Marco Chali: Wimbo wa 'Freedom' sio wa Mr. Blue

kedrick

JF-Expert Member
Apr 25, 2015
5,059
4,866
Mr Blue analalamika kuwa Sugu ameupora wimbo wake ‘Freedom’ aliokuwa amemshirikisha kwa kutoa verse zake na kuufanyia video iliyotoka jana.

Lakini katika kila malalamiko, ni vyema kusikiliza pande zote zinazohusika kwenye jambo husika ili kuupata ukweli. MJ Records walioutayarisha wimbo huo wamezungumza kuelezea mambo yalikuwaje.

Producer mkuu wa studio hiyo, Marco Chali ameiambia Bongo5 kuwa beat ya wimbo huo ilitengenezwa na mdogo wake, Daxo Chali aliyetengeneza chorus yake na alimpa msanii wake Lizzy aliyeingiza. “Ngoma ilikuwa ipo tayari na ilikuwa inasubiria verse tu kadhaa halafu ilikuwa ni ngoma yake [Daxo]. Kwahiyo jamaa [Blue] akawa ameipenda tukampa akasema atamshirikisha Mr Two,” amesema Marco.

Walipoifanya, Blue aliiamua kuiachia kupitia Mkito peke yake kwa maana kwamba hakuiachia ngoma rasmi. Anasema baada ya muda Sugu alimpigia simu kumuomba kuwa afanye version nyingine ya wimbo huo na aifanyie kabisa na video.

Anadai alimuambia Sugu aongee na Daxo waliyekubali kuufanya tena hadi video ikafanyika huku yeye [Marco] akiwa hajui chochote kilichoendelea baada ya hapo. Na Marco anasema pia hakuhusika kwenye uingizaji wa sauti zote mbili zaidi ya kuzifanyia mixing peke yake.

Marco amesema anadhani wawili hao [Sugu na Blue] waliongea kuhusu hatua hiyo na kwamba wao kama studio hawakuwa na kipingamizi chochote kuhusu kurudiwa kwa wimbo huo kwasababu walitaka wimbo ufike mahali.

Hata hivyo Marco amedai kuwa wote wawili [Sugu na Blue] hawakulipia wimbo huo na kwamba MJ Records iliwapa kwasababu ya ‘love’ tu. Marco anasema anashangaa kuona Mr Blue sasa hivi anatoa malalamiko hayo. “Ni kwasababu mimi nilipenda tu kutoa studio bure kwanini usijitahidi ukapeleka hiyo nyimbo ikafika sehemu ikafahamika, at least pia akili za watu zilizotumika watu wazione. Na ndio hicho kitu naona ni kizuri, yeye kwa mfano angefanya hata video, sidhani kama Sugu angerudia huo wimbo,” ameongeza Marco.


8d2a24a9e35fc0b651e46a03a898a247.jpg

Maneno ya mwenywe wimbo halisi
 
Tatizo la blue ni kosa alilolifanya miaka mingi iliyopita kosa lenyewe ni KUACHA SHULE.....

na hili ni janga kwa wasanii wetu wengi...

shule shule shule...
elimu elimu elimu....

mwenzake sugu hata kama shule hajapita ni kuwa yuko karibu na kina tundu lissu, marando angalau sheria anazijua jua... na kukaa kaa bungeni nako kunasaidia

sasa mwenzangu na mie huyu anashinda na nyandu tozi na bob micharazo kuna anayejua sheria hapo??



b-o-b-micharazo.jpg
 
Kuna watu jasho liliwatoka kwenye ile post ya kumtuhumu Sugu kaiba wimbo nadhani kwenye post hi watakuwa wanabinua midomo kama watoto wa kike...Kweli elimu ni muhimu...amejisemea Blue mwenyewe Ukilala Unalaliwa nadhani kapata picha tayari
 
"Kwahiyo jamaa [Blue] akawa ameipenda tukampa
akasema atamshirikisha Mr Two"

Hapa Marco chali kajimaliza mwenyewe mmempa wimbo alafu leo mnasema sio wa kwake. Tunajua mmemgeuka sababu ya pesa ila Sugu ni mwizi na atabaki kuwa hivyo alafu anajifanya mtetezi wa haki za wasanii.
 
Tatizo la wasanii na baadhi ya vijana ni kukosa kuwa na vision kipindi wakiwa wanapesa,wanafanya matumizi na anasa za kila namna,bila kuwaza kuwa kuna kesho,huyu dogo alihit sana enzi zake,na amefanya show nyingi sana enzi zile,tatizo they dont invest or save,badala yake they buy liabilities kama magari ya gharama na wanawake,"Mr Blue maisha uliyonayo ni matokeo ya Decisions na Choices ulizofanya huko nyuma,so dont blame anybody hapa,you have to take 100% responsibility kwa yote yanayokutokea",komaa usichoke na bado una muda...
 
Huyu dogo chenga sana, tokea aanze kuropoka juu ya Diamond kujiita simba wakati mnyama mwenyewe katulia mwituni, Afande sele katulia, Malkia wa shauzi katulia nikamuona kama BOYA lililokosa muelekeo baharini..

Kwa alichoongea Marco chali basi Diamond hana umiliki wa robo tatu ya nyimbo zake. Kuanzia kamwambie mpaka ukimwona zote album mbili ni za producers Diamond hajalipa ata senti nyimbo zote hizo.
 
Watu watamtetea tu Sugu kwa sababu ni mheshimiwa... msanii anapewa ngoma anaifanyia kazi, then ngoma hiyohiyo anapewa mtu mwingine! Anafanya na video kabsa! Is this right kweli? Mi nadhani yuole aliyekuwa wa kwanza kupewa ndiyo mwenye ngoma yake, suala la promo linahusikaje? Posho bungeni ale, mshahara wa ubunge ale, mpaka ngoma za machalii nazo azibake? Wakale wapi sasa...
 
idea sio yake na beat sio yake I was on blue sside lakini haya maelezo ya daxo na Marco yanamanisha nyimbo ni Mali ya mj recs
Hayo ni maneno wanaweza kuongea lolote kuhalalisha uovu wao ila kama una akili zinakutosha utaelewa huo wimbo ni wa Mr blue.

Eti tukaona tumpe blue alafu huo wimbo sio wake ni wetu. Sasa kama mlimpa unabakije kuwa wa kwenu na unaendaje kuwa wa sugu...

Wimbo upo mkito. Com mr blue ft sugu.. Jiulize pesa huko mkito anachukua mj records au mr blue.
 
Unatuchanganyia mada mkuu! Tujadili kwanza hili la Blu, ukirefer mifano ya namna hiyo hatuwez kuelewana
Nimetoa mfano wa Diamond sababu kuna mademu wa Diamond walijaribu kuingiza beef lake na Dai kumkandamiza byser eti jina sijui nini. Na ni kweli kwa maelezo ya Marco chali album zote mbili za kwanza za Diamond sio zake moja ya Bob junior nyingine ya Maneke.
 
Nimetoa mfano wa Diamond sababu kuna mademu wa Diamond walijaribu kuingiza beef lake na Dai kumkandamiza byser eti jina sijui nini. Na ni kweli kwa maelezo ya Marco chali album zote mbili za kwanza za Diamond sio zake moja ya Bob junior nyingine ya Maneke.
Its ok mkuu lakini kwan ukirekodi ngoma studio, hatimiliki inakuwa ya nani? Ya producer au ya msanii? na msanii akiwa chini ya lebo je? Hatimiliki ni yake au record label?
 
Tatizo la wasanii na baadhi ya vijana ni kukosa kuwa na vision kipindi wakiwa wanapesa,wanafanya matumizi na anasa za kila namna,bila kuwaza kuwa kuna kesho,huyu dogo alihit sana enzi zake,na amefanya show nyingi sana enzi zile,tatizo they dont invest or save,badala yake they buy liabilities kama magari ya gharama na wanawake,"Mr Blue maisha uliyonayo ni matokeo ya Decisions na Choices ulizofanya huko nyuma,so dont blame anybody hapa,you have to take 100% responsibility kwa yote yanayokutokea",komaa usichoke na bado una muda...
blue alihit sana nakumbuka Enzi zake sana sema ndio hivyo starehe za kipuuzi na usela sela wa kijinga jinga ....diamond amewashikisha adabu hwa wasanii wasiojitambua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom