Elections 2010 Mapungufu ya sera ya elimu bure

Mtu Mmoja said:
1. enzi zile mwalimu nyerere anatoa elimu bure watz tulikuwa wangapi? na sasa tuko wangapi?
2. uchumi umeimarika kiasi gani?
3. vyanzo vingine (mbadala) vya mapato vina potential ya kutoa mapato kiasi gani?
4. maendedeleo katika sekta nyingine yanahitaji kiasi gani? au kila senti ianyokusanywa na serikali ipelekwe kugharimia elmu?
5. kiasi gni kitabaki kwa ajli ya sekta zingine muhimu kama maji, miundombinu, ulinzi nk?
6. nk

nadhani haya ndo yanayopaswa kujadiliwa ili kumsaidia mheshimiwa mbunge na jamii kwa ujumla na sio kumshambulia personally na chama chake. hayo mimi hayanisaidii chochote, hata kama wapiga kura wamechagua zezeta watajaza wenyewe na uchaguzi umekwisha.

lets discuss issues wazee

Mtu Mmoja,

..kwanza hakuna kitu kama "elimu bure" au "afya bure." huduma zote hizo kwa namna moja au nyingine zinagharimiwa na kodi wanazolipa wananchi, na vyanzo vingine vya mapato ya serikali.

..suala la "elimu bure" maana yake ni kuondoa michango na ada za shule ambazo zinatoka moja kwa moja mifukoni mwa wazazi.


..hoja kwamba wakati wa Mwalimu kulikuwa na wanafunzi wachache kuliko wakati huu haina uzito. pamoja na wanafunzi kuongezeka, walipa kodi nao wameongezeka, na serikali ya sasa hivi ina vyanzo vingi vya mapato kuliko wakati wa Mwalimu Nyerere. wakati wa utawala wa Mwalimu hatukuwa na migodi sita ya dhahabu kama ilivyo sasa hivi.

..kinachopaswa kufanyika ni kurudisha uzalendo na nidhamu ya matumizi serikalini. Mwalimu aliongoza nchi akiwa na baraza la mawaziri dogo kuliko hili la sasa hivi. tena mawaziri wake walikuwa na elimu ndogo kuliko hawa tulionao sasa hivi. kwa msingi huo hakuna sababu yoyote ile kwa serikali ya JK kushindwa ku-deliver kulingana na matarajio ya wa-Tanzania.


..Tanzania sasa hivi tumo katika 5 bora ya wazalishaji wa dhahabu. sielewi kwanini elimu yetu ni gharama[ya kulipia], na kiwango cha chini, kuliko jirani zetu wa Kenya na Uganda, ambao hawajabarikiwa kuwa na rasilimali kulinganisha na sisi.

..kama Kenya na Uganda wameweza , kwanini Tanzania tushindwe?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom