Elli
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 55,470
- 85,946
Juzi kwenye mazishi ya marehemu Mzee James Irenge ambaye alikuwa mwalimu wa baba wa taifa Julias Kambarage Nyerere katika shule ya Msingi Mwisenge ambaye alifariki akiwa na umri zaidi ya miaka 120 niliona na kusikia kitu cha aibu sana, ushuhuda wa ajabu, huu ulitamkwa na kiongozi wa familia hio ambaye niliskia kwa maskio na macho yangu kuuona anchokisema kuwa hadi Mzee Irenge anafariki dunia bado alikua akiidai serikali mafao yake ya Ualimu ikiwamo nauli ya kusafirishiwa mizigo yake.
Hili lilizungumzwa mbele ya kiongozi wa kitaifa na tangu juzi nimekua nikifuatilia kuona labda kutakua na hatua yoyote itakayokuwa imechukuliwa na viongozi wa kitaifa lakini suala hili limekuwa kimya na hakuna alieoneka kujiguswa na statement ile. hali ile niliitafsiri kuwa ni aibu kubwa kwa taifa ambalo limekuwa likijivunia kutunza watu exceptional kama hawa!!!
Wasi wasi wangu ni kuwa; kama hili limefanyika kwa mtu kama huyu, vipi hal;i ya walimu hawa wa "kawaida" wasio na title yoyote? Ni lini kazi na utu wetu vitaheshimiwa? Source ya Taarifa Hii ilikua ni ITV taarifa ya habari