Maradhi yanayomsibu binadamu na tiba yake

MATATIZO YA MACHO: KONJACTIVA (CONJUCTIVITS): Ni maradhi ya macho sehemu ya utando au ute sehemu ya conjuctiva, ambayo inaunganisha sehemu ya ndani ya jicho na kope. SABABU:

Yanaweza kusababishwa na vumbi, moshi, upepo ulio na ubaridi, kuweza kutumia macho kwa muda mrefu kutizama kwa mfano kusoma, kukaa katika mwanga mkali wa jua, upepo wenye ukavu na ujoto wenye hali ya umoto, mvuke, gesi, moto, kemikali, n.k.

DALILI
: Kujikuna, kuvimba macho, macho kuwa mekundu, macho kutoa maji au machozi, kuhisi kuna mchanga ndani ya macho, kuogopa mwanga mkali, n.k.

TIBA: Weka macho yawe safi na uyakoshe kwa maji ya baridi. Epusha macho kutokana na joto, baridi, moshi, vumbi, macho yasitumie nguvu sana kama vile kusoma sana. Tumia dawa za kulainisha choo ikiwa hupati choo vizuri kwa sababu pia huchangia katika maumivu ya kichwa na macho.

MARADHI YA KUTOPATA CHOO (CONSTIPATION):

Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huwa hapati choo kwa wepesi. Haja kubwa inaweza kutoka baada ya siku moja au mbili au zaidi na ikitoka huwa ni kigumu na hutoka kwa shida na wakati mwingine huwa kama cha mbuzi. Wagonjwa wengine hupata maumivu wakati wa kwenda haja kubwa. Mtu mwenye afya nzuri hupata haja kubwa kwa kiwango cha chini mara moja kwa siku. Na choo huwa laini na hutoka bila matatizo.

SABABU ZA MARADHI HUSIKA:
(1) Upungufu wa vitamini mwilini hasa vitamin B.
(2) Maradhi ndani ya utumbo mpana.
(3) Kula vitu vigumu na vikavu kama vile vyakula vya ngano.
(4) Upungufu wa ulaji matunda na mboga.
(5) Kutokunywa maji ya kutosha.
(6) Upungufu wa fibre kwenye chakula zinazopatikana kwenye maganda ya mahindi.
(7) Ukosefu wa kufanya mazoezi ya viungo.

TIBA: :
Chukua glasi moja ya maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili vikubwa vya Asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habitsoda. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.

Tiba ya Pili: Kunywa kwa wingi maji ya Uvugvugu ya kunywa ya kutosha na pia ule kwa wingi matunda na mboga za majani.

Tiba ya Tatu: Kula kila siku asubuhi tende saba kabla ya chakula cha asubuhi. Tende hufanya choo kuwa laini. H. MARADHI YA

KUHARISHA: MARADHI ya kuharisha ni maradhi ambayo mgonjwa hupata haja kubwa mara kwa mara na haja kubwa huwa laini na wakati mwingine huambatana na gesi au maumivu.
SABABU ZAKE: (1) Kula chakula kichafu. (2) Kula chakula kilichoingia viini vya maradhi.

TIBA: Chukua kijiko kimoja cha Maua ya babu naji (chamomile) ukoroge ndani ya kikombe cha chai na maji ya moto. Yakishapoa unywe bila ya kuongeza sukari.Fanya hivyo kutwa mara tatu. Ndani ya babunaji mna virutubisho vyenye uwezo wa kusitisha kuharisha.

Tiba ya pili: Chukua anisuni (aniseed) kijiko kimoja kidogo uweke ndani ya kikombe kimoja cha chai cha maji ya moto yaliyochemka kisha ukoroge. Wacha dawa ikae ndani ya maji dakika tano kisha uchuje halafu uongeze asali kijiko kimoja. unywa kikombe kimoja kutwa mara mbili. Zaidi ya hayo, tukuweke wazi tu kuwa, dawa hii pia huvipa nguvu jamii ya viungo vya kulia chakula.



 

KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA:
Hali ya kujisikia kuwa unataka kutapika lakini hutapiki inaitwa kichefuchefu (Nausea). Hali hii ni kawaida sana hasa wakati unaposafiri kwa chombo kama meli au ndege, hali ya ujauzito,kupata harufu mbaya, kuona au kuhisi kinyaa baada
ya kuona kitu au chakula Fulani kibaya chenye ladha na harufu mbaya, wengine hupata kichefuchefu akimuona mtu mwengine akitapika. Hali ya kichefuchefu humsababishia mtu kuweza kutapika wakati mwingine.

TIBA: Chukua kijiko kimoja kidogo cha unga wa pilipili manga ukoroge ndani ya glasi moja ya maji halafu ukamulie ndani yake ndimu nusu. Kunywa glasi moja kutwa mara tatu.

MARADHI YA GESI TUMBONI (COLIC): Msokoto wa tumbo

Ikiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri tumboni, hukusanya gesi tumboni na kufanya mingurumo humo na kumsababishia maumivu, humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka jasho na machovu bila ya

kufanya kazi. Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu kuumwa kwa mgongo au kiuno. Ikiwa gesi hii itakosa kutoka kwa njia ya haja kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya presha sehemu au

karibu ya moyo na kusababisha maumivu ya moyo.

TIBA: Chukua asali robo lita , unga wa arki susi vijiko vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili vikubwa. Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni.


Hemorrhoids, Pils, MARADHI YA BAWASIRI (MGORO) FUTURU:
Haya ni maradhi ambayo humsibu mgonjwa sehemu ya haja kubwa ambayo humsababisha kupata maumivu.
DALILI ZAKE:
(1) Kupata choo kigumu.
(2) Kutokwa damu sehemu ya hajakubwa baada ya kujisaidia.
(3) Muwasho au maumivu na joto kali sehemu ya bawasiri.
(4) Kupata maumivu wakati unapokaa.
(5) Vidonda au kutokwa nje na kijinyama sehemu ya kutokea haja kubwa.
(6) Upungufu wa nguvu za kiume.

TIBA: Jambo la kwanza
kabla ya tiba mgonjwa aweze kutibiwa maradhi ya kutopata choo vizuri ikiwa anayo kwa sababu huzidisha maradhi haya. Pia epuka kula Nyama hasa ya ngombe, Pilipili na vitu vikali. Halkadhalika usinywe maziwa kwa wingi.

Tiba: Kunywa juisi ya tikiti maji asubuhi kabla ya chakula na usiku kabla ya kulala.Dawa hii hutibu na kuondoa maumivu ya bawasiri.

Tiba ya Pili: Ikiwa ni bawasiri ya kutoka nje au yenye vidonda, paka mafuta ya nyonyo.


MATATIZO YA HEDHI: Matatizo ya Hedhi yanawagusa moja kwa moja

hata hivyo nayo yana tiba yake inayolingana na aina ya tatizo husika.


TIBA YA HEDHI ILIYOFUNGA (AMENERRHOEA)
: Kanuni ya kwanza: Tafuna ufuta kiasi cha kijiko kimoja kila siku mara tatu. Fanya hivyo hadi upate hedhi. Ni bora zaidi kula ufuta kabla ya zile siku ambazo hedhi hutoka na uendelee wakati inapotoka hedhi. Dawa hii ni hatari kwa mwanamke mja mzito, hivyo atahadhari nayo,na tangu hapoyeye haimuhusu.

TIBA YA HEDHI ISIYOTOKA VIZURI: Chukua Jirjir (rocket) kijiko kimoja ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa uchuje. Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kutwa mara tatu.

TIBA YA HEDHI INAYOTOKA KWA WINGI ZAIDI YA ADA:
TIBA Kanuni ya kwanza
Chukua kijiko kimoja cha maua ya Babunaji (Chamomile) ukoroge ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto. Yakishapoa, unywe kikombe kimoja kutwa mara tatu kabla ya kula.



TIBA YA MAUMIVU YA HEDHI YANAYOTOKA KIDOGOKIDOGO (DYSMENORRHOEA):
Tiba: Chukua Nanaa na utayarishe mfano wa chai. Kunywa kikombe kimoja cha chai kutwa mara tatu.

Tiba ya Pili:
Chukua mvuje wa kidonge (kidonge kimoja ) na unga wa pilipili manga (black Peper) gramu 50. Weka dawa hizi mbili ndani ya glasi moja ya maji kisha uifunike na uiache ilowane. Bila ya kuchuja kunywa kijiko kimoja kikubwa kutwa mara moja .Rudia tena kunywa siku ya pili ikiwa hujapata mabadiliko.Dawa hii huzibua hedhi iliyoganda au kufunga.

TIBA YA HEDHI INAYOCHELEWA KUTOKA KWA SIKU ZAKE AU KUTOKA KABLA YA SIKU ZAKE KUFIKA: Hapa maana yake ni kuwa baina ya hedhi mbili huenda yakakaribiana sana au kuachana sana kinyume na ada. Yaani siku za tarehe zake haziendi sawa Chukua bakdonise (parsley) gramu 50 kisha uweke ndani ya maji lita moja, ichemshe kwa muda wa dakika tano na ikishapoa uchuje. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili.

MARADHI YA MATATIZO YA MKOJO: UCHAFU kutoka mwilini hutolewa nje ya mwili kwa mfumo wa mkojo, kinyesi, jasho kupitia kwenye ngozi. Ikiwa kutatokea kizuizi chochote cha kuzuia uchafu kutoka mwilini sumu ya uchafu huu baadae huchanganyikana na damu na kusababisha maradhi mbalimbali.Figo ni kiungo ambacho hutoa sumu mwilini kupitia njia ya mkojo.

VIJIWE VYA KIBOFU CHA MKOJO (DYSURIA): Maradhi haya hutokea kwa kupatikana vijiwe kwenye kibofu cha mkojo. Vijiwe hivi huzuia mkojo kutoka vizuri na kufa yatoke matone matone.

SABABU:
(1) Kula nafaka mbichi kwa mfano: mchele, mahindi, njugu karanga, n.k.
(2) Vyakula vilivyoisha muda wake wa matumizi au vyakula vyenye viwango vya chini ambavyo havistahiki kuliwa na binadamu.
(3) Vyakula vigumu ambavyo tumbo haliwezi kusaga vizuri na hata likisaga, litasaga kwa mashaka kwa mfano chakula ambacho hakijaiva vizuri au nyama ngumu.
(4) Kutotafuna chakula vizuri kwa sababu ndani ya tumbo hamna meno, kwa hivyo utalipa tumbo kazi ya ziada.

TIBA: : Chukua mbegu za matango vijiko vitano vikubwa na mbegu za tikiti maji vijiko vitano vikubwa uchemshe kwenye maji robo lita. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili.

MKOJO AMBAO HAUTOKI AU HUTOKA MATONE: TIBA YAKE: Chukua kikombe kimoja cha uji wa ngano uchanganye na kijiko kimoja kidogo cha unga wa uwatu na kijiko kimoja kikubwa cha samli safi ya ngombe. Koroga kwa kijiko. Kunywa kikombe kimoja kutwa mara mbili. Dawa hii hutibu mkojo ambao hautoki au hutoka matone madogo.

KUTOKWA KWA MKOJO KWA WINGI BILA YA KHIARI (POLYURIA): Haya ni maradhi ya kutokwa na mkojo bila ya khiari . Kabla mkojo haujakusanyika vizuri kwenye kibofu cha mkojo na mgonjwa kujiandaa kwenda25
chooni, hutokwa na mkojo hata kabla ya kufika chooni.

SABABU:

(1) Kulegea kwa kibofu cha mkojo.
(2) Maradhi ya kisukari.
(3) Kuwa na minyoo tumboni.
(4 Kutumia madawa ambayo huchochea kutokwa kwa mkojo.
(5) Kuwa katika mazingira au hali ya
hewa ya baridi.
(6) Kunywa kwa wingi vinywaji, pombe,n.k.

TIBA:: Chukua kijiko kimoja kidogo cha chai cha unga wa harmal, vijiko viwili vikubwa vya unga wa tangawizi,kijiko kimoja cha unga wa mdalasini na vijiko viwili vikubwa vya unga wa pilipili manga. Vichanganye vyote pamoja. Changanya kijiko kimoja cha chai ndani ya kikombe cha maji ya moto ukoroge na yakishapoa unywe kikombe kimoja
kutwa mara mbili asubuhi kabla ya chakula.



KIKOJOZI: Kikojozi ni mtu ambae hukojoa kitandani usiku au mchana wakati anapokua amelala usingizi. Anaweza kuwa mtoto au mtu mzima. SABABU: Sababu kubwa za mtu kuwa kikojozi ni pamoja na Kulegea kwa kibofu cha mkojo Kuota usingizini kuwa mtu anakojoa, na kuwa na usingizi mzito kuliko kiasi.

KULEGEA KIBOFU: Ikiwa kibofu cha mkojo kimelegea mkojo utakua hauna kizuizi cha kuzuia unapokua umeshakusanyika kwenye kibofu.

TIBA:
Chukua asali nusu lita, unga wa kamun aswad vijiko sita vikubwa na unga wa habat soda vijiko vitatu vikubwa halafu ukoroge vyote pamoja. Chota vijiko viwili vikubwa vya mchanganyiko huu wa dawa ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto halafu unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili.

KUKOJOA KWA SABABU YA NDOTO: Sifa ya mtu anayekojoa kitandani akiwa usingizini anaweza akaota kuwa amekwenda chooni kukojoa lakini akiamka asubuhi anajikuta kuwa amekojoa kitandani, na anapokuwa anakojoa kitandani huwa anahisi raha wakati ule wa kukojoa.

SABABU:


Hii huwa ni athari za ndoto za kishetani kwa sababu shetani humuotesha ndoto za kukojoa na akamkojoza kwa kihakika. Hali hii pia huwatokea watu wazima bila kujali jinsia wala umri, wazima au wagonjwa.

TIBA: ( Kwa aliyekuwa ni Muislam) Hakikisha umeshika udhu kabla ya kulala halafu usome kabla ya kulala Ayatul Qursii, Suratul-Ikhlas, Suratul Falaq na Suratul Nas mara tatu tatu kama inavyosema hadithi. Pia kabla ya kulala uombe dua ya kulala. Ukifanya hivyo shetani atakaa mbali nawe na ndoto hizi hazitatokea tena. Kwa Aliyekuwa ni Mkristo Asome Dua za ndani ya Biblia

ANAEKOJOA KWA SABABU YA USINGIZI MZITO:
Hali kama hii huwatokea watoto ambao hucheza sana mchana kisha wakachoka. Wanapoenda kulala huwa wamechoka sana na hata usiku wakati wamelala hawawezi kupata hisia ya kutaka kwenda kukojoa chooni kwa sababu wamezidiwa na usingizi.


TIBA: Tiba yake ni mtoto aweze kupunguza mchezo na aweze kulala kidogo mchana kama ilivyo katika mafundisho ya sunnah. Tiba ya pekee ni mtoto adhibitiwe na kupangiwa ratiba za kucheza, na kupangiwa muda wa kutosha kuweza kupumzika, ikiwezekana alale mchana kidogo.

Source. Herbalist Dr. Mzizimkavu
 
  • Mshubiri - Aloe - kuungua, vidonda vy amafua, ngozi iliyokauka, uchungu, kuchomeka na miale ya jua.
  • Arnica – kuchubukwa na kufura. Paka krimu ya Arnica au umeze vidonge vya Arnica ili kuzuia kufura au kuchibukwa.
  • Echinacea - mafua, maambukizi, kutibu vidonda
  • Mbegu za Flax– kuzuia saratani, gesi kwa tumbo, cholestroli ya juu mwilini, kukoma hedhi, ugonjwa wa mdomo na meno, shida za wakati wa hedhi
  • Garlic – kutibu na kuzuia saratani, ugonjwa wa moyo, shida za kutembea kwa damu, cholestroli ya juu, shinikizo la damu, maambukizo ya ngozi
  • Ginkgo Biloba – inasaidia kusafirishwa kwa damu, zuia kupoteza fahamu, kuumwa na kichwa, mfadhaiko
  • Ginseng – shinikizo la damu, ugonjwa wa sukari, mfadhaiko
  • Lavender – kuumwa na kichwa, mfadhaiko, kukatwa,kuchomeka, kuumwa na kudingwa na mdudu na kukosa usingizi. (si salama kwa mama wajawazito)
  • Melatonin - Alzheimer's, kutibu saratani, mfadhaiko, UKIMWI, kukosa usingizi
  • Rescue Remedy - mshtuko, wasiwasi or kukosa usingizi
  • St. John's Wort - mfadhaiko, uchovu, kukosa usingizi, uchungu, PMS, ponya vidonda
  • Mafuta au dawa ya kuchua yaTea-Tree – kuzuia kuvu na kuponya vodonda vya kuchomeka au kukatwa, chunusi, jipu na kuumwa na wadudu.
 
Asante sana Mkuu,
kwa ukweli baada ya kustaafu nina hakika ya bonge la ajira,
asante sana, MUNGU aendelee kukutunza mkuu.

Naomba unijuze dawa ya bahati. (naongea pole pole wasisikie hawa watoto
watanisuta bure japo na wenyewe watafaidika).
 
Asante sana Mkuu,
kwa ukweli baada ya kustaafu nina hakika ya bonge la ajira,
asante sana, MUNGU aendelee kukutunza mkuu.

Naomba unijuze dawa ya bahati. (naongea pole pole wasisikie hawa watoto
watanisuta bure japo na wenyewe watafaidika).
Mimi Ninakupa Dawa ya Bahati jaribu kupata Majani ya mkunazi uyaweke nyumbani kwako sehemu ya kivuli ndani ya nyumba yako mpaka yakauke kisha uyatwange hayo

majani ya mkunazi kisha uchanganye na maji uwe yale maji yake kila unapotaka kutoka nje ya nyumba yako jipake mwilini mwako pamoja na usoni kwa manuwizo yako kisha utoke nje nenda na shughuli zako ukafanye uyatakao utaona bahati ikikujia kila upande kwa baraka ya huo mti wa peponi mkunazi.. Fanya hiyo kwa muda wa kama mwezi kisha unipe feedback.
 
MARADHI YA KUHARISHA:
MARADHI ya kuharisha ni maradhi ambayo
mgonjwa hupata haja kubwa mara kwa mara na
haja kubwa huwa laini na wakati mwingine
huambatana na gesi au maumivu.

SABABU ZAKE:
(1) Kula chakula kichafu.
(2) Kula chakula kilichoingia viini vya maradhi.

TIBA:
Chukua kijiko kimoja cha Maua ya babu naji
(chamomile) ukoroge ndani ya kikombe cha chai na

Tiba ya Pili:
Chukua anisuni (aniseed) kijiko kimoja kidogo
uweke ndani ya kikombe kimoja cha chai cha maji
ya moto yaliyochemka kisha ukoroge. Wacha dawa
ikae ndani ya maji dakika tano kisha uchuje halafu
uongeze asali kijiko kimoja. unywa kikombe kimoja
kutwa mara mbili.
Zaidi ya hayo, tukuweke wazi tu kuwa, dawa hii
pia huvipa nguvu jamii ya viungo vya kulia
chakula.

KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA:

Hali ya kujisikia kuwa unataka kutapika lakini
hutapiki inaitwa kichefuchefu (Nausea). Hali hii ni

kawaida sana hasa wakati unaposafiri kwa chombo
kama meli au ndege, hali ya ujauzito,kupata harufu

mbaya, kuona au kuhisi kinyaa baada ya kuona
kitu au chakula Fulani kibaya chenye ladha na

harufu mbaya, wengine hupata kichefuchefu
akimuona mtu mwengine akitapika. Hali ya
kichefuchefu humsababishia mtu kuweza kutapika
wakati mwingine.

TIBA:
Chukua kijiko kimoja kidogo cha unga wa pilipili
manga ukoroge ndani ya glasi moja ya maji halafu
ukamulie ndani yake ndimu nusu. Kunywa glasi
moja kutwa mara tatu.

GESI TUMBONI (COLIC):

Ikiwa mtu atakula kwa wingi vyakula vinavyoleta
gesi halafu vyakula hivyo visisagike vizuri

tumboni, hukusanya gesi tumboni na kufanya
mingurumo humo na kumsababishia maumivu,
humkosesha mtu utulivu na kumfanya kutoka

jasho na machovu bila ya kufanya kazi.
Mtu hujisikia mara kwa mara aende haja kubwa na
akienda hapati choo. Pia humsababishia mtu

kuumwa kwa mgongo au kiuno.
Ikiwa gesi hii itakosa kutoka kwa njia ya haja
kubwa, basi yaweza kupanda juu na kufanya
presha sehemu au karibu ya moyo na kusababisha
maumivu ya moyo.

TIBA:

Chukua Asali safi mbichi iwe ya Asali ya nyuki robo lita , unga wa arki susi vijiko
vitatu vikubwa na unga wa habat soda vijiko viwili

vikubwa. Koroga zote pamoja kwa kijiko. Chukua
vijiko viwili vya mchanganyiko huu ukoroge ndani

ya kikombe cha maji ya moto halafu yakishapoa
unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi

na jioni.

Ugonjwa wa BAWASIRI (MGORO): hemorrhoids, piles
Haya ni maradhi ambayo humsibu mgonjwa
sehemu ya haja kubwa ambayo humsababisha
kupata maumivu.

DALILI ZAKE:
(1) Kupata choo kigumu.
(2) Kutokwa damu sehemu ya haja kubwa
baada ya kujisaidia.
(3) Muwasho au maumivu na joto kali sehemu
ya bawasiri.
(4) Kupata maumivu wakati unapokaa.
(5) Vidonda au kutokwa nje na kijinyama
sehemu ya kutokea haja kubwa.
(6) Upungufu wa nguvu za kiume.

TIBA:
Jambo la kwanza kabla ya tiba mgonjwa aweze
kutibiwa maradhi ya kutopata choo vizuri ikiwa

anayo kwa sababu huzidisha maradhi haya. Pia
epuka kula Nyama hasa ya ngombe, Pilipili na vitu

vikali. Halkadhalika usinywe maziwa kwa wingi.

Kanuni ya kwanza:

Kunywa juisi ya tikiti maji asubuhi kabla ya
chakula na usiku kabla ya kulala.Dawa hii hutibu
na kuondoa maumivu ya bawasiri.

Kanuni ya pili:

Ikiwa ni
bawasiri ya kutoka nje au yenye vidonda, paka
mafuta ya nyonyo . na pia uende Hospitali kufanya oparesheni kuiondowa kabisa hiyo iliyotoka nje Bawasiri.

Source. Herbalist Dr. Mzizimkavu
 
KUJITIBU KWA HABBAT SAWDAA (HABA SODA - CHEMBE NYEUSI) NIGELLA SATIVA SEED

HABBAT SAWDA  TIBA MBADALA YA MARADHI YA UKIMWI.jpg



"Habbat-Sawdaa inatibu kila Maradhi isipokuwa Mauti"

Yafuatayo hapa chini ni baadhi ya matatizo na magonjwa ambayo yanaweza kutibika kwa kirahisi kwa kutumia Habbat-Sawdaa.
Kwa faida ya Afya kwa ujumla:

Kunywa kijiko kimoja cha mafuta ya Habbat-Sawdaa asubuhi na usiku, au kunywa japo asubuhi kabla ya kifungua kinywa, unaweza kunywa kijiko kimoja cha mafuta peke yake au ukachanganya na kijiko kimoja cha asali safi.

Vipele (chunusi) Na Ngozi:

Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu) kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple). Paka katika sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.

Upara (Alopeshia):

Sugua mafuta ya Habbat-Sawdaa katika mabaka yanayokusumuba.

Pumu:

Tia ½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.

Kuumwa kwa Mgongo (Sehemu ya Chini):

Changanya asali pamoja na ¼ (robo) kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.

Mwiba Wa Nyuki Na Nyigu:

Tia ½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.

Kibofu cha Mkojo/Figo:

Kunywa maji ya moto yaliyochanganywa na½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa pamoja na asali kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Changanya vikombe viwili vya Habbat-Sawdaa iliyosagwa na ½ (nusu) kikombe cha asali safi. Kunywa kijiko kimoja cha mchanganyiko pamoja na kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Mchanganyiko unaweza kukaa kwa siku 15 na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.

Jiwe La Figo:

Kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyochanganwa pamoja na gilasi (bilauri) moja ya asali, vitunguu saumu vitatu vilivyosagwa na karafuu. Changanya vitunguu saumu pamoja na asali na Habbat-Sawdaa. Kunywa kijiko kimoja kabla ya kula chakula na kwa pendekezo kula limau (bila ya kumenywa). Rudia haya kwa wiki moja Insha-Allah jiwe litaondoka.

Maathiriko Ya Figo:

Changanya baadhi ya Habbat-Sawdaa pamoja na mafuta ya alizeti. Chukua mchanganyiko na weka katika sehemu ambapo figo limeathirika. Kunywa kijiko cha Habbat-Sawdaa asubuhi. Rudia haya kwa muda wa wiki moja Insha-Allah maathiriko yatatibika.

Mafua:

Chukua mbegu za Habbat-Sawdaa 21, ziweke katika kitambaa na roweka usiku. Tumia kama matone kwenye pua siku ya pili nusa poda ya Habbat-Sawdaa iliyomo katika kitambaa.

Kikohozi:

Tumia matone matatu au manne ya mafuta ya Habbat-Sawdaa kwenye kahawa au chai.

Bawasiri:

Kula unga wa Habbat-Sawdaa pamoja na maji.

Shinikizo la damu (high blood pressure):

Changanya kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, kijiko kimoja cha asali safi na kitunguu kiasi kidogo. Chukua mchanganyo kabla ya kufungua kinywa kwa siku ishirini.

Uwasho Na Maumivu Ya Jino Na Ufizi:

Chemsha Habbat-Sawdaa katika siki na itumie kwa kusukutulia meno na ufizi. Na jikinge kutumia dawa za msuwaki za kibiashara na tumia dawa za msuwaki ambazo zinatengenezwa kutoka kwenye nyuzi za mboga za mti wa siwak ambao kwa karne ulikuwa unatumiwa na Wahindi, Waafrika na Waarabu, ni msuwaki wa kiasili.

Kumbukumbu (memory):

Kunywa kijiko kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa na changanya na asali mara mbili kwa siku.

Utaratibu Wa Ulinzi Wa Mwili:

Kula kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa na asali mchana na usiku Kutoweza kuzuia haja ndogo (mkojo): Kunywa kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa pamoja na asali, kisha kunywa maji ya vugu vugu.

Jaundice:

Tumia Habbat-Sawdaa pamoja na maziwa.
Maumivu Sugu ya kichwa (Maumivu ya kichwa ya upande mmoja, maumivu ya kichwa):
Kaanga Habbat-Sawdaa na iweke katika kitambaa cha pamba, funga au weka tu kitambaa katika kikomo (kipaji cha uso). Roweka Habbat-Sawdaa ndani ya siki wakati wa usiku, siku ya pili ivuruge kufanya unga. Ingiza katika pua halafu vuta pumzi.

Ngozi kavu:

Changanya asali pamoja na robo kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.

Upepo:

Changanya asali pamoja na robo kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.

Minyoo:

Kunywa Habbat-Sawdaa pamoja na siki kuondoa minyoo

Kunyonyoka Nywele:

Ataukanda unga wa Habbat-Sawdaa katika juisi ya chirichiri pamoja na kijiko cha siki nyepesi na kikombe cha mafuta ya zeituni, halafu asugue kichwani kwa mafuta hayo kila siku jioni pamoja na kukiosha kichwa kwa maji na sabuni kabla ya kupaka.

Maumivu ya Kichwa:

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa , karafuu iliosagwa nusu ya kiwango cha Habbat-Sawdaa na anisuni (anise), halafu achanganye pamoja. Achukue kiasi cha kijiko kimoja (cha chai), wakati wa kuumwa na kichwa, na ale na maziwa lala (mala), pamoja na kupasugua mahala paumapo kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa .

Ukosefu Wa Usingizi:

Atachukua kijiko cha Habbat-Sawdaa , achanganye na gilasi ya maziwa moto yaliochanganywa na asali, baada ya kupoa kiasi atakunywa.

Chawa Na Mayai Yake:

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa uliosagwa vizuri aukande kwenye siki mpaka uwe kama marhamu, halafu ajipake kichwani &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; baada ya kunyoa nywele au kuisugua marhamu kwenye mashina ya nywele, halafu aketi katika mwanga wa jua kitambo cha robo-saa. Na hataosha kichwa ela baada ya masaa matano. Atafanya hivyo kila siku kwa muda wa wiki moja.

Kisunzi Na Maumivu Ya Sikio:

Tone moja la mafuta ya Habbat-Sawdaa ndani ya sikio husafisha sikio, pamoja na kuyanywa na kusugua sehemu za panda na nyuma ya kichwa, humaliza kisunzi.

Upaa Na Mabaka:

Utachukua kijiko cha unga wa Habbat-Sawdaa, siki kiasi cha kikombe kimoja na juisi ya kitunguu saumu kiasi cha kijiko kidogo, vyote hivyo utavichanganya na vitakua namna ya marhamu, utajipaka baada ya kunyoa sehemu ya nywele na kuchanja kidogo &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; kisha utafunga bendeji, utaiacha mpaka asubuhi, baadae utajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa,utaendelea hivyo kwa muda wa wiki moja.

Malengelenge ya Neva katika Ngozi:

Atajipaka &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; sehemu ya malengelenge &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; mafuta ya Habbat-Sawdaa mara tatu kila siku mpaka iondoke kwa Uwezo wa Allah.

Maradhi Ya Wanawake Na Uzazi:

Dawa kubwa inayosahilisha kuzaa ni Habbat-Sawdaa iliochemshwa ikachanganywa na asali na kiziduo cha babunaji (chamomile). H abat sawdaa ni kama burashi katika uke wa mwanamke yenye faida kubwa kwao pamoja na kutumua mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kila kinywaji cha moto kwa maradhi yote ya wanawake.

Meno Na Maumivu Ya Mafido na Koo:

Kiziduo cha Habbat-Sawdaa na kutumia kwa kusukutua kwa kugogomoa, husaidia mno maradhi yote ya mdomo na koo, vivyo hivyo pamoja na kubugia kijiko cha Habbat-Sawdaa na kumeza kwa maji yenye vuguvugu kila siku na kujipaka mafuta yake sehemu ya koo kwa nje na kuusugua ufizi kwa ndani.

Maradhi Ya Tezi:

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa na aukande kwa asali na mkate wa nyuki kila siku, kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Chunusi (Acne)

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa aukande katika mafuta ya ufuta (simsimu) pamoja na kijiko cha unga wa ngano. Vyote hivyo atajipaka usoni kuanzia jioni hadi asubuhi, halafu ataosha kwa maji yenye vuguvugu kwa sabuni. Ataendelea kufanya hivyo kwa muda wa wiki moja. Na awe akinywa mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kinywaji chochote cha moto.

Maradhi Yote ya Ngozi:

Atachukua mafuta ya Habbat-Sawdaa, mafuta ya waridi (marashi jabali) na unga wa ngano asili, vyote hivyo kwa viwango sawa, ule unga wa ngano uwe zaidi kuliko mafuta, halafu aukande vizuri. Kabla ya kujipaka, apanguse sehemu yenye ungonjwa kwa kitambaa kilichoroweshwa siki nyepesi, halafu aketi kwenye jua, baadae ajipake dawa hio kila siku. Lakini ajizuie na kila chenye kuchochea hisia kama vile, samaki, mayai, maembe na mfano wake.

Sugu (Chunjua) (Wart)

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa aukande katika siki nzito na asugue kwa kitambaa cha sufi au katani mahala pa sugu asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja.

Kuung`arisha Uso Na Kuurembesha

Ataukanda unga wa Habbat-Sawdaa katika mafuta ya zeituni, na atajipaka usoni halafu apigwe na mwanga wa jua kidogo. Tiba hiyo ataifanya wakati wowote katika mchana na siku yoyote.

Kuunganisha Mvunjiko Haraka

Supu ya adesi (dengu), kitunguu maji pamoja na yai la kuchemsha na kijiko kikubwa cha unga wa Habbat-Sawdaa , utachanganya na supu hiyo japo siku baada ya siku; halafu anywe. Na atasugua sehemu zilizo karibu na mvunjiko kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa, na baada ya kufungua bendeji atajisugua kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa yenye vuguvugu; kila siku.

Mvilio Wa Damu (Contusion)

Atachemsha vizuri konde moja la Habbat-Sawdaa katika chombo cha maji, kisha atakiingiza kiungo kilichovilia damu ndani ya maji hayo- yenye vuguvugu- kwa muda wa robo-saa au zaidi pamoja na kukitaharakisha kiungo hicho. Baada ya hapo atajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa bila ya kufunga kitu. Lakini hatakiwi kukipa uzito kiungo hicho au kukitaabisha. Tiba hiyo ataifanya kila siku kabla ya kulala.

Baridi Yabisi (Rheumatism)

Atachemsha mafuta ya Habbat-Sawdaa na atasugua kwayo ile sehemu yenye ugonjwa, atasugua kwa nguvu kama kwamba yuwasugua mfupa wala sio ngozi! Na atayanywa baada ya kuyachemsha vyema na kuyachanganya na asali kidogo. Ataendelea na tiba hiyo huku akiwa ni mwenye imani na yakini kuwa Allah Atamponya.

Kisukari (Diabetes)

Utachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kikombe kimoja, manemane (myrrh) iliosagwa kiasi cha kijiko kikubwa, habbarrashad nusu kikombe, komamanga iliosagwa kiasi cha kikombe kimoja, mzizi wa kabichi uliosagwa baada ya kukaushwa kiasi cha kikombe kimoja na kijiko kidogo cha mvuje. Vyote hivyo atavichanganya na atakula kabla ya kula chakula kiasi cha kijiko kimoja, atakula na maziwa lala ili iwe rahisi kumeza.

Shinikizo la Damu (High Blood)

Kila unywapo kinywaji cha moto, tia matone machache ya mafuta ya Habbat-Sawdaa. Pia ujipake mafuta hayo mwili wote, japo wiki mara moja.

Uvimbe Wa Figo(Nephritis)

Atatengeneza kibandiko (cha kitambaa) kutokana na unga wa Habbat-Sawdaa uliokandwa katika mafuta ya zeituni, atabandika sehemu yenye maumivu ya figo pamoja na kubugia funda la kijiko cha Habbat-Sawdaa kila siku kabla ya kula chakula kwa muda wa wiki moja tu; uvimbe utakwisha insha Allah.

Kuvunjavunja Vijiwe Vya Tumboni:

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kikombe kimoja kisha aukande katika kikombe cha asali, na atasaga kitungu u saumu punje tatu; atakua akichukua nusu yake akila kabla ya kula chakula kila siku. Pia itakua bora lau atakula limau kila baada ya kula dawa; kwani husafisha kabisa.

Kukojoa Kwa Maumivu (Dysuria)

Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa juu ya kinena kabla ya kulala pamoja na kunywa kikombe cha mafuta hayo yaliochemshwa na kutiwa asali; kila siku kabla ya kulala.

Kukojoa Bila Kukusudia

Atachukua Habbat-Sawdaa na maganda ya mayai yaliosafishwa na yakaokwa na kusagwa halafu yakachanganywa na Habbat-Sawdaa kisha yakaokwa na kusagwa halafu yakachanganywa na Habbat-Sawdaa kisha aingize kwenye maziwa; hatimae anywe kiasi cha kikombe kimoja kila siku na wakati wowote.

Jongo (Edema)

Ataweka kibandiko (cha kitambaa) cha unga wa Habbat-Sawdaa uliokandwa katika siki juu ya kitovu, kwanza ataweka kitambaa. Pia atakula Habbat-Sawdaa kijiko kimoja asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja.

Kifuko Cha Nyongo Na Vijiwe Vyake:

Atachukua Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja, manemane iliosagwa robo kijiko na asali kiasi cha kikombe kimoja; vyote hivyo atavichanganya viwe mraba (kama jamu); halafu awe akila kila asubuhi na jioni.

Wengu:

Ataweka kibandiko (kilichopashwa moto) cha Habbat-Sawdaa iliokandwa katika mafuta ya zeti katika ubavu wa kushoto; jioni. Na wakati huo huo ata kunywa kikombe cha kiziduo cha uwatu kilichochanganywa asali na mafuta ya Habbat-Sawdaa kidogo, ataendalea na dawa hiyo kwa muda wa wiki mbili mfululizo.

Maradhi Yote ya Kifua na Baridi:

Atachukua mafuta ya Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kikubwa atie kwenye maji halafu ayaweke juu ya moto mpaka ianze kufuka moshi, hapo aanze kuuvuta ule moshi puani huku akiwa amejifunika kichwa ili ule moshi usiende upande mwingine. Atafanya hivyo kila siku kabla ya kulala, pamoja na kunywa kiziduo cha zaatari kilichochanganywa na unga wa Habbat-Sawdaa; asubuhi na jioni.

Moyo na Mzungukoa wa Damu:

Kuwa na imani katika maneno ya Mtume (Swalla Llahu 'alayhi wa sallam) Kwa sababu jambo hili ni katika muktadha wa imani. Mtume (Swalla Llahu 'alayhi wa sallam) alipotuambia kuwa Habbat-Sawdaa ni dawa ya kila ugonjwa, basi hakuna shaka hata chembe kuwa ni dawa ya maradhi yote yanayomfika mwanaaadamu. Mgonjwa wa moyo asikate tamaa kutokana na rehma ya Allah; ni juu yake akithirishe kutumia Habbat-Sawdaa kwa namna yoyote iwayo; iwe ni kwa kula nzima au kwa kunywa wakati wowote uwao.

Mchango (Msokoto Wa Tumbo) (Colic)

Atachemsha vyema anisuni, kamun na nana kwa vipimo sawa na atatia asali kidogo, halafu atie matone saba ya Habbat-Sawdaa ; atakunywa kinywaji hicho kikiwa na vuguvugu pamoja na kupaka mafuta ya Habbat-Sawdaa mahala panaposokota. Baada ya muda mchache maumivu yataondoka.

Kuhara:

Atachukua juisi ya chirichiri iliochanganywa na unga wa Habbat-Sawdaa kijiko kikumbwa, atakunywa kiasi cha kikombe kimoja mara tatu kwa siku.

Uziwi:

Atachemsha Habbat-Sawdaa pamoja na karafuu, na atakunywa bila ya kuongeza kitu; mara tatu kwa siku.

Gesi Na Maumivu:

Atabugia unga laini wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja kabla ya kula chakula akifwatisha gilasi ya maji yenye vuguvugu iliotiwa asali ya muwa kiasi cha vijiko vitatu; atakariri kila siku kwa muda wa wiki moja.

Asidi (Acidness)

Motone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa yaliotiwa kwenye maziwa ya moto na asali; humaliza asidi.

Uvimbe Wa Tumbo:

Atachukuwa unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja na kijiko cha urkusus (licorice) hivyo atavichanganya na juisi ya pea iliotengenezwa pamoja na kokwa zake; halafu anywe; ataona nafuu kubwa.

Maradhi Ya Macho:

Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa sehemu za panda kandokando ya macho na kope, atafanya hivyo kabla ya kulala pamoja na kunywa matone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kinywaji chochote cha moto au katika juisi ya karoti.

Amiba (Vijidudu) (Amebiasis)

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja pamoja na kijiko cha kitunguusaumu kilichosagwa, atachangana katika kikombe cha juisi ya nyanya iliotiwa chumvi kidogo; atakunywa kila siku kabla ya kula chakula kwa muda wa wiki mbili mfululizo.

Kichocho (Bilharziasis)

Atakula Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja asubuhi na jioni, yawezekana kuila Habbat-Sawdaa katika chakula kama vile mkate pamoja na kujipaka mafuta yake katika ubavu wa kulia. Ataendelea na dawa hio kwa muda wa miezi mitatu mfululizo. Baadae atapata nguvu na nishati.

Kutoa Wadudu Tumboni:

Atakula sandwichi moto ya vitu hivi: kijiko kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa, punje tatu za vitunguu, kijiko kimoja cha mafuta ya zeti, pilipilimanga kidogo na punje kumi za boga (calabash), asubuhi atakunywa kinywaji cha shimari au mafuta ya mbono mara moja pekee.

Utasa:

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa, unga wa uwatu na mbegu ya figili kwa vipimo sawa, atakula kijiko kimoja asubuhi na jioni ilihali imekorogwa katika nusu kikombe cha asali, baadae atafuatisha kunywa kikombe kikubwa cha maziwa ya ngamia; basi inshaAllaah itakuwa kheri.

Tezikibofu (Prostate gland)

Atajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa chini ya mgongo na atajipaka chini ya korodani (mapumbu) na kusugua kwa mzunguko pamoja na kula unga wa Habbat-Sawdaa kijiko kimoja, na robo kijiko kidogo cha manemane katika nusu gilasi ya asali iliotiwa katika maji yenye vuguvugu; kila siku na wakati wowote apendao.

Pumu (Asthma)

Atanusa moshi wa mafuta a Habbat-Sawdaa asubuhi na jioni. Pia atakula unga wake asubuhi na jioni kabla ya kula chakula kila siku na pia kujipaka mafuta yake kifuani na kooni kabla ya kulala kila siku.

Kidonda:

Atayachanganya matone kumi ya mafuta ya Habbat-Sawdaa, katika kikombe cha asali na kijiko kimoja cha maganda ya komamanga yaliyokaushwa na kusagwa. Atakula kila siku kabla ya kula chakula; baadae atakunywa gilasi ya maziwa yasiyotiwa chochote.

Saratani (Cancer)

Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa mara tatu kila siku na kula kijiko cha unga wake kila amalizapo kula katika kikombe cha juisi ya karoti. Ataendelea hivyo kwa muda wa miezi mitatu.

Nguvu Za Kiume:

Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja achanganye (apige) ndani ya mayai saba ya kienyeji kisha anywe; atafanya hivyo siku baada siku kwa muda wa mwezi mmoja. Basi hata kama ana miaka 120 atapata nguvu za barobaro!

Udhaifu kwa Ujumla:

Atachukua unga wa habat sosa kiasi cha kikombe kimoja, uwatu mfano wake na ambari ilioyeyushwa kiasi cha kijiko kidogo, vyote atavichanganya katika chombo chenye asali iwe kama jamu; halafu awe akila kama jamu kila siku na wakati wowote apendao lakini kwa mkate wa ngano asili.
Kabla ya kuanza kula, jipatie Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kidogo na uitafune kwa meno yako, na unywe maji ya kawaida yaliochanganywa na siki kidogo.

Kutibu Ulegevu Na Uvivu:

Atakunywa- kabla ya kula &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; juisi ya machungwa iliochanganywa matone kumi ya mafuta ya Habbat-Sawdaa. Ataendelea hivyo kwa muda wa siku kumi. Baada ya hapo ataona nishati na uchangamfu.

Nishati akilini Na Wepesi Wa Kuhifadhi:

Atachemsha nanaa (mint leaf), aichanganye na asali na aingize matone saba ya mafuta ya Habbat-Sawdaa; anywe kinywaji hiki kikiwa na vuguvugu wakati wowote apendao. Basi ataionea namna fahamu itakavofanya kazi



Dawa hii HABBA SOUDA kwa kiingereza inaitwa (Nigella Sativa seed ) picha hii

BLACK SEED BENEFITS.jpg


 
Kuamsha tamaa ya kiume au kike
Juisi ya tangawizi nusu kijiko pamoja na yai nusu iliochemshwa na asali. Tumia kila siku kwa muda wa mwezi mmoja.



Dawa ya Ugonjwa wa kipindupindu

mtu kama ana ugonjwa wa kipindupindu atengeneze juisi ya kitunguu thaumu kisha anywe mgonjwa kikombe kimoja asubuhi na kimoja jioni basi kwa uwezo wa Allah atapona


kuondoa vijiwe Tumboni

Kunywa juisi ya mananasi kila siku kwa muda wa siku kumi na tano au mwezi mmoja Inshaallah kwa uwezo wa Allah vijiwe vitaondoka


Dawa Ya Tumbo Na Kutapika

Chukuwa Komamanga kali Kata Vipande Vipande Pamoja Na Maganda Yake Chemsha Mpaka Iwe Kama Shira Mpe Mngonjwa Kijiko Kidogo Anywe Inshaallah Mwenyezi Mungu Atamponesha Amina


Ugonjwa wa uchovu wa mwili (sluggishness and laziness)

Tumia kijiko kimoja cha mafuta ya habba sauda pamoja na glasi moja ya maji ya machungwa changanya pamoja kunywa kila siku asubuhi kwa muda wa siku kumi (10) utaona mabadiliko yake.


 
mzizimkavu nimekusoma sana ila tatizo ni majina ya miti inasumbua sana maana sijui ni kwa kilugha au ni kiswahili maana nimetoka kapa kwenye majina ya miti (dawa) naomba kama unaweza tuelezea kwa njia nyingine kama unapost hata picha yake yaweza saidia zaidia
 
mzizimkavu nimekusoma sana ila tatizo ni majina ya miti inasumbua sana maana sijui ni kwa kilugha au ni kiswahili maana nimetoka kapa kwenye majina ya miti (dawa) naomba kama unaweza tuelezea kwa njia nyingine kama unapost hata picha yake yaweza saidia zaidia
Mkuu@Mwanaweja kila kitu nimeweka wazi kwa kiswahili na kiingereza wewe kama kuna kitu kinakushinda kopi uniwekee hapo uliza huu mti unaitwaje kwa lugha ya

kiingereza na kiswahili? Dawa hizo zinapatika kwenye maduka ya wauza Dawa za kiarabu hapo karibu na Sokoni kariakoo wapemba nenda kaulize utazipata mkuu nimetowa elim yangu hapo wewe kazi yako ni kukopi kisha ukaulizie karibu na maeneo ya kariakoo Sokoni utazipata hizi dawa.
 
Duh, hili ni somo kubwa sana. Ingawa nimewahi kuwa
medical personnel kabla sijaacha na kufanya kazi nyingine
lakini nikiri kuwa hapa nimepata mambo mengi niliyokuwa
siyajui. Nimelazimika kuyakopi ili niyasome baadaye taratibu...
 
Mimi Ninakupa Dawa ya Bahati jaribu kupata Majani ya mkunazi uyaweke nyumbani kwako sehemu ya kivuli ndani ya nyumba yako mpaka yakauke kisha uyatwange hayo

majani ya mkunazi kisha uchanganye na maji uwe yale maji yake kila unapotaka kutoka nje ya nyumba yako jipake mwilini mwako pamoja na usoni kwa manuwizo yako kisha utoke nje nenda na shughuli zako ukafanye uyatakao utaona bahati ikikujia kila upande kwa baraka ya huo mti wa peponi mkunazi.. Fanya hiyo kwa muda wa kama mwezi kisha unipe feedback.
Mkunazi unaitwaje scientific.naona hii ipo kiimani zaidi
 
Back
Top Bottom