Marehemu maandamano ya Chadema Mkenya

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MMOJA kati ya watu watatu waliokufa kutokana na majeraha kwenye maandamano ya Chadema jijini hapa juzi ni raia wa Kenya.

Paul Njuguna Kayehe, mwenye kitambulisho cha uraia namba 25066938, alifariki dunia jana katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru alikokuwa amelazwa.

Taarifa za kifo cha Mkenya huyo ambaye haijulikani aliingia vipi kwenye maandamano hayo, yaliyogubikwa na ghasia zilizotokana na Polisi kuyazuia, zilitolewa jana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Dk Salesh Toure.

Kifo hicho, kinafanya waliopoteza maisha kutokana na maandamano hayo yaliyofanyika Januari 5 kuwa watatu.

Hata hivyo, Dk Toure hakutoa ufafanuzi zaidi bali alisema majeruhi wengine bado wamelazwa ingawa hali zao si nzuri sana.

Kwa mujibu wa Dk Toure, wengine waliokufa siku ya tukio kutokana na majeraha ya risasi ni Dennis Michael mkazi wa Sakina na George Mwita.

Wakati huo huo, Umoja wa Wakristo Mkoa wa Arusha, umesema haumtambui Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo, kwa madai kuwa hakuchaguliwa kihalali na hivyo kusema amri za Mungu zilikiukwa.

Akitoa taarifa ya Umoja huo jana, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Arusha, Joseph Lobulu, alisema kutokana na hali hiyo, hawatampa ushirikiano wowote katika shughuli za maendeleo mkoani hapa.

Pia waliiomba Serikali kuingilia kati mkanganyiko huo wa uchaguzi ili kuepusha damu kumwagika na walimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, kwa dhamira yake ya kutaka kuwapatanisha CCM na Chadema kwa amani na upendo.

Umoja huo pia ulieleza kusikitishwa kwake na jinsi Polisi ilivyotumia nguvu nyingi kukabiliana na waandamanaji wa Chadema ambapo Askofu Lobulu katika taarifa hiyo, alisema walitumia nguvu kubwa ‘kuua nzi’.

“Hatutakuwa tayari kuona nguvu hizi kubwa zikitumika tena mkoani Arusha,” alisema Askofu huyo katika taarifa hiyo.
 
Back
Top Bottom