Sawa mpaka hapo tunakubaliana.
Hao mawakili wasiofungamana na chama chama chochote ni akina nani na wanapatikana wapi hapa Tanzania.
Sijui una maana gani na neno makada, lakini nimepitia listi ya viongozi wa Chadema na sijaliona jina la Marando.
Sawa sawa hakuna miiko yoyote ya kitaaluma (ethics) aliyovunja Marando. Sana sana kaweka ushabiki pembeni kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake na hapa Marando yafaa apewe sifa.
Swali ni je, ungependa kuona vibaka wakichomwa moto ?
Lazima tuwe waangalifu sana tunapolitumia neno public opinion tusije tukawa tunaombea laws of the jungle. Kuna mtu kauliza, je mtuhumiwa wa mauaji asipate huduma ya daktari bingwa, mtuhumiwa wa ubakaji asipewe huduma yoyote na mtuhumiwa wa wizi asipewe ulinzi wa polisi. Wakili au jaji akiruhusu mahakama ya maoni ya watu kuzuia utoaji wa haki, huyo haswaa ndiye kakosa maadili ya kitaaluma. Je kwa hawa watuhumiwa kutetewa na Marando, kutazuia vipi kutendeka au kuonekana kutendewa kwa haki ?
Wana JF
Kwanza na-declare interest mm ni mfuasi na mwanachama wa CHADEMA, Hili swala la Marando kuwa wakili wa baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi km vile manji na mahalu litakuja kuwa na madhara makubwa sana hapo badae ktk harakati za chama za kuchua dola natambua kabisa ile ni professional yake na ni vigumu aache kazi aliyoisomea kwa muda mrefu, lakini kabla ya kuchua kazi lazima mtu ufanya client assessment.
Kwa kuwa ameamua kuwa ktk siasa na kufanikiwa kuwa mjumbe wa cc ya cdm ni wakati wake muafaka wa kuhakikisha kimoja kati ya professional yake na siasa hakuna kinacholeta madhara kwa kingine. Kwa hiyo moja ya criteria ya kutumika kwake kum-accept client iwe ni asiwe mtuhumiwa wa ufisadi. Nionavyo mm professional yake kwa sasa inaleta madhara ktk siasa si kwake tu bali kwa Chadema kwa ujumla coz ni vigumu sana mtu kupinga ufisadi majukwaani na kuukubali mahakamani na watu wote wakaamua kukuamini ww ni mpiganaji wa kweli wa ufisadi.
Swala kubwa la sisi wana-chadema tunalotakiwa kulielewa ni kwamba asilimia kubwa ya wananchi hawawezi kutofautisha professional na siasa kiasi kwamba point tutakayoitumia kuuelezea uma ya kuwa hii ni siasa na hii ni professional haitaweza kuzaa matunda yeyote. Marando na uongozi wa juu ulitazame hili kwa mapana na marefu ili nguvu iliyokwisha tumika kukifikisha chama hapa isije kupotea kirahisi kisa mtu mmoja ambae ana uwezo wa kuchua kesi zingine na kuendelea na maisha.
Tujiulize swali dogo kwa mfano leo ROSTAM amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa KAGODA na marando akafanya km anavyofanya kwa wale wa EPA itakuwa sahihi? Au kuwatetea wa EPA itakuwa halali na kumtetea Rostam itakuwa haramu wakati wote ni mafisadi?
Nawasilisha
Wewe ni chadema tawi gani na kadi namba ngapi Mkuu? Ilinikusaidie husiyo ya fahamu!
Unaposema achague mteja kwa kuangalia aina ya kosa analoshtakiwa nalo sijui unajenga hoja yako juu ya nini? unataka kusema kuna makosa ya jinai ambayo CDM inayaunga mkono na yapo mbayo CDM haiyaungi mkono!
Kama ikiwa CDM haiungi mkono makosa yote ya jinai kwanini husiseme kuwa wanachama wa CDM wasimtete mtu yeyote anayeshtakiwa na serikali mahakamani? kama ikiwa vyama vya siasa vitafanya ujinga huo vyote nani atamtetea nani? and then! nini kitafuata au CDM ikichuwa madaraka itapereka mswada wa sheria kuomba mawakili wote wasiruhusiwe kuwa wanachama wa vyama vya siasa? Hii hoja ya ajabu sana.
Kwanini husiseme kuwa watuhumiwa waiperekwe Mahakamani wafungwe moja kwa moja na polisi? Maana Wakili ni sehemu ya Mahakama na kazi ya Wakili si kusaidia mtuhumiwa hasifungwe bali ni kuisaidia mahakama itende haki na itoe hukumu kwa mujibu wa sheria za nchni bila upendeleo wowote.
Haki ya watanzania wanaoshtakiwa ni haki ya kikatiba chama chochote ambacho kinafikia kupingana na haki hizo hakifai mbele ya Jamii kwa ujumla wake maana huwezi kuubiri haki na wakati mwingine ukaipinga, unachotaka wewe kifanyike ndio kinyume na mataraji ya wengi, maana kuitaka CDM ipingane na haki za msingi za watanzania walizopewa kwa mujibu wa sheria.
yah, umejibu sahihi kabisaRole ya Marando ni kubwa sana hasa upande wa kotini kwa maslahi ya wapinzani wote nchini. Siku zote amekuwa akisema hakubaliani na aina ya watu wanaoletwa kotini kwa tuhuma za ufisadi kwakuwa ni dagaa tu, mapapa hayaletwi. Hivi karibuni aliulizwa swali hilo kwenye mdahalo na akina Nape akaeleza hivyo hivyo. Kwa maneno rahisi ni kuwa washitakiwa wa ufisadi wanabambikwa kesi. Fikiria kubambikwa kesi na machungu yake? Ulishawahi kufuatilia au hata kuiskia kesi ya Mahalu? Umeshaskia mashahidi wanaotakiwa Mahakamani kumtetea mshitakiwa? Dogo, TAFAKARI!
nimependa avatar yakoHata mm nimekuwa najiuliza maswali mengi sana kuhusu huyu bw. Marando. Anachukua majukumu ya kuwatetea mafisadi mahakamani lakini anakwenda kuwasema majukwaani. Yaani hii inawachanganya sana watu ambao tayari walishaanza kujenga imani na CHADEMA. Kama Dr. Slaa kwa bahati atapita hapa atolee ufafanuzi suala hili akiwa kama Katibu mkuu wa chama.
tofautisha kati ya daktari na mwanasheria; unapozungumzia daktari unazungumzia uhai wa mtu, lakini c dhani kama unapomtetea fisadi unaokoa uhai wake! kwamba usipomtetea atakufa! kilichompeleka huko marando ni njaa, sasa ili kuinusuru chadema inabidi achagua kati ya siasa au kuwatetea mafisadi! kinyume cha hapo chadema inabidi ifyate mkia kuzungumzia mafisadi, maana huwezi kukipinga kitu ambacho mwenyewe unakitetea huo utakuwa ni unafiki! yaani itakuwa ni sawa na kusema nyama ya kiti ni haramu lakini mchuzi wake unakunywa!!!!!!!!!!!wewe jamaa .... hivi ukiwa kama daktari halafu mwizi akaletwa hospitalini ameumizwa vibaya je hautamtibu kwasababu ni mwizi ?
na mimi naomba nikuulize kaswali kadogo; hivi mh. marando anapokwenda kuwatetea hawa mafisadi anapoulizwa na hakimu kuwa watuhumiwa wake ni wezi, wameiba pesa za epa kwa mfano; huwa anajibu nn? ndio au hapana? yaani kwa niaba ya watuhumiwa marando huwa anakubali au huzikana tuhuma?Mimi nina kaswali kadogo tu kwa mtoa mada, je ni kosa kumtetea mtuhumiwa ? Kama jibu ni hapana, wewe ungetaka hao watuhumiwa watetewe na mawakili wa aina gani au wa chama gani ? Je, kama swala la ethics linazingatiwa katika kuwatetea watuhumiwa, unataka kusema kuwa wale mawakili wasio na ethics ndio wajitokeze kuwatetea ? Na kama ni hivyo hao mawakili wenye sifa za kukosa ethics ni mawakili wa namna gani na ni kama yupi kwa mfano hapa Tanzania.
Sasa wakili kama tayari anayo sifa ya kutokuwa na ethics, kwa nini na yeye asifunguliwe kesi na kama itakuwa hivyo yeye mwenyewe atatetewa na wakili wa aina gani ? Na mwisho hebu tupe mwanga kidogo tu, Marando ungependekeza awatetee wahalifu wa aina gani kwani uhalifu si ni uhalifu tu mbele ya sheria ? Labda mimi ni mzito na sio great thinker lakini kwa kawaida ninavyoelewa, kosa linavyozidi kuwa kubwa ndivyo wakili mashuhuri na makini zaidi anavyohitajika kutoa utetezi.
Je, kwa mfano tu, mtuhumiwa wa kosa kubwa kama la uuaji hastahili kutetewa na Marando kwa sababu Chadema inalaani mauaji ?

kwa uelewa wako ni vigumu sana kuweza kutambua professionalism and its ethical codes of conduct ...... kazi ya wakili ni kumtetea mhalifu na sio kuhukumu yupi ni mhalifu na yupi si mhalifu .... kwani hii kazi ya wakili ni kutetea watu wasio na makosa? ... silly mind ! .... as well daktari jukumu lake ni kutoa tiba kwa mgonjwa pasipo kuangalia ameathirika vipi na ugonjwa wake .... your thinking capacity is very low

hata wewe ukifanya uhalifu sasa hivi ... katiba inasema you have the right for an attorney (legal representative ) na serikali pia ina jukumu la kugharamia wakili wa kukutetea

kwa hiyo chadema na uongozi wote haioni hili na kukemea ni wewe tu mwenye narrow mind unaeona ?

try to be analytical ....

Chukulia wewe in lawyer mzuri sana, na kuna kibaka mmoja amembaka binti yako na kafikishwa mahakamani. Sasa anataka kukukodi umtetee. Je utamtetea?

Chukulia wewe in lawyer mzuri sana, na kuna kibaka mmoja amembaka binti yako na kafikishwa mahakamani. Sasa anataka kukukodi umtetee. Je utamtetea?

kamwe mshitaki hawezi kuwa mshitakiwa naturally (plaintiff as defendant ), hiyo haitakuwa kesi

Mshitaki ni Jamhuri na sio wewe.
ni simple logic too! unahubiri la kupinga ufisadi kesho unaenda kisutu kuwatetea mafisadi!Sawa kabisa mkuu,
Hata mimi niliwauliza hao watu wa sheria na maadili ya uwakili swali kama hilo.....Unaweza kumtetea mtu ambaye ana tuhuma za kumuua baba yako?????