Marando atangaza kulitetea MwanaHalisi bure

kumbe msemo wa member mmoja humu kuwa Tanzania kuna crummy press ama hakuna press una kaukweli.... ama kweli asiyekubali kushindwa si mshindani.
 
Wakili Mabere Marando anawakilisha Gazeti la Mwanahalisi na pia Mkurugenzi wa Hali Halisi Bw. Saed Kubenea. Je, sasa wana mpango gani baada ya kujikuta wanafungiwa kuchapisha gazeti hilo kwa muda wa miezi mitatu?

Aliyefungia gazeti hilo ni Waziri wa Habari, utamaduni na Michezo Mhe. George Mkuchika. Je alifanya kosa kulifungia gazeti hilo? NI kwanini basi hakuyafungia magazeti mengine ambayo yaliandika habari zinazoshabihiana na zile zilizosababisha gazeti la Mwanahalisi kufungiwa.

Wakati huo huo Kijarida cha "Cheche" nacho kiko mitaani; What a wednesday Eh?

Kupata majibu ya yote hayo sikiliza kidokezo hiki:

[media]http://www.klhnews.com/images/podcasts/maberemkuchikaintro.MP3[/media]
nia ya MKK naona ni kusafisha Mkuchika...na pia anakiuka azimio ya jukwaa la wahariri kutokuandika habari za mkuchika...
 
Wakili Mabere Marando anawakilisha Gazeti la Mwanahalisi na pia Mkurugenzi wa Hali Halisi Bw. Saed Kubenea. Je, sasa wana mpango gani baada ya kujikuta wanafungiwa kuchapisha gazeti hilo kwa muda wa miezi mitatu?

Aliyefungia gazeti hilo ni Waziri wa Habari, utamaduni na Michezo Mhe. George Mkuchika. Je alifanya kosa kulifungia gazeti hilo? NI kwanini basi hakuyafungia magazeti mengine ambayo yaliandika habari zinazoshabihiana na zile zilizosababisha gazeti la Mwanahalisi kufungiwa.

Wakati huo huo Kijarida cha "Cheche" nacho kiko mitaani; What a wednesday Eh?

Kupata majibu ya yote hayo sikiliza kidokezo hiki:

[media]http://www.klhnews.com/images/podcasts/maberemkuchikaintro.MP3[/media]

Yaleyale.

kazi kwelikweli
 
hahahahahahahaha....
Kula tano Mkuu, nimesikiliza mahojiano. Hivi mawaziri wa namna hii tunawapata wapi? Waziri hawezi kujibu hata maswali rahisi naman hiyo? Duh, kaazi kweli kweli? Where does jk get his cabinet ministers, nisaidieni jamani.. Huwa anawachagua kwa vigezo vipi?
 
Ama kweli sasa serikali ina ogopa kivuli chake yenyewe.bila shaka huyo mheshimiwa aliye ambiwa afungie gazeti la Mwanahalisi kasahau kuwa siku hizi kuna technologia ya TEKINOHAMA, Kudhibiti vyombo vya Habari sasa hivi ni ngummu kama kuondoa roho ya mtu.Blogs na podcast zitafanya kazi yake.Serikali hii ijifunze kujikosoa na kukosolewa .
 
Niliposikiliza mahojiano nilicheka sana, lakini baada ya muda nilianza kutafakari nikasikitika. Nimegundua kuwa mkuchika sio waziri wa k, bali ni waziri wangu. What a loss to me? Lakini wakati naendelea kutafakari kauli za waziri wangu mwisho nikashindwa kumuelewa alichoongea, hasa sababu za kufungiwa kwa mwanahalisi Je;
1. Ni kuandika habari za uchochezi (hakusisitiza sana hili na hakuweza kuthibitisha)
2. Ni kutokana na "records" zake za nyuma za kuandika "uongo"? (hili limepata msisitizo)
3. Ni kutokana na kuandika "uongo" kuwa Makongoro alienda dar kwa jk? (msisitizo mkuu)

Nimechanganyikiwa hapo... May God help Tanzania, jk na mawaziri wetu hasa wa aina ya kina mkuchika, la sivyo tumekwisha (ukizingatia kuwa 210 CCM bado ina nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi unless God helps Tanzania as I pray)
 
hahahahahahahaha....
Kula tano Mkuu, nimesikiliza mahojiano. Hivi mawaziri wa namna hii tunawapata wapi? Waziri hawezi kujibu hata maswali rahisi naman hiyo? Duh, kaazi kweli kweli? Where does jk get his cabinet ministers, nisaidieni jamani.. Huwa anawachagua kwa vigezo vipi?

Ni Mawaziri wetu hawa na ni sisi tumewachagua kuwa wabunge. We have to deal with what we got..
 
Mabiti.. umesikiliza ukiwa Bongo au nje ya nchi... ningependa kujua usikivu ukoje nyumbani na umetumia dial up, dsl au internet capability gani?
 
Mabiti.. umesikiliza ukiwa Bongo au nje ya nchi... ningependa kujua usikivu ukoje nyumbani na umetumia dial up, dsl au internet capability gani?

Wakati mwingine inakuwa tatizo kidogo kusikiliza klh nyumbani ukitumia dial ups au providers wasio na nguvu. Muda wote nimekuwa natumia AT&T card kwenye laptop yangu na connection huwa ni nzuri kama vile tu uko magharibi. As longer as ukipata connection, usikivu ni mzuri tu hata kwenye dial ups
 
Marando ampinga Mkuchika

Mwandishi Wetu Oktoba 15, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Ni kwa kufungiwa MwanaHalisi

Ataidai Serikali fidia ya hasara

SERIKALI imekuwa ikilitafuta gazeti la MwanaHalisi kwa muda mrefu hivyo kulifungia wiki hii kunahitimisha mpango huo, wakili na mwanasiasa maarufu, Mabere Marando, amesema.

Marando, ambaye ni wakili wa kampuni ya magazeti ya Hali Halisi, inayomiliki gazeti hilo la kila wiki, amesema pia kwamba wateja wake wamedhamiria kuchukua hatua za kisheria dhidi ya agizo la kufungiwa lililotangazwa Jumatatu na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika.

Alikuwa akizungumza juzi katika mahojiano maalumu kuhusu kufungiwa kwa miezi mitatu kwa gazeti hilo kwenye kituo kimoja cha mtandao wa radio cha Kijijini Leo Hii News (klhnews.com) kinachorusha matangazo yake kutokea Detroit, Marekani. Mahojiano hayo yalikaririwa Dar es Salaam.

Alisema kwa mtazamo wake Serikali ilikuwa tayari imedhamiria kulifungia gazeti hilo linalodaiwa kuandika habari za uchochezi, hata kabla ya kusikia maelezo ambayo ililitaka litowe kwa vile kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikilitafutia sababu ya kulifunga.

" Kabla MwanaHalisi hawajapata muda wa kujieleza, wao (Serikali) wakatoa tangazo kwenye gazeti la Serikali kuhusu kulifungia gazeti hilo," alisema Marando.

Alipoulizwa kuhusu mtazamo wa kisheria Marando alisema kuwa wateja wake wamekwisha kuanza kujiandaa kuchukua hatua za kisheria ili kutengua uamuzi wa Waziri Mkuchika.

Pamoja na kutaka kutengua uamuzi huo Marando amesema: "Kuwazuia kutoa gazeti hilo ni kuwatia hasara, kwa hiyo tutawapa Serikali notisi ya madai kwa kusababishia gazeti hilo hasara".

Kuhusu maoni kwamba Sheria ya Magazeti haitoi nafasi ya uamuzi wa Waziri kutenguliwa, Marando alisema: "Ndiyo Waziri ana uamuzi wa mwisho lakini kuna utaratibu kuwa unapotaka kuchukua hatua ambazo zitamuathiri mtu lazima umpe muda wa kujieleza na hilo Serikali haikulifanya".

Alidai Marando: " Wakati Serikali imetoa barua ya kutaka maelezo toka MwanaHalisi tarehe tisa, kumbe wakati huo huo walikuwa wamekwisha kutuma tangazo la kulifungia gazeti hilo ili lichapwe kwenye Gazeti la Serikali lililotoka kesho yake", akiongeza kwamba inaonekana kuwa Serikali haikuwa na nia ya kusikiliza maelezo ya MwanaHalisi.

" Nia yao ilikuwa ni kutaka kufunga tu. Sheria hairuhusu hivyo. Tunachotaka kufanya safari hii ni kuwafundisha kuwa hata kama wameudhika na kukasirika ni lazima wajisikie kubanwa na sheria", alisema Marando akiongeza kwamba kwa njia hiyo watasaidia kuirudisha Serikali kwenye mstari wa kufuata sheria.

Lakini Waziri Mkuchika, naye akizungumza na mtandao huo huo juzi, alisema kuwa uamuzi wa kulifungia gazeti la MwanaHalisi umepokelewa vizuri na baadhi ya watu ambao wameona kuwa Serikali imekuwa ikivumilia habari za kichochezi.

"MwanaHalisi wameonywa mara nyingi kutokana na maandishi yao, lakini hawakuwa tayari kubadilika," alisema Mkuchika kwenye mahojiano hayo akiongeza: "Kuna habari huko nyuma wamewahi kuandika ambazo ni za uongo. Mojawapo ni madai kuwa Makongoro Nyerere aliondoka Tarime kuja Dar es Salaam kumuomba Rais Jakaya Kikwete ajaribu kuzipatanisha pande mbili za CCM zinazogongana mkoani Mara ili kusaidia uchaguzi wa Tarime. Hilo halikuwa kweli kwani Makongoro mwenyewe amedai kuwa hajawahi kutoka Tarime kuja Dar es Salaam, isipokuwa alipokwenda kwenye mazishi ya mama yake Butiku kule Butiama".

Alipoulizwa ni kwanini amelifungia gazeti hilo na kama kwa kufanya hivyo si kutishia uhuru wa vyombo vya habari, Mkuchika alisema: "Tanzania tuna taratibu zetu; nyie huko (Marekani) mnaweza kuwapiga viongozi wenu mayai lakini sisi hapa tunaheshimu viongozi wetu".

Katika mahojiano yake ambayo, kama ya Marando, nayo yanapatikana kwenye mtandao huo wa Watanzania walioko nje, Mkuchika alisema pia kuwa kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi ni ujumbe kwa magazeti mengine ambayo yanaandika habari za kichochezi na kwamba jambo hilo halitavumiliwa tena.

"Sisi tuna sheria zetu na hizo ndizo tunazifuata, hatufuati sheria za Marekani" alisema Mkuchika ambaye amehojiwa mara kadhaa kwenye mtandao huo.
 
Aisee nimesikiliza mahojiano...................

Kwanza namshukuru sana MMKJJ....
Kwanza inaonekana kuwa Mkuchika ana KIBURI cha ajabu........you can simply tell just from his tone......"wewe elewa unavyoelewa na sisi serikali tutaelewa tunavyoelewa"......damn.......what a dumb respond!!

Pili ana inferiority complex na hawezi kupambana na hoja......"mimi ni waziri wa habari haya magazeti nayasoma kila siku........nimesoma literature...." another dumb respond!!....badala ya kujibu hoja ya msingi yeye anasema anasoma magazeti na eti kuwa alisoma literature.......ni wangapi wamesoma literature na kila siku wanasoma magazeti.....and they simply can't get it.........kama wewe Mkuchika

Shame on you Mkuchika

......inaonekana uamuzi ulikuwa zaidi kwenye personnal zaidi ya utendaji wa just

Mwanakijiji tunashukuru kwa kutufukulia huu uwezo mdogo wa kujibu maswali.......na inaonyesha ni jinsi gani serikali ina kazi ngumu ya kuongoza........kama watu wenyewe ndio kama akina Mkuchika............
 
Back
Top Bottom