Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim!

Zumbemkuu nimekubaliana nawe.
Alisema wakati madakatari walipogoma alikaa kimya akaenda Davos kula kuku. Waliporejea kazini akijitokeza na kusema atahakikisha mgomo hautatokea tena. Leo hii tunashuhudia chini ya wiki mbili baada ya kauli hiyo wamegoma na yuko kimya. Sijui anajiandaa kwenda kula kuku tena wapi!!!

Vile yuko kaskazini lazima atinge Bilila Kempiski(sijui na yenyewe ishakuwa Hyatt)

006980-10-exterior-pool-sunset.jpg
 
Sidhani kama ana huruma, mimi naona ni kiburi, huwa hashauriki hasa kwa mambo sensitive yanayohusu nchi. Ni mtu wa kupokea tuu ushauri kutoka kwa wasaidizi wake matokeo yake nchi inaendeshwa kwa majungu na visasi. Kwa maana nyingine hana uwezo wa kutoa maamuzi.

Mfano mzuri badala ya kutumia bongo kuongoza na kukuza uchumi kwa kutumia rasilimali tulizokuwa nazo yeye anaamini kuwa omba omba kwa mataifa ya nje ndiyo uchumi utakuwa.

Kwa kweli matarajio yangu kwake yamekwisha kabisa.
 
Mapungufu ya Kikwete unaweza kuyatambua haraka sana hasa ukimlinganisha na urais wa Mkapa. Kwanza, Kikwete ni mtu aliyetamani sana kwenda Ikulu. Na Mwalimu alionya kwamba ukiona mtu ana uchu wa kupitiliza kuwa rais hyo tu inapaswa kuwa signal kwa wapiga kuara kuwa huyo mtu hatufai kama kiongozi na ni wa kuogopa kama ukoma. Sasa sijui sisi wabongo tunamuenzi vipi Nyerere ikiwa hata maonyo yake ya msingi tuliyapuuza 2005 na tukayapuuza tena 2010.

Pili, kama ambavyo wengine wameshasema, Kikwete ana popstar mentality hivi. Hauchukulii urais kama kazi ya kihistoria ya kubadilisha maisha ya watanzania. Yeye kwake ni bora liende -- "Nyerere alianza hakuyamaliza, Mwinyi akaja hakuayamaliza, Mkapa akapita hakuyamaliza na hata yeye watu wasitegemee kwamba mimi nitayamaliza".

Tatu, tofauti na Mkapa, Kikwete hana kipaji cha kupanga timu nzuri ya wasaidizi yenye kuleta matokeo bora kiuchumi na kimaendeleo. Namba mbili wake kwa awamu zote ni bogus, Lowassa ni fisadi aliyekubuhu, Pinda amepinda balaa. Kule Ikulu yupo Wassira na Lukuvi, astagafirulahi! Mwenye auheni katika timu yake ni Magufuli tu, na ukijaribu kuchunguza sana, Magufuli alisajiliwa na Mkapa.
 
Duh!
Siamini kama na wewe Pasco unanunua huo utumbo...
Kwa mara ya kwanza nimeanza kuelewa mjadala wako na MTM..



Ok, sawa "JK ameangushwa"
sasa itasaidia nini sisi kuorodhesha mapufu yake hapa??
Sababu hao "watendaji" aliowategemea ni bado anawategemea....
Kwa maana yako ni kuwa JK yupo chini kaanguka na hatoamka sababu bado yupo na watendaji walewale...
Haitafaa kitu kwa miaka hii 3 iliyobaki.

Mkuu tegemea maafa zaidi ya haya kwa miaka mitatu ijayo
Maana hakuna litakalofanyika na wala tusitegemee lolote kuwa bora chini ya watu waliopo hapa kwa sasa
 
JK hakujiandaa yeye binafsi kuwa rais wa Tanzania, bali aliandaliwa na wana-mtandao ambao nao walijiandaa kuja kukwapua mara baada ya kumuweka ikulu.JK alizidiwa kwa mbali sana na wakuu wa mtandao RA na EL, WOTE HAWA LEO HAWANA shida naye tena. RA tayari ameshatoka kwenye chama na hivyo tracing ya his where about is too remote.EL yeye amejikusanyia njugu za kutosha kuhakikisha anatinga magogoni at any cost.

JK kaachwa hana pa kushika kila kitu anaona mzigo kwani hata washauri wake ni wanamtandao waliowekwa na RA na EL na hivyo hawako kwa maslahi ya JK
 
Kaka, I really buy your comments!!!!!!!!!!!!!!! This government headed by this guy is like a bunch of commedians, I can not see anyone and anywhere within this government who can act diligently for the benefits of the nation............. Wote wamepotea na wamepoteza ujasiri hakuna hata mwenye mark ya uzalendo, tunakwenda wapi ndugu zangu. Mbaya zaidi mkulu wao ndo haeleweki haeleweki, kwa mtu mwenye akili timamu huwezi kumteua mtu akusaidie kuongoza then anakudiappoint unalalamika badala ya kuact accordingly..... Haina jipya huyu jamaa na hana la kujitetea............ Kazi tunayo, sioni Tanzania baada ya uongozi wa Kikwete...........
 
Rais Kikwete ana tatizo moja tu, anapenda kuwa rais lakini hapendi/anakwepa majukumu yanayoambata na urais. Cheng nyingi!
 
JG, kuna msemo
'everyone has a price, the problem is to know what it is'

(am just thinking loud)

Duh!
Siamini kama na wewe Pasco unanunua huo utumbo...
Kwa mara ya kwanza nimeanza kuelewa mjadala wako na MTM..
 
Mkuu Kongosho, mission na vission ni ile ilani ya uchaguzi aliyoinadi na kuchaguliwa. He had a mission ya maisha bora kwa kila Mtanzania na vision Tanzania yenye neema inawezekana kupitia ari mpya, kasi mpya, na nguvu mpya!. Watendaji aliowategemea ndio wamemwangusha!.

Kufuatana na maelezo yako inaelekea hujui tofauti kati ya VISION na MISSION!! Vision ni maono yako unavyotaka vitu viwe na Mission ni jinsi utakavyofanikisha kufikia hayo malengo ya maono yako!! Tukirudi kwenye mada, Jakaya ana mapungufu ya kuamini sana ushirikina katika utendaji wake!![ usiniambie nikupe ushahidi kwani Sheikh Yahya kafa!!] Maisha bora kwa kila mtanzania haiwezi kuwa mission!!
 
Safari za nje ya nji zipungue.Sometimes anaambata na umati wa watu na wote wanagharamiwa na kodi ya wananchi.Sometimes kuna safari amabazo waziri wa mambo ya nje au mawaziri husika wanaweza kuwakilisha na wapunguze idadi ya wasindikizaji.
JK anasafiri na umati wa watu, wenhi wao hawana lolote, wanakwenda SHOPPING!
Ni mzigo kwa wananchi.
No wonder teachers and doctors are striking!
 
Tatizo la Kikwete ni moja tu - uvivu! Si mchapakazi. Hasomi wala hafikiri wala haandiki. Rais gani huyo?
 
Mfano wa kwanza wa udhaifu huu wa huruma uliyopitiliza ni pale alipowasamehe majizi ya EPA na kutaruhusu yarudishe fedha yalizo kwiba na kusemehewa kutofikishwa mahakamani!. Spika Sitta pia alimlaumu rais JK kwa upole huu! Lingekuwa ni bunge makini, imperchment process ingeanza right away!

Mkuu Pasco,

Si kweli kwamba ni huruma ndio ilimfanya awaache waachiwe. Ni kwamba the whole saga ya EPA ilikuwa inagusa fedha za kampeni yake na pia ilikuwa inagusa watu wake wa karibu na hakuwa tayari kuwashughulikia. Ndio maana mpaka leo hii akina Maranda wanatumikia kifungo na wengine kesi zao hazisongi mbele na wengine hawajafikishwa mahakamani, lakini ki-misingi wote walifanya makosa yanayofanana. Lugha nzuri hapa ni kwamba JK ni mnafiki, huwa haamanishi kile anachosema.
 
hizi sentensi huwa zinasemwa sana na majuha wa CCM

Juzi mnyika kasema hivi hivi
leo ww unasema hivi hivi

kesho sijui nani atasema

You are dead wrong my dear pasco........all i can say no is think again and you have a room to correct that view!
Kwani Mnyika naye ni juha wa CCM?, au ni Mnyika gani unaye mzungumzia hapa?
 
Sasa nitoe constructive criticisms.

JK ni Rais anayependa sifa, hilo ni tatizo ambalo litagharimu sana legacy yake. Hotuba yake ya kwanza kwa Bunge lake akiwa kama Rais, aliahidi mambo mengi sana ambayo kama angeyatekeleza yangeweza kumpa umaarufu mkubwa sana, lakini ilipokuja kwenye utekelezaji ilikuwa ni zero. Mfano, aliahidi kurudisha nyumba zilizouzwa na serikali ya Mkapa, hakutimiza. Aliahidi kupitia upya mikataba mipya, hakuna kilichofanyika. Aliahidi kupambana na ufisadi, lakini akawa wa kwanza kuficha uvundo wa ufisadi wa Mkapa, Chenge na wengineo wengi ambao walikuwa wamegubikwa na tuhuma za ufisadi ambazo ushahidi wake ulikuwa wazi kabisa.

Mwaka 2005 hakuuzwa na Ilani ya Chama chake, bali aliuzwa na mtandao, vyombo vya habari na ule unafiki wake kwamba yeye ni mtu wa watu. Ndio maana kila kukicha utamuona yuko kwenye misiba. A day baada ya kuchaguliwa kuwa Rais alidamkia Muhimbili, watu wakasema sasa tumepata Rais atakayejali afya za walalahoi. Sasa kama Rais anajali afya za walalahoi na watendaji wakuu wa Wizara ya Afya wana tuhuma kibao, kwanini hizo tuhuma zisifuatiliwe? Halafu leo anasema hawezi kufanya mabadiliko kwa shinikizo la madaktari, sasa kama wameona kwamba viongozi wa wizara hawafai, wao wafanye nini?

Nani anafanya assessment ya utendaji kazi wa kiongozi? Ni Appointing Authority au yule anayeongozwa? Mjomba alishasema tutapima size ya kiatu after 5 yrs, so the Drs have all the rights za ku-judge utendaji kazi wa mawaziri wa wizara yao.

Nije swala la Katiba, pia JK kwa kupenda sifa na alipoona kwamba upinzani unapata umaarufu, alikurupuka na kuahidi katiba mpya. Bahati mbaya hakujua kwamba Katiba mpya inamuweka mahali pagumu zaidi maana wana CCM walikuwa hawataki mabadiliko. Matokeo yake mwanzo kwenye hotuba akawasema wapinzani na kudai kwamba atajaribu u-dictator na baadaye akaja kulamba matapishi yake kwa kuwaruhusu wapinzani wapeleke mapendekezo yao na alikubaliana nao. JK alifanya hivyo baada ya kuona wananchi wako against msimamo wa chama chake. Ndio maana nasema kwamba JK anapenda sana sifa na hiyo ni weakness mbaya sana.

Kitendo cha kupata 61% kwenye uchaguzi uliopita, lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa JK, hakutegemea ashuke kutoka 80% mpaka hapo, na hapo NEC (Tume ya Uchaguzi) ilikuwa imemsaidia sana kuchakachua na yeye anajua hilo. Kama wasingemsaidia, hata hizo 61 zisingefika. Ndipo akaunda Kamati ya Mukama kuchunguza kiini cha CCM kufanya vibaya kwenye huo uchaguzi. Ndipo ikaja Falsafa ya Vua Gamba, ambayo nayo imezidi kumuweka pabaya maana ameshindwa kuitekeleza kama wananchi walivyokuwa wakitegemea.

To conclude, ni kwamba kwa kuwa Rais wetu anapenda masifa, mara nyingi huwa ni mkurupukaji wa kuweka ahadi tamu na nzuri kusikika masikioni mwa wananchi bila kuzifanyia tathimini ya kina ili kuona kama ni ahadi ambazo zinatekelezeka au la. Matokeo yake sasa, Pinda ndo amekuwa mbebeshwa lawama halafu JK yuko kimya hasemi kitu kabisa na hasa akishapima upepo kwamba wananchi wako against. Ninamuonea huruma Pinda kwa kuwa wakati mwingine ni ngumu sana kufanya kazi na mtu ambaye anapenda credit iende kwake all the time na mabaya yote wabebeshwe wengine.
 
aliingia kwenye urais bila vission wala mission.
Hili ni pungufu kubwa sana hata katika maisha ya mtu mmoja mmoja.

Katika ngazi ya uraisi ni balaa zaidi.
Mkuu Kongosho, mission na vission ni ile ilani ya uchaguzi aliyoinadi na kuchaguliwa. He had a mission ya maisha bora kwa kila Mtanzania na vision Tanzania yenye neema inawezekana kupitia ari mpya, kasi mpya, na nguvu mpya!. Watendaji aliowategemea ndio wamemwangusha!.
Pasco, kama wasaidizi ndo wanamuangusha, sasa mbona yeye ndo bingwa wa kuwalinda? Mifano ya Jairo, ngeleja, wahusika wa EPA ambao wapo kwenye serikali na chama chake?

Au tufanye hivi, ni watumishi na wasaidizi wake wepi hao wanaomuangusha? Yeye anajua hilo? Kama anajua anafanya nini? Kama hajui ni kwanini hajui wakati mtu kama wewe pasco wa jf unajua kwamba wasaidizi ndo wanamuangusha?

This is a lame excuse...!
 
TZ haijawahi kuwa na haitakuja kuwa na rais dhaifu kama JK....i can swear on this....hata Mzee Mwinyi alikuwa bora mara dufu kumzidi JK......Mwinyi yeye uzuri wake alikuwa anatambua udhaifu wake na hivyo alijitahidi kuweka washauri makini kwenye mambo ya msingi kama uchumi at least akamaliza urais wake bila mabalaa na vilio kama anayoleta JK TZ ya sasa....

Nasema hatujawa na hatutakuja daima kuwa na rais hovyo kama tulie nae sasa.......mtu anayejifanya mjuaji kumbe hamnazo....mtu aliyepewa madaraka makubwa na katiba kuisimamia nchi lakini anachofanya ni mzaha......mtu mwenye majibu mepesi siku zote kwa mambo makubwa ya nchi.....kwa kifupi hatuna rais serious TZ kuelekea karibu miaka 10 sasa...kosa walilolifanya watanzania kumpa huyu bwana urais watalijutia kwa miaka mingi saaana.......ifike mahali sasa watanzania wajifunze....
 
Mkuu Kongosho, mission na vission ni ile ilani ya uchaguzi aliyoinadi na kuchaguliwa. He had a mission ya maisha bora kwa kila Mtanzania na vision Tanzania yenye neema inawezekana kupitia ari mpya, kasi mpya, na nguvu mpya!. Watendaji aliowategemea ndio wamemwangusha!.

Hamna kitu kinachotukwamisha kimaendeleo kama hii kauli.
Haina tofauti na mchakato unaendelea, upembuzi yakinifu unafanyika na juhudi za kutafuta wahisani zinafanyika.
Yeye ni mtendaji mkuu, [ unlike, say Rais wa Israel, au German, au Malkia wa UK], ni mkuu wa majeshi, ana power of the purse, anachagua hao watendaji without approval from anybody/anything.
Come on Pasco, spare us this nonsense.
 
Back
Top Bottom