Maranda ajihalalishia fedha zilizoibwa EPA

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,139
MFANYABIASHARA maarufu ambaye pia ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rajabu Maranda, anayedaiwa kuiibia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Sh bilioni 1.8 za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), amekiri kujipatia fedha hizo na kudai ziliingizwa kihalali.

Maranda alidai hayo jana wakati akitoa ushahidi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akiongozwa na Wakili wake, Majura Magafu, akisema madai yote dhidi yake na mwenzake Farijala Hussein si halali na kuiomba Mahakama kuyatupilia mbali.

Alidai hakuna kipindi chochote alichokaa na kupanga kuiibia BoT bali fedha hizo waliingiziwa katika akaunti waliyofungua kwa jina la biashara la Kiloloma & Brothers Limited.

Akielezea namna fedha hizo zilivyoingizwa na BoT mikononi mwao, alidai kuwa hakumbuki ni kipindi gani lakini mwaka 2005 Hussein ambaye ni binamu yake, alifika katika ofisi yake barabara ya Bagamoyo katika kituo cha mafuta cha BP, Mbezi Beach, akiwa na mtu aliyemtambulisha kwake kama Charles Kisa na kumweleza kwamba mtu huyo anahitaji msaada.

Aidha, alidai baada ya maongezi ya muda mrefu na mtu huyo alihitaji kuazimwa Sh milioni 500 kwa ajili ya kudai deni BoT alilokabidhiwa na Kampuni ya BC Cars Export ya Mumbai India, walikubaliana, kwa sababu mtu huyo anamiliki Kampuni ya Kiloloma & Brothers, ambayo ndiyo inayotakiwa kudai fedha hizo na hivyo awaingize katika umiliki wa kampuni hiyo ili wadai pamoja.

“Charles baada ya maongezi ya siku hiyo na kukubaliana, ilichukua siku mbili akaleta karatasi kutoka Brela za kuruhusiwa kuwa wabia katika kampuni hiyo nasi tukawa na uhakika wa fedha hizo, hivyo sikuwa na neno nikampa Sh milioni 500 kama alivyoomba.

“Tulikubaliana kugawana faida itakayopatikana ambayo ni asilimia 40,” alidai Maranda na kuongeza kwamba aliwaonesha pia kivuli cha nyaraka za kuhamisha deni kutoka BC Cars kwenda kampuni yao ambayo tayari ilikuwa imepelekwa BoT kudai deni hilo.

Aliendelea kudai kuwa Charles ndiye aliyekwenda Brela kubadilisha majina ya wamiliki wa Kiloloma, baada ya hapo Hussein alikwenda Benki ya Afrika kufungua akaunti nyingine ya kampuni hiyo na mtia saini akawa Maranda, ili kudhibiti utokaji wa fedha ili ile ya kwao irudi.

Baada ya hapo namba ya akaunti hiyo ilipelekwa na Charles BoT kwa ajili ya fedha hizo kuingizwa.

Alidai, pia kuwa muda mfupi baadaye, fedha ziliingia katika akaunti hiyo na walipotaka kutoa zile Sh milioni 500 alizomwazima Charles, benki iliwakatalia mpaka wajue uhalali wa fedha hizo, ambapo Naibu Gavana, Juma Reli, aliwaeleza kuwa fedha hizo ni halali hazina matatizo, na wao kuruhusiwa kuzitoa.

Alidai baada ya kutoa fedha za Maranda walitoa ile asilimia 60 na kutuma India kulipa deni na baadaye kuendelea na utoaji.

Alisisitiza kwamba hakuna malalamiko yoyote waliyopata katika upokeaji na utoaji wa fedha hizo mpaka sasa si kutoka BoT wala BC Cars.

Katika maswali na mawakili wa Serikali, Maranda alikiri kutokuwa makini kusoma nyaraka alizokuwa akiletewa na Charles katika mchakato huo wa kutoa fedha, alidai hakuwa makini kuzisoma yeye alikuwa tu akiangalia kama fedha zipo na pia majina yao yeye na Husein yapo.

Hata alipooneshwa vielelezo vya Mahakama vilivyokuwa vikionesha kwamba Kiloloma ilisajiliwa wakati mchakato wa kudai deni BoT umeshaanza ikiwa na namba ya usajili, alidai yeye hajui hilo.

Ilidaiwa na mawakili hao kwamba Kiloloma ilipewa usajili kwa jina la Charles Kisa Aprili 14, 2005 wakati iliwasilisha maombi BoT ya kudai deni hilo Aprili 5 mwaka huo huo.

Hatimaye Wakili wa Serikali Kuu, Boniface Stanslaus alimhoji Maranda: “Nyie mliendelea kutega kwenye hela tu wakati Charles alienda BoT mlikoona kwenye hatari?” Maranda akajibu “hapana”.

Mara kadhaa shahidi huyo alidai kuwa alichokuwa anajali zaidi ni fedha kwani ndiyo maisha, hata nyaraka alizokuwa akiletewa hakutilia maanani kuzisoma.
 
Nikiwaambia kesio hii ya EPA wameuziwa watu na watatoka hatiani very soon mtaniona mshamba
 
Nchi yetu imekwisha!Tuendelee kucheka cheka,watu wetu vijijini wanahangaika,viongozi wetu kila siku kuruka Ulaya,hela yetu inaishia kwa wahindi,hakuna hata mtu mmoja anasota KEKO kutokana na EPA!Oh my GOD!Tumekosa nini kwa Mungu sisi Watanzania?Akina Rashis Maranda wametumiwa na viongozi wa SISIEM,kuchota hela !!!
 
huyu bwana nasikia alituletea VOG KUPITIA NDEGE YA BRITISH AIRWAYA CARGO AWAKUAMINI WAKUU WA UK WENYEWE HATIMAE LILISHUKA NA DADA ZETU WAKAUZWA SANA NA WAHANGA HAWA
 
Back
Top Bottom