CPU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 3,863
- 686
Marafiki ni sehemu muhimu sana kwenye maisha ya kila mmoja wetu. Kila siku tunashauriana ishu za mapenzi..tunapeana tahadhari na kushauriana pia kufarijiana ila nadhani swala la urafiki hatulipi uzito ipasavyo!!!
Kama tunavyolipa umuhimu swala la kuchagua nani anafaa kua mpenzi wako ndivyo ilivyo muhimu kuchagua marafiki pia.Kuna aina za marafiki ambao wakati mwingine inabidi tukae mbali nao....marafiki wagomvi, waongo,wafitini, wachonganishi,wambea,wenye wivu kiasi cha kutopenda maendeleo yako, wasio na heshima n.k
Ndani ya wiki mbili nimeshuhudia
.....wasichana wawili wanaoitana marafiki, wanaochekeana wakiwa pamoja wameharibiana mambo yao vibaya sana.
.....Mwingine alikua na tatizo na mwenzake kama watu wazima badala ya kuyamaliza wenyewe akafikisha mpaka taarifa ambazo hazikupaswa kwa mzazi wa mwenzake.Hao ni watu wazima ila bado wanakua kama watoto!!!
.....Mwingine amembeza mwenzake kwamba hana busara.
Kwenye makundi yote hayo matatu hamna heshima ya kweli, urafiki uliojaa mapenzi ya ukweli wala ukomavu wa akili.Siku zote sio vizuri kua rafiki na mtu ambae hajakomaa kiakili sawa na wewe kwasababu ni rahisi sana kutokuelewana nayo inaweza kupelekea chuki inayoweza kuharibu kabisa utu wa mtu....mkaishia kuchukiana maisha!!
Kitu kingine ni kwamba mara nyingi watu unaoonekana nao wanakudefine ulivyo...inawezekana kabisa sivyo ila kama mtu hakufahamu anachukulia kile anachoona au kusikia kuhusu kundi lile la wadada/wakaka kama tabia yako binafsi...kwahiyo kaa mbali na watu usiopenda kuhusishwa nao!
Nwyz nimeona tu tukumbushane umuhimu wa kuchagua marafiki.Kua rafiki na mtu unaeelewana nae lugha...heshimianeni na mpendane.Ukishamwita mtu rafiki yako then unakua na jukumu la kulinda hadhi/sifa ya mwenzako badala ya kuiharibu, kumpa moyo badala ya kumvunja, kumpa faraja badala ya kumpa wakati mgumu, kumheshimu badala ya kumdaharau, kumtunzia siri badala ya kuivujisha n.k.
Tupendane!!
Nawakilisha!!!
Pengine tujiulize yafuatayo kwanza, je nini definition ya RAFIKI???
Je watu unaokutana nao makazini na maofisini na mnafanya kazi pamoja ni automatically marafiki au sio marafiki??
Je inawezekana mtu unafanya nae kazi kila siku ofisi moja usiwe na urafiki nae (kama uliamua kumkwepa) ???