Marando na Prof Safari nao wamcharaza Nape ile mbaya

HA ha haaaa!
Huu sasa ni mchezo tuliocheza zamani tukiwa watoto tukiuita dimba-dimba!
Labda kama gazeti linaeleza mambo mengine zaidi, lakini otherwise hii ni kawaida ya Nape!
 
Unaona ya kawaida kwa sababu wewe ni ccm au? Huoni ni ujinga kuzungumzia mshahara wa mtu kama Dr Slaa anayehangaika mchana na usiku kuwalipua mafisadi. Hivi watu wanafikiria nini wakijua raisi wenu ambaye kila kitu analipiwa analipwa mshahara kiasi gani au wakurugenzi wa mashirika?:pound:
 
Duu hapa pameniacha hoi, hebu tuwekeeni aina ya vipaza sauti hivo. hivi inakuwa je kama jk akinunua mabasi harafu ccm wakamshawishi wayanunue.Ha ha ha ha ufisadi mwingine bwana.

"Alisema katika magari hayo kuna vipaza sauti vyenye thamani ya dola za Marekani 148,000 sawa na Sh. milioni 222, jenereta tatu zilizonunuliwa kwa Sh. milioni 47 kwa kila gari kwamba yana bodi maalumu yenye uwezo wa kubeba watu wasiopungua 12"
 
ha ha ha

"Pia alisema magari hayo kila moja lina uwezo wa kubeba mapipa ya mafuta ya helikopta, jukwaa la kuhutubia na vifaa vya matangazo ambavyo vyote vimejengwa kwa Sh. milioni 48.4."
 
Alisema Mbowe aliombwa, na kamati kuu iliunda kamati ya watu wanne chini ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Mohammed Issa kumwomba akiachie chama mitambo hiyo baada ya majadiliano marefu.

Wajumbe wengine wa Kamati hiyo, waliobariki kuwa ni Mabere Marando, Mkurugenzi wa Rasilimali, Suzan Lyimo (MB) na Anthony Komu, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.

Teh teh teh : boya
 
teh teh teh teh teh

"Kwanza magari yanayozungumziwa chakavu yamenunuliwa nje na kuanzia kazi CHADEMA mpaka leo, na hayajawahi kutumiwa na Mbowe," alisema"

Du kwa hiyo nje , duuuuuuu ndo qualification?
 
Mbowe ametoka kwenye kukopesha fedha mnakodi helkopita anatembea yeye na kuwadai mamilion ye fedha. Sasa amekuja na njia mbadala ya kununua mafuso, teh teh teh bei zenyewe mhhhhh. Thugs tu hawa tusidanganyane. . kama mnabisha leteni picha za fuso hizo tutafute bei yake halali. Pia hivyo vipaza sauti vya robo bilioni.
 
Sorry Nape!! umeshika pabaya brother, Laiti ungelijua ungeendeleza porojo zako uko mitaani, but kwa sasa naona mwishowako kisiasa ndiyo umekaribia. Ulitegemea nini ulipo anza porojo zako za kashfa!! au ndiyo ile stailiyako ya kufikisha ujumbe bila kuuchuja, sasa wenzako wanakucheka kwa sababu ya kuropoka kwako. Kwishaaaa Nape kama nakuona vile!!!!!
 
Pole sana Nape. Bado mapacha watatu hawajakulipua sijui utaficha wapi uso wako. Na ule ujumbe wa kwenye facebook umeishia wapi vile?
 
wabushoma.CCM walishapoteza dira na mvuto.Wakati wa maneno umekwisha,watanzania tunataka vitendo na siyo maneno yaleyale kila kukicha, maendeleo ya watu,kuondoa pengo kubwa kati ya matajiri na maskin,na mgao sawa wa raslimali za taifa.Siasa majukwaani ni kukwepa matatizo ya msingi yanayolikabili taifa
 
Angalieni hizo gharama alizoainisha komu. Hivi mnatetea masilahi gani ya Taifa?
 
Baija Bolobi KUMLIPA SLAA FEDHA HIZO SIYO UFISADI HATA KIDOGO,HE DESERVES SO MUCH MORE THAN THAT,KAZI YA MIKONO YAKE ITAFAIDIWA NA GENERATIONS OF TANZANIANS!!
 
Last edited by a moderator:
Kipigo hicho anakistahili dogo maana amejisahau.

Ni huyu huyu alikuwa akimshutumu sana JK kwa kushindwa kuongoza CCM mpaka inatekwa na mafisadi. Ni huyu huyu aliingia katika deal ya kujiunga na Chadema kwa sharti la kuachiwa jimbo la Ubungo ili Mnyika afanye kazi za chama.

Ninapomuona anawasema Chadema simuelewi.

Yeye apambane na mafisadi wa chama chake aachane na Chadema.

Ufisadi ndani ya CCM na serikali yake ni hatari kuliko "ufisadi" wa Chadema wa kumlipa Dr. Slaa shilingi milioni saba kwa mwezi.

Hivi nyie CDM mbona mnafikir chama chenu ni untouchable wakati sisi tunajua kwamba nayo ina mapungufu mengi sana ambayo nilifikiri huu ndiyo wakati wake wa kuyafanyia kazi kama mnataka chama chenu kije kipewe dhamana ya kuongoza nchi hii hapo baadae. Kuna utoto na ushabiki wa kijinga humu ndani na fikra za kwamba wao CDM peke yao ndiyo wana hati miliki ya kuzungumzia ufisadi, na kwamba mtu aliye CDM ni malaika. Huyu Marando ni mtu ambaye tunajua kwamba ni mchafu. Ndiye beneficiary mkubwa wa proceeds za ufisadi na kila mara amekuwa akitumiwa na hao hao mafisadi kupata kinga ambayo inaiweka nchi hii katika mazingira ambayo haiwezi kuwachukulia hatua.

Anachofanya sasa hivi ni kutumia privileged information inayotokana na kesi za wateja wake ili kutoa tafsiri potofu na hata wakati mwingine kuzitumia kama nyenzo ya kisiasa dhidi ya mahasimu wake. Ukweli ni kwamba Jeetu ni mwizi na kama kwa sababu yoyote ile alitoa chochote kwenda kwa mtu hiyo haina maana kwamba hao waliopewa walihusika na wizi. Ni kama yeye anavyotumia fedha za ada ya uwakili ambazo zinatokana na mapato hayo ya EPA halafu mtu aseme yeye naye ni fisadi. Ni vizuri hoja hizi zijadiliwe kwa haki bila upotoshaji wa kijinga. CDM you are not indispensable, kama kuna ufisadi tutausema na ni vizuri wafuasi wake wawe na maturity na kuelewa kwamba nao wanafanya makosa na inapotokea hivyo waache juvenile arguments na ku-attack personalities.
 
teh teh teh teh teh

"Kwanza magari yanayozungumziwa chakavu yamenunuliwa nje na kuanzia kazi CHADEMA mpaka leo, na hayajawahi kutumiwa na Mbowe, alisema"

Du kwa hiyo nje , duuuuuuu ndo qualification?

Yalinunuliwa na Mbowe yakiwa mapya, yakatumiwa na chama wakati wa uchaguzi, hadi ,ajuzi walipoyahitaji. Hivi hilo gari la TOT CCM walinunua sh gapi?
 
Yalinunuliwa na Mbowe yakiwa mapya, yakatumiwa na chama wakati wa uchaguzi, hadi ,ajuzi walipoyahitaji. Hivi hilo gari la TOT CCM walinunua sh gapi?

Ahaa
Kumbe wizi wa ccm kwa tot chadema wanafuata nyayo zake. Harafu nakushauri usome habari hiyo hapo juu nasio ushabiki tu usio na tija.
 
Whether yalinunuliwa mapya na Mbowe au vinginevyo, ukweli ni kwamba sasa hivi magari haya ni ya Mbowe ambayo yalitumiwa na CDM wa arrangement maalum. Yatakapouzwa CDM yatakuwa yanauzwa kama magari machakavu (used) na kitendo hicho ni kinyume na sheria za manunuzi ya umma na kwa kusisitiza mpango huo na kama utafanikiwa, huo utakuwa ni ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi. Kwa hiyo siyo dhambi kusema kwamba CDM ni mafisadi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom