa TANU mjini Dodoma.DC, Bwana Smith, alimshutumu Taratibu kwa kuunda chama haramu na kwa kuitishamkutano usio na idhini ya serikali katika Community Centre jana yake ambaoulielekea kuvuruga amani. Bila woga Taratibu alijibu kwamba yeye alikuwa namamlaka ya kuitisha mkutano kwa sababu alikuwa mwanachama wa chama cha siasakilichosajiliwa kihalali. Taratibu aliichomoa kadi yake ya TANU kutoka mfukonikwake yenye rangi nyeusi na kijani na kumwonyesha DC. Bwana Smith alimuulizaHassan Suleiman kama ikiwa na yeye pia alikuwa na kadi ya TANU. Hassan Suleimanhakuwa nayo. Hassan Suleiman na DC walizungumza Kiingereza kwa muda baada yahapo aliwataka wote wawili kuandika maelezo yao. Baada ya kuandika maelezo yakeTaratibu aliruhusiwa kurudi nyumbani. Inasadikiwa kuwa wakati ule mwanachamapekee wa TANU mjini Dodoma walikuwa Haruna Taratibu na Alexander Kanyamaraambae yeye alikata kadi yake Dar esSalaam.Wasomi waMakerere, ambao Mwangosi aliwaamini sana katika kuunda TANU, walipopata habarikuhusu mkasa wa Taratibu na DC, Bwana Smith, waliogopa. Waliamua kujiweka mbalikabisa na TANU na mambo ya siasa nakuendelea na kazi yao ya kufundisha. Haruna Taratibu na Omari Suleiman sasawaliamua kugeuza mbinu, waliitisha mkutano wa siri usiku nyumbani kwa Swedi binAthumani. Mkutano huu uliamua kuwa Taratibu lazima aende makao makuu ya TANUDar es Salaam akazungumze na Nyerere ana kwa ana kuhusu matatizo yaliyokuwayakiikabili TANU Dodoma. Mahdi Mwinchumualiyekuwa mwanachama wa TANU Dar es Salaam alijitolea kufuatana na Taratibu hadimakao makuu ya chama Dar es Salaam kwa kuwa alikuwa akijuana na viongozi waTANU. Said Mussa mjumbe mwingine wa ile kamati ya siri alijitolea vilevilekufuatana na Taratibu na Mwinchumu hadi Dar es Salaam. Siku ya kuondoka JobLusinde alikwenda stesheni ya gari moshi kuagana na ule ujumbe uliokuwaukielekea Dar es Salaam, makao makuu ya TANU. Lusinde aliuambia ule ujumbe kuwajamaa wa Makerere wanaunga mkono maamuzi yote yatakayoamuliwa na ile kamati yasiri.Kwa bahatinzuri katika gari moshi lile lile ambamo Taratibu na wenzake walikuwawakisafiri kulikuwa na wajumbe wa TANU kutoka Kigoma, Bukoba na Mwanzawakisafiri kwenda Dar es Salaam kuhudhuria mkutano mkuu wa kwanza wa mwaka waTANU. Wahudumu ndani ya gari moshi walipofahamu kuwa walikuwa na wajumbe waTANU kwenye gari moshi lile, waliwafanyia heshima kubwa. Mmoja wa wahudumu walealijitolea kumpa malazi Salum Mussa nyumbani kwake Dar es Salaam. MahdiMwinchumu aliwapeleka Haruna Taratibu na Said Mussa makao makuu ya TANU NewStreet ambako walifanya mazungumzo na Nyerere pamoja na Rupia. Uongozi wa makaomakuu ulielezwa kwa ufupi matatizo yaliyokuwa yakikabili Dodoma katika kufunguatawi la TANU. Papo hapo Nyerere alimwalika Taratibu kuhudhuria mkutano mkuuHindu Mandal Hall kama mjumbe wa Jimbo la Kati. Mkutano ule ulimchagua Taratibu kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa yaTANU. Taratibu na ujumbe wake walirudiDodoma washindi, walikwenda Dar es Salaam watu wasiojulikana na walirudinyumbani wakifuatana na mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa wa TANU, chombo cha juukabisa katika chama. Nyerere alimpa Taratibu dafari ya tasjili ya wanachama,kadi mia moja hamsini za uanachama wa TANU na nakala hamsini za "Billof Rights." Kazi ya kuwahamasisha na kuwaingiza watu TANU alipewa OmariSuleiman, na fundi cherahani mwingine aliyejulikana kwa jina la Abdu MohamedMkamba. Mara tu baba mwenye nyumba wake alipopata habari za kuwa mpangaji wake,Haruna Taratibu alikuwa mwanachama wa TANU, alimfukuza kutoka kwenye nyumbayake.Baada ya kupatakikundi kidogo cha wanachama, Taratibu alipiga simu makao makuu ya TANU nakuzungumza na kaimu katibu, Elias Kissenge akaomba ruhusa ya kufanya uchaguzi.Kissenge hakuweza kutoa uamuzi wowote wa maana kuhusu tatizo la uongozi wa TANUDodoma. Taratibu alifanikiwa kumpata Kambona ambae aliidhinisha uchaguziufanyike kwa shuruti moja la kuwa Hassan Suleiman na Ali Ponda waruhusiwekushiriki na kugombea uongozi wa chama. Kusisitiza kwa Kambona juu ya uongoziwa zamani wa TAA kuongoza chama kipya huenda kulishawishiwa na mafanikio yazamani ya uongozi wa Hassan Suleiman mbae alimfahamu huko Dodoma wakati Kambonaalipokuwa mwalimu akifundisha KikuyuSecondary School. Kwa bahati mbaya, wanachama wa TANU waliokuwa wanainukia nachama pale mjini Dodoma waliwaona Hassan Suleiman na Ali Ponda kama wasalitikutokana na kutokushirikiana na wenzao katika kuanzisha TANU. Wakatiametatizwa na tatizo la uchaguzi wa TANU, Taratibu alijulishwa na makao makuukuwa makamo wa rais, John Rupia, atapita Dodoma kwa gari moshi akiwa njianikwenda Tabora kushughulikia mambo ya chama. Gari moshi liliposimama DodomaRupia alishangazwa kuona kundi la wananchama wa TANU wakimsubiri katika kituocha gari moshi wakimtaka avunje safari waende mjini kujadili na kutatua tatizola uchaguzi. Rupia aliwaeleza wanachama wa TANU wa Dodoma kuwa yeye hakuwa na idhini kutoka makao makuukufanya shughuli yoyote ya chama mjini Dodoma. Wanachama wa TANU hawakutakakusikia lolote na walimwambia Rupia kuwa wamechoshwa na makao makuu kwakushindwa kwake kutoa uamuzi wa tatizo la uchaguzi. Mizigo ya Rupia ilishushwachini kutoka kwenye gari moshi na Rupia akawa hana khiyari isipokuwa kuwafuatawale wanachama wa TANU hadi mjini.Ghafla mjimzima ukavuma tetesi kuwa makamu wa rais wa TANU, John Rupia, yupo mjinikufungua tawi la TANU. Rupia alimwita Hassan Suleimna na akamtaka alete hati yatasjili ya TANU Hindu Mandal siku inayofuata, mahali ambako mkutano utafanyika.Hassan Suleiman hakutokea mkutanoni lakini alimtuma mtu apeleke ile hati. AliPonda alihudhuria mkutano ule. Rupia alikuwa mwenyekiti wa mkutano na TANUikafanya uchaguzi wake wa kwanza. Alexander Kanyamara alichaguliwa Rais; Haruna Taratibu Makamu wa Rais,Abdu Mohamed Mwamba, Katibu na Omari Suleiman Mweka Hazina. Miongoni mwawanachama waasisi alikuwa mwanamke mmoja wa Kimanyema, Binti Maftah Karenga;wengine walikuwa Bakari Yenga, Maalim Khalfan, mwanachuoni wa Kiislamualiyekuwa akiheshimiwa sana pale mjini, Idd Waziri na Said Suleiman. Walewasomi wa Makerere hata mmoja hakujitokeza kwenye mkutano huu wakuasisi TANU. Ali Ponda, mwanasiasa mkongwe alipuuzwa na hakuchaguliwa kushikawadhifa wowote. Walipoona hawakupewa wadhifa wowote katika TANU, Ali Ponda naHassan Suleiman walijiunga na UTP kuipinga TANU.Baada yauchaguzi huo, wale mafundi cherahani wawili, Abdu Mohamed Mkamba na OmariSuleiman, walianza kuhamasisha wananchi waziwazi kujiunga na TANU ili wapiganieuhuru wa Tanganyika. Tawi la TANU la Dodoma baada ya kujizatiti pale mjini,lilituma wanaharakati kuwahamasisha watu wa Kondoa ili wafungue tawi la TANUkatika wilaya hiyo. Abdallah Jumbe alizipenyeza kadi za TANU na kuzipelekakwenye wilaya hiyo kwa siri akaanza kuandikisha watu. D.C. wa Singida alikuwajeuri sana kiasi kwamba ni baada ya Mkutano Mkuu wa Tabora wa mwaka 1958 ndipo Abdallah Jumbe aliweza kufanikiwa kufungua tawi mjini Singida. Wakati huo TANUilikuwa na nguvu sana ikiwa na wajumbe wake katka Baraza la Kutunga Sheria. Kwaajili hii hakuna Mzungu aliyethubutu kuwa fedhuli kwa TANU na kuwabughudhiwanachama wake.Hii kwamuhtasari ndiyo historia ya marehemu Omar Suleiman na wenzake waliopiganiauhuru wa Tanganyika historia ambayo si wengi wanaifahamu na kwa ajili hii ikawaimepotea hata historia ya wazalendo wengine aliokuwanao baga kwa bega katikakuitafutia Tanganyika heshima yake. Mungu ailaze roho ya Mzee Omar Suleiman mahali pema peponi.

12 Februari 2012

Kwenye hadithi yako nimehesabu mashujaa 17! Loh, sikujua TZ tuna utajiri wa ''mashujaa'' wengi kiasi hiki. RIP Mzee Suleiman
 
Karibu tena, Mohamed Said!
Tupo...
Tuendelee na darsa lako...
 
Assalamu alaikum mzee Said naomba unisaidie speech ya Nyerere ya mwaka 1985 aliyokua anawaaga wazee wa Dar es salaam.
 
Ahsante M.Said kwa kutupa historia ya Babu yetu Marehemu Omar Suleiman
je waweza tupa pia na historia ya Bint Waziri huyu pia nyumba yake ilitumika kama kituo cha mikutano ya TANU kabla ya uhuru na inasemekana ndii nyuma aliyikuwa akigikia Hayati Mwl. Nyerere alipokuwa akija Dodoma nazamani palikiwa na kibao kikieleza hayo.
 
Back
Top Bottom