Mara ya Nne leo nalishwa na Mungu. Miujiza na Mungu yupo

Kutokana na changamoto wakati mwingine unajikuta upo kazini mambo hayajakaa sawa hata pesa ya Lunch hamna.
Mara ya kwanza ilipotokea nilichukulia tu kuwa ni coincidence haikuwa na lolote jipya.

Ofisini kwangu nafanya kazi na raia wa nchi mbali mbali hasa za asia na kiarabu. Siku hiyo nimeenda kazini nina pesa ya nauli tu. Hata sikuweza kwenda na gari sometme mambo yanakuwa tight sana ndugu zangu. Basi mchana akaja dada mmoja mwenye asil ya kihindi akaniletea chakula toka kwao. Nikamshukuru sana. Nikala na kingine nikaenda nacho home.

Siku zikapita kuna siku tena ikatokea nipo majalala mchana hauelewek na njaa inauma sana.mida ya saa tano na nusu akaja dada mwingine akaleta msosi akaniwekea mezani pangu akaondoka. Nikamshukuru Mungu pia maana ulikuwa muujiza.

Siku nyingine ikatokea tena hivyo hivyo hali mbaya kiuchumi sina pesa ya kula. Akaja mama mmoja ambaye yeye anatokea nchi za kiarabu.ilikuwa siku moja baada ya Eid akanikabidhi mfuko mkubwa. Kuwa hiyo ni zawadi yangu ya sikukuu....maskini mpaka machoz yalikaribia kunitoka maana kiukweli sikuwa na pesa na nlikuwa na njaa mchana umekaribia sisi wengine tunakula mara tano kwa siku ukikosa chakula mchana unachanganyikiwa. Nikapiga msosi birian,nyama na makando kando mengine. Mwingine nikagawa kwa jamaa zangu na kidogo nikabeba.

Leo ndo imebidi niwashirikishe wenzangu kuwa miujiza ipo na Mungu anaweza walisha watu wake. Sina hili wala lile najua mchana ukifika sina pesa mfukoni sababu nliyokuwa nayo kuna mtu nlimpa kwa dharura. Mara nakuta mezani pangu ofisin pana mfuko. Nikaweka pembeni maana sikujua ni wa nani.nikaendelea kutumia computer yangu. Mara akaingia dada mmoja akanambia ule mfuko una lunch yangu maalum.nikachukua nikamshukuru Mungu.

Nashukuru kwa mambo haya ambayo kwa mtizamo wa kibinadamu ni kama madogo sana. Lakin ukitizama kwa undani unagundua ni mambo makubwa na si kwamba ni coincidence.
Hahaha! Duh..we jamaa ni nouma,unabofya mpakato then hela ya kula tizi?nafikili akija masikini hapa kutoa na yeye ya moyoni mpaka tutajikuta tunamchangia,ila kwa wewe jamaa endelea kuletewa lunch
 
Mkuu Chizi Maarifa nimekuelewa sana.
Ila nilichojifunza humu ni kwamba madogo wengi hawajui changamoto za maisha na wanadhani ukiwa na kazi unakuwa umemaliza. Kibaya zaidi wengine hata kazi hawana halafu wanajidai kuponda, heeheeeee kweli haya maajabu yako Tanzania tu.
Kiukweli hata mimi nimeshangaa sana.
Kuna watu hawana imani kabisa!
Binafsi nimeiamini hii habari 100% maana hata mimi hunitokea sana.
Alhamdulillah Mungu hajawahi kunitupa nikakosa namna
 
Siku yako ya kuliwa yaja ndipo utajua anayekulisha ni shetani si Mungu..!
 
Chizi Maarifa mimi nahisi ulishamnog'oneza mtu hapo ofisini kuhusu hali yako ya kifedha na mambo ya ujenzi. Watu kwa ustaarabu wao wanakusoma siku unapokuja mtupu sababu labda unapokuwa na pesa huwa unaaga kwenda kula au huwa wanakuona unakuja na chochote. Ukija mkono mtupu, wanapeana taarifa kisiri siri. Mungu anakuja kwa njia nyingi. "Nilikuwa na njaa, ukanilisha".
 
Bangi zingine bhana
****
sio bhang ndg huwa ni mambo ya ajabu sana..!/
Acha nihadisie ya kwangu niya kitambo kidogo..
***
wakati nasoma primary schools/ mzazi alinizoesha kunipa 500/-ya kula shuleni./ wakaja tokea wanoko gani wakaja mwambia mama unamzoesha mtoto tabia mbaya...!/
hakika kuanzia siku ile ni kushibishwa kwa sana asb./
lakini chaajabu wakati siku moja nacheza nyumbani kama ujuavyo Watoto na kuchezea michanga/
nikawa nafukua pahala kwa mikono!,hamadi pesa tele zikawepo pale,amini usiamini niliendelea kuchukua mia 500 kila siku mpa namaliza la saba/through automatic way sikutilia maanani kale kashimo / ile sight ikajanipotea kila nijaribu kuchimba puktyuuu hamna kitu.
 
Sasa mkuu ukiangalia tukio la jamaa yetu ni muujiza kweli?
 
Kutokana na changamoto wakati mwingine unajikuta upo kazini mambo hayajakaa sawa hata pesa ya Lunch hamna.
Mara ya kwanza ilipotokea nilichukulia tu kuwa ni coincidence haikuwa na lolote jipya.

Ofisini kwangu nafanya kazi na raia wa nchi mbali mbali hasa za asia na kiarabu. Siku hiyo nimeenda kazini nina pesa ya nauli tu. Hata sikuweza kwenda na gari sometme mambo yanakuwa tight sana ndugu zangu. Basi mchana akaja dada mmoja mwenye asil ya kihindi akaniletea chakula toka kwao. Nikamshukuru sana. Nikala na kingine nikaenda nacho home.

Siku zikapita kuna siku tena ikatokea nipo majalala mchana hauelewek na njaa inauma sana.mida ya saa tano na nusu akaja dada mwingine akaleta msosi akaniwekea mezani pangu akaondoka. Nikamshukuru Mungu pia maana ulikuwa muujiza.

Siku nyingine ikatokea tena hivyo hivyo hali mbaya kiuchumi sina pesa ya kula. Akaja mama mmoja ambaye yeye anatokea nchi za kiarabu.ilikuwa siku moja baada ya Eid akanikabidhi mfuko mkubwa. Kuwa hiyo ni zawadi yangu ya sikukuu....maskini mpaka machoz yalikaribia kunitoka maana kiukweli sikuwa na pesa na nlikuwa na njaa mchana umekaribia sisi wengine tunakula mara tano kwa siku ukikosa chakula mchana unachanganyikiwa. Nikapiga msosi birian,nyama na makando kando mengine. Mwingine nikagawa kwa jamaa zangu na kidogo nikabeba.

Leo ndo imebidi niwashirikishe wenzangu kuwa miujiza ipo na Mungu anaweza walisha watu wake. Sina hili wala lile najua mchana ukifika sina pesa mfukoni sababu nliyokuwa nayo kuna mtu nlimpa kwa dharura. Mara nakuta mezani pangu ofisin pana mfuko. Nikaweka pembeni maana sikujua ni wa nani.nikaendelea kutumia computer yangu. Mara akaingia dada mmoja akanambia ule mfuko una lunch yangu maalum.nikachukua nikamshukuru Mungu.

Nashukuru kwa mambo haya ambayo kwa mtizamo wa kibinadamu ni kama madogo sana. Lakin ukitizama kwa undani unagundua ni mambo makubwa na si kwamba ni coincidence.
..Udumu Kula shambani mwa Bwana Mkuu
 
waarabu?? usikute unalishwa na majini
Ahssannttee JJ, Jini huyo ndo tulo mtoa pangoni ulikuwa kama pimbi.... ukakimbilia mnazini tukakuteremsha na kukuvika kaptura ukafurahi ukaanza kunena Woo woo tchue thuu.. tukaulainisha ulimi ukajua kutamka "Kiswahili" !!
 
Na hii ndo shida kubwa ya JF ya miaka hii. kuna watoto wamemaliza kidato cha nne na wengine darasa la saba wapo humu. ukiwaeleza changamoto kama hizi hawazielew kwa sababu wengi wapo kwa wazazi. ni ngumu sana najua nlipokuwa mdogo nlikuwa pia simwelew mzee nikimwomba pesa akisema hana na wakati namwona ana drive n.k nasema anawezaje kusema hana halafu ana drive, anavaa anaenda kazini n.k but kuna siku tunakula wali na maharage na matembele tu. wakati hayo si mazoea. kumbe sometime anakosa then mama zile ambazo huwa zinabaki siku nyingine ndo anazitumia kununulia mahitaji nyumbani. huwa namkumbuka mama yangu kwa kuwa ni moja ya wanawake wenye akili. so mzee akitoa pesa ya chakula mama anafanya bajeti yake anabakiza nyingine za matumizi yake binafsi na nyingine kwa ajili ya dharura. sometime mzee anaweza rudi kachanganyikiwa kabisa hana kitu mambo hayajenda ok. but unakuta mama kesho ananunua kuku na kupika chakula kizuri wakati mzee analalamika kuwa biznez zake hazijaenda sawa week nzima.

haya mambo ni watu wazima wanaelewa. watoto hawawezi kuelewa. kuwa kuan kipindi ukizipata unajaza mafuta full tank kwenye gari kwa ajili ya dharura. then unatembea una tsh 30,000 tu kwenye wallet ambayo hiyo huitumii hata iweje week nzima unaenda na kurudi kazini una 30,000 kwenye wallet..unashinda na njaa but hiyo haitoki kwenye wallet.

Mkuu Chizi Maarifa nimekuelewa sana.
Ila nilichojifunza humu ni kwamba madogo wengi hawajui changamoto za maisha na wanadhani ukiwa na kazi unakuwa umemaliza. Kibaya zaidi wengine hata kazi hawana halafu wanajidai kuponda, heeheeeee kweli haya maajabu yako Tanzania tu.
 
Nashukuruni sana hata kwa comments za kebehi. Kila jambo lina sababu yake. Majini si tatizo kwangu. Hayanipi shida maana si kitu cha kuniogipesha. Yenyewe yanapaswa kuniogopa mimi. Mungu hutumia watu ambao hata hatuwadhanii. Kama unasoma Biblia utakumbuka habari ya Eliya aliyelishwa na Kunguru.

Kukosa pesa huwa inatokea hata kwa mtu anayepokea mamilion kuna kipindi Mungu anataka tu aonekane kwa namna yake kwa vitu vidogo.kwa maana neno la msalaba kwao wanaopotoea ni UPUUZI.1 wakor 6:18.

So nawaelewa ila nashukuru nimetimiza kushare nanyi hili jambo. Ukikaa ukafikiria kwa akili za kiroho kuna ujumbe mkubwa zaid ya huu unaouona. Mungu alimtumia mwanamke mjane wa Sareptha Kumlisha Eliya pia.

Anyway mimi si Eliya lakin nataka tu ujenge ufaham huo. Na pia kuondoa dhana chafu za sex wakat wote. Ukifikiria hivyo kila wakat utajikuta huna marafiki wa kike mnaoheshimiana maana we umeweka akilin sex tu
You are blessed...
Baraka za Mwenyeezzi Mungu huja kwa mifumo mbalimbali... Ubarikiwe sana,
Achana na wachangiaji wa JF wenye kejeri na kebehi.... wengi wao hawana Exposure!!
 
suala si rangi au race. Yesu alipewa maji na mwanamke MSAMARIA. Mungu anapotaka kufanya jambo hutumia vilivyo vinyonge kutenda makuu. so dini,rangi kabila si kitu. na mimi ni Mkristo but trust me hao ndio ambao nimekuwa nikishirikiana nao kwa ukaribu wakiwepo na wakristo wengine pia. Uarabu ,uhindi au uzungu wao has got nothing to do with me. mi nawaona kama ni viumbe vya Mungu. kuhusu jinsia zao hilo kwangu si tatizo pia na halikuwah kuwa tatizo. mi nafaham mchango mkubwa walio nao wanawake katika maisha. na hasa kuwasaidia watu au wenye shida kuliko wanaume.

na kwa bahati mbaya au nzuri sikulelewa yale maisha ya kuamini mwanamke akiwa kind kwako basi atakuwa anakutaka au anataka uwe na uhusiano naye wa kimapenzi. alas....thats not how i was raised by my parents ambao wanaamini kila mtu anapaswa aheshimiwe kwa kiwango kile kile ninachotaka mimi niheshimiwe.

kebehi au kashfa zinazokuwa posted after what i have said wala si shida kwangu. najua wengine wanafanya yale ambao baba yao aliyatenda huko nyuma kwa watu wa Mungu, mitume na manabii. but kwa hiki ambacho nimeandika ni kile ambcho ninaamini so silazimishi mtu aamini hivi ila nimeona kumshukuru Mungu au kutoa ushuhuda huu ni jambo jema pia. kitu ambacho ni wazi shetani asingependa maana anapenda aone mitandao siku zote itumike negatively.

Hapo kwenye neno waarabu badilisha andika wazungu...uone maajabu ya comments humu jf. Utashangaaa hutakosa "amein" kama 1000 hiv...!
Just try!
 
Back
Top Bottom