Elections 2010 Mapungufu ya sera ya elimu bure

..Uganda walikuwa wanatoa elimu bure toka msingi mpaka o-level. majuzi Museveni kaongeza na a-levels.

..suala hili litahitaji pesa nyingi. lakini badala ya kulipinga wazo hili 100% labda tungeanza kutoa elimu ya chuo kikuu bure.

..vilevile ni lazima kuongeza bajeti ya elimu ili kuboresha viwango, manaake sasa hivi kinachotolewa siyo elimu bali ni uozo tu.

Kwa nini waTanzania mnakazia sana kuonhelea matumizi, hamuongelei kuongeza uwezo (mapato) wa nchi na Wananchi wake kiuchumi... this to me is the only solution for our nation.
 
Kasheshe said:
Kwa nini waTanzania mnakazia sana kuonhelea matumizi, hamuongelei kuongeza uwezo (mapato) wa nchi na Wananchi wake kiuchumi... this to me is the only solution for our nation.

Kasheshe,

..kuna wachangiaji kama wewe wanadai hakuna pesa[uwezo] za kutoa huduma ya elimu bure. halafu wako wengine wanadai pesa[uwezo] zipo isipokuwa zinatumika kwa mambo ya anasa za JK na viongozi wenzake. zaidi, wapo wanaodai kwamba idea ya kutoa huduma ya elimu bure ni uwendawazimu na haipaswi hata kufikiriwa.

..jinsi siku zinavyokwenda ukweli unajibainisha kwamba hii idea ya "free education" siyo jambo la kiuendawazimu kama walivyokuwa wakidai JK,Kinana, Sitta, etc etc. mataifa mengi makubwa mfano Marekani yanatoa elimu kwa vijana wao. hata majirani zetu wa Afrika Mashariki kama Kenya na Uganda wanatoa elimu bure.

..binafsi nadhani tuache ubishi usio na tija, na kama taifa tujiwekee lengo na kuanzisha mchakato wa kutoa elimu bure kwa vijana wetu. ndani ya mchakato huo ndipo zitakapoibuka ideas za kuongeza mapato, kupunguza matumizi, kupanua uwigo wa kodi, etc etc. pia kutaibuka hoja kwamba lengo letu na kutoa huduma ya elimu bure ni lazima liende sambamba na kuhakikisha viwango vya elimu inayotolewa haviathiriki.

..vilevile tukitoa elimu bora kwa wananchi wengi zaidi, ndivyo tunavyowazesha kuwa na uwezo wa kumudu maisha yao, kuongeza tija ktk uzalishaji na pato la taifa.

..TATIZO NINALOLIONA NI KWAMBA JK NA VIONGOZI WA CCM WANAZUNGUMZIA SUALA LA ELIMU KAMA VILE NI KERO KWAO. TUCHUKULIE SUALA LA UTOAJI ELIMU KAMA UWEKEZAJI FOR THE FUTURE OF OUR NATION.
 
ndugu si vibaya nikiwadokeza namna nilivyofanikiwa katika uchaguzi huu na nilivyopangua hoja za wapinzani wa CCM jimboni. leo nitaanza na sera ya elimu bure kama ilivyonadia na chadema.

mimi nilinadi sera ya elimu nafuu na yenye wigo mpana kama inavyotekelezwa na CCM kupitia dhana maarufu ya wananchi kuchangia gharama za elimu.

mapungufu ya elimu ya bure niliyoyaanisha na yakaeleweka kwa wapiga kura ni pamoja na:

1. kupunguza idadi ya watakaopata elimu na kufanya mtoto kuchaguliwa kwenda sekondari kuwa sawa na bahati kama ilivyokuwa zamani. hii ni kwa sababu asilimia 20 ya bajeti ya nchi inakwenda kwenye elimu na kama wanachi hawatachangia baadhi ya gharama, basi uwezo wa serikali kusomesha watazania hautatosha kwa levels zote za elimu. niliweka wazi kwa uwezo wa elimu kutollewa bure upo hata sasa ila hofu ni kuwa idadi ya wanafunzi wanodahiliwa itapungua mwaka hadi mwaka hata kama fedha za elimu hazitakutana na wabadhirifu.

niliongeza kuwa uzuri wa elimu ya kuchangia ni kutoa fursa nyingi zaidi za elimu ata kwa wasio na uwezo kabia amabo wanakopa na kurejesha wakishamaliza elimu/mafunzo na kuajiriwa. inapendeza hasa ukizingatia kwamab wanarudisha katika muda mrefu kuliko mkopo wa kawaida unaotolewa na taasisi za fedha na ni baaada tu ya kupata lazi ya uhakika.

kupitia sera ya kuchangia elimu, sekta ya elimu imepanuka katika ngazi zote kuanzia elimu yaawali, msingi, sekondari, ufundi stadi hadi ile ya juu. mfano hai ni kutapakaa vyuo vikuu nchi nzima tofauti na ilivyokuwa zamani amabapo vyo vikuu vilikuwa UDSM na SUA pekee. pia vyuo vinavyotoa elimu ya juu navyo vimeongezeka na kutapakaa nchi nzima

ubora wa elimu unategemea bidii na uwezo wa mwanafunzi. kama mwanafunzi ataenda kucheza chuoni, basi hata kama ungempeeka kusoma ng'ambo anaweza kurejea na cheti lakini bila elimu.

hayo ni machache tu kati ya mengi niliyonadi kpinga sera ya elimu bure ya chadema. nshukuru nilieleweka na nilishinda bila kuchakachua

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Kwani Uganda na Kenya wana muujiza gani wao watoe elimu ya bure lakini sisi tusiweze.

Maoni yako haya yanaonyesha mapungufu makubwa sana katika uwezo wako kiuongozi.
 
Mbunge wa CCM,
Mkuu wangu nadhani wewe umechaguliwa kuwa mbunge kwa sababu nyingine na sio hoja zako kwani sielewi kabisa ulichokiandika hapo. Unasema bajeti ya serikali ktk elimu ni asilimia 20 na inahitaji mchango wa wananchi pasipo mchango wao serikali haiwezi kugharamia elimu ktk level zote..

Je, asilimia hiyo ikiongezeka hadi asilimia 25 kutokana na kupungua posho na chai zenu, kupunguza baraza la mawaziri na kikubwa zaidi viongozi wote wa serikali kuanza kulijilipia gharama za maisha badala ya serikali kuwalipa mishahara minono kisha kuendelea kuchukua dhamana ya gharama zote za maisha yao kwa ujumla.

Na umesha piga hesabu ya fedha ambazo serikali huwalipa walimu hewa na matumizi mengine yasiyohusiana na elimu wakati wizara inapofanya matumizi yake?..Hata shule zilizojengwa zimejengwa kwa nguvu ya wananchi lakini mmevuta mabillioni toka kwa wafadhili hizo fedha zimetumika wapi ikiwa shule zilijengwa na wananchi pasipo kulipwa isipokuwa kuwapunguzia wao muda wa uzalishaji..

Mkuu wangu ni rahisi kabisa elimu ya msingi hadi sekondari kupatikana bure ikiwa Mh.Sitta pekee yake anasomesha watoto 200 - BURE, yeye akiwalipia ada kila mwaka na kuwatunza kama wanawe kwa mshahara na posho alokuwa akipewa.. kwa nini dhamana hiyo isiwe ya serikali badala yake itolewe na mtu binafsi ambaye sii mfanyabiashara wala tajiri anayemiliki mamillioni ya fedha... Hivi kweli nyie Viongozi hamuoni aibu kuwa huo Ubunge wenu unawapa nguvu ya kuepeleka maendeleo vijijini mwenu kwa kutumia fedha mnazochuma! kutumia nafasi hii kununua kura za wananchi hali uwakilishi wenu upo bungeni ambako ndiko fedha hutoka na sii mifukoni mwenu..

Kisha yaonyesha wazi unashindwa kabisa kuelewa nini maana ya elimu bure. Kinachozungumziwa hapa ni serikali kutoa elimu bure ktk shule zake (public schools) na sii shule za Private. Sasa ningekuomba utueleze kwa ufasaha zaidi huko kuchangia kwa wananchi kumewezeshaje ujenzi wa shule nyingine nyingi zaidi ya UDSM na SUA, ni kiasi gani cha michango ya wananchi kimepelekea ujenzi wa hizo shule nyingine. Pengine itakuwa vizuri zaidi ukituambia ni kiasi gani cha fedha serikali hukusanya kutokana na ada hizo kila mwaka na hutumika vipi ili tupate picha halisi ya madai yako.
 
Naona sera zako hazina mashiko kabisa. Kama hao wananchi walikupenda kwa sababu ya sera hizo basi wamekula hasara kabisa. Mimi naamini kabisa elimu bure Tanzania inawezekana kama serikali ikiamua kufanya hivyo. Huyu mwananchi unayemchangisha wewe analipa michango mingine lukuki in all walks of life.

Huo mtazamo wa kuwa Tanzania ni nchi masikini ni mtazamo potofu kabisa na ni wakuwanyonya wananchi. Utakukuta kiongozi anahuburi umaskini wa Tanzania wakati yeye mwenyewe kajilimbikizia mali kibao na anaendelea kula raha na anasa kwa kwenda mbele.

Yaelekea wewe ulitafuta ubunge kwa ajili tu ya kujinufaisha wewe na familia yako. Siku moja hao wananchi unaowadanganya kwa sera potofu watakuja kuamka.
 
kama hiki ndo kiwango cha kujenga hoja na kujieleza walichonacho wabunge wa ccm, then waanze kutafuta biashara ya kufanya baada ya 2015.
 
mi naona wenzangu badala ya kujadili hoja mnaleta malalmiko juu ya viongozi wa CCM, kuhusu kuongeza mapato kama alivyosema kasheshe, mi naona itawezakana lakini kwa muda filani na si kwa papo kwa hapo kama wanachadema wanvyoamini
 
Kama aina hii ya wabunge ndiyo CCM imechakachua na kutupelekea Bungeni tumekwisha; natamani sana kumfahamu mbunge huyu ambaye kwa kila vipimo ameonyesha ni zezeta na atakuwa mzigo mzito kwa waliompigia kura (kama hakuchakachua) Bungeni. Nashauri CHADEMA wafanye juhudi kum - identify ili Operesheni Sangara ipelekwe jimboni kwake kuwazindua waliomchagua kwa bahati mbaya kwamba walikosea sana, kisha tukutane 2015 na kuona kama atarudi kusinzia Bungeni.
Mimi naamini kwa mtindo huu mwaka 2015 CCM itakuwa chama pinzani Bungeni kikiwa na wabunge wachache kabisaaa....
 
Kama kweli wewe ni mbunge, na huo ndiyo uwezo wako wa kufikiri, for sure you need six of you to make one John Mnyika. Nikupe tu siri kuwa viongozi wa CCM waliokuwa wanapinga kuwa sera ya elimu bure haiwezekani, ndani ya nafsi zao walijua kuwa inawezekana, sema walikuwa wanatunza heshima ya chama. Sasa kama wewe unataka kuwaamini kuwa elimu bure haiwezekani, jua kwamba you will not make any litle representative.

Take my words; Kama huo ndio uwezo wako wa kufikiri, next time hutakuwepo bungeni. shukuru sana ignorance wa wananchi wa jimbo lako kwa sasa...
 
Fisi maji weeeeeeeeeeeeeeeee, hata hicho kidogo cha kuchangia wananchi wanacho ungekijuliza wengine hata kula ni shida .
 
Huyu ni mbunge gani!?? Wa jimbo lipi??
Nashukuru si wajimbo langu kwani mimi ni wachadema!
 
ndugu si vibaya nikiwadokeza namna nilivyofanikiwa katika uchaguzi huu na nilivyopangua hoja za wapinzani wa CCM jimboni. leo nitaanza na sera ya elimu bure kama ilivyonadia na chadema.

mimi nilinadi sera ya elimu nafuu na yenye wigo mpana kama inavyotekelezwa na CCM kupitia dhana maarufu ya wananchi kuchangia gharama za elimu.

mapungufu ya elimu ya bure niliyoyaanisha na yakaeleweka kwa wapiga kura ni pamoja na:

1. kupunguza idadi ya watakaopata elimu na kufanya mtoto kuchaguliwa kwenda sekondari kuwa sawa na bahati kama ilivyokuwa zamani. hii ni kwa sababu asilimia 20 ya bajeti ya nchi inakwenda kwenye elimu na kama wanachi hawatachangia baadhi ya gharama, basi uwezo wa serikali kusomesha watazania hautatosha kwa levels zote za elimu. niliweka wazi kwa uwezo wa elimu kutollewa bure upo hata sasa ila hofu ni kuwa idadi ya wanafunzi wanodahiliwa itapungua mwaka hadi mwaka hata kama fedha za elimu hazitakutana na wabadhirifu.

niliongeza kuwa uzuri wa elimu ya kuchangia ni kutoa fursa nyingi zaidi za elimu ata kwa wasio na uwezo kabia amabo wanakopa na kurejesha wakishamaliza elimu/mafunzo na kuajiriwa. inapendeza hasa ukizingatia kwamab wanarudisha katika muda mrefu kuliko mkopo wa kawaida unaotolewa na taasisi za fedha na ni baaada tu ya kupata lazi ya uhakika.

kupitia sera ya kuchangia elimu, sekta ya elimu imepanuka katika ngazi zote kuanzia elimu yaawali, msingi, sekondari, ufundi stadi hadi ile ya juu. mfano hai ni kutapakaa vyuo vikuu nchi nzima tofauti na ilivyokuwa zamani amabapo vyo vikuu vilikuwa UDSM na SUA pekee. pia vyuo vinavyotoa elimu ya juu navyo vimeongezeka na kutapakaa nchi nzima

ubora wa elimu unategemea bidii na uwezo wa mwanafunzi. kama mwanafunzi ataenda kucheza chuoni, basi hata kama ungempeeka kusoma ng'ambo anaweza kurejea na cheti lakini bila elimu.

hayo ni machache tu kati ya mengi niliyonadi kpinga sera ya elimu bure ya chadema. nshukuru nilieleweka na nilishinda bila kuchakachua

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
nina wasi wasi sana na huo UDAKTARI WAKO mkuu!.....
pole sana
 
japo sijaaapishwa, tayari niko kazini na kwa sasa nafanya kazi ya kuteua kamati za kunisaidia kufuatilia shughuli za maendeleo jimboni ikiwa ni pamoja na kupanga mikakati ya kutafuta fedha za maendeleo kwa kuanzia na usambazaji wa maji ya bomba jimbo zima katika miaka mitano ijayo.

yaani baada ya ushundi huu, nimeanza rasmi kampeni ya uchaguzi mkuu wa 2015 kwa matendo. wapinzani wasahau kabisa kushinda hapa jimboni

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

ulishinda kwa halali au kwa kuchakachua?na ni jimbo gani hilo?
 
Siku zote ulikuwa wapi? Watu tumesambaza vitabu shule zaidi ya mia na wala si wabunge na hatuutaki huo ubunge. Hivyo basi mm siku zote nawaona watu wa aina yako ni matapeli wanaofikiri maendeleo yatakuja iwapo wao watakuwa wabunge. Kumbuka ww si wa kwanza kufikiri namna hii na matokeo tunayajua kwa waliokutangulia
Asenti
 
Mbunge wa CCM,

Kama alivosema Mkandara huo ubunge utakuwa hukuupata kwa kupangua hoja, bali kuna mengine yaliyojificha nyuma ya pazia ambayo wewe binafsi unayajua na ndio pekee mwenye uwezo wa kuyatolea maelezo.

Suala la kusema elimu ya bure haiwezekani ukaweka nukta, ukisimama mbele ya watu wenye akili timamu watakuona taahira tu. Uwezo wa serikali kugharamikia kitu unategemea mapato yake. Sasa nikionancho ni serikali ya chama chako kuishiwa fikra za kuongeza mapato yake au kupangilia vyema hata yale mapato kidogo inayoyapata hivi sasa. Hapo ndio tatizo linapoanzia. Hakuna miujiza..it is simple common sense.
 
1. enzi zile mwalimu nyerere anatoa elimu bure watz tulikuwa wangapi? na sasa tuko wangapi?
2. uchumi umeimarika kiasi gani?
3. vyanzo vingine (mbadala) vya mapato vina potential ya kutoa mapato kiasi gani?
4. maendedeleo katika sekta nyingine yanahitaji kiasi gani? au kila senti ianyokusanywa na serikali ipelekwe kugharimia elmu?
5. kiasi gni kitabaki kwa ajli ya sekta zingine muhimu kama maji, miundombinu, ulinzi nk?
6. nk

nadhani haya ndo yanayopaswa kujadiliwa ili kumsaidia mheshimiwa mbunge na jamii kwa ujumla na sio kumshambulia personally na chama chake. hayo mimi hayanisaidii chochote, hata kama wapiga kura wamechagua zezeta watajaza wenyewe na uchaguzi umekwisha.

lets discuss issues wazee
 
Back
Top Bottom