Mapungufu niliyoyaona pale Jangwani - muhimu CHADEMA kuyafanyia kazi

Ni mawazo mauri ya kujenga. binafsi naamini wahusika watayafanyia kazi ili kusiwepo kasoro next time
 
Maudhui ya mkutano yalikuwa ni nini na yalifikiwa?
Ratiba ya mkutano jinsi iliyopangwa ilitekelezwa?
Majibu ya maswali hayo yananifanya nione kwamba katika mkutano ule HAPAKUWA NA MAPUNGUFU.
Mapungufu yanatokana na mambo kufanyika yakiwa na tofauti na jinsi yalivyopangwa.
Tatizo linalokuja ni kwamba kuna watu wanauzoefu na style ya mikutano ambayo wameiweka kichwani na mtiririko wa ratiba waliouzoea, wakiona tofauti na hayo wanaona kwamba ni mapungufu.
 
Nilipata faraja kuhudhuria mkutano wa Jumamosi, niliona fahari sana kuhudhuria badala ya kuwa 'commentator' tu mitandaoni etc. Ni vizuri kujitokeza na kuwa counted out! Ni muda muafaka wa watu kuchukua hatua ktk ukombozi wa nchi hii dhidi ya udhalimu wa CCM.

Binafsi niliona dosari kadhaa ambazo ningependa uongozi ewa juu wa CDM wazifanyie kazi.

1. Kulikuwa na mapungufu ya gender. Idadi ya akina mama, hata kama ni vijana ilikuwa ndogo kulinganisha na wanaume. Nadhani hii inataka kusema akina mama wengi wanapenda CCM? Nadhani kuna haja ya kuhamasisha akina mama wajitokeze kwa wingi kwenye hii mikutano na pia kujiunga na CDM. SIna uhakika na mikoani ila kwa pale Chadema square Jumamosi akina mama walikuwa wachache.

2. Wengi waliojitokeza ni vijana. Wako wapi watu wa rika nyingine? Nadhani ukombozi wa nchi hii ni wetu sote na si vijana pekee. Naelewa vijana ni wepesi zaidi kuhamasika na kuwa tayari kwa mabadiliko, lkn kwa hatua mbayo nchi hii imefika, nadhani watu wote, vijana, middle ages na watu wazima sote tunatakiwa kujitokeza kuikomboa Tanganyika yetu!

Mmapungufu mengine tayari yameshasemwa na wengine. NI hayo tu kwa sasa!
 
Natumaini wamekusikia na kukuelewa tu. Tusonge mbele pamoja ili kuleta ukombozi
 
Kasoro ulizoziainisha ni za msingi, wahusika wanatakiwa kuzifanyia kazi. Ipo siku wakishika dola hawatakiwi kufanya kazi kwa propaganda. Wananchi wanahitaji kujua hatu ambazo chama kimefikia katika jitihada zake za kuiamsha jamii, na ni mategemeo ya takwimu hata za matukio na takwimu za matarajio siku zijazo zina umuhimu wa kujenga kujiamini na kuamsha zaidi ari ya watu kuitikia na kufikia malengo.
Tupo pamoja karibu sana mkuu.
 
Mkuu Kurunzi, hongera kwa kuwa bold na kuleta ukosoaji wa CDM in a constructive criticism. Sisi tuliofanya hivyo kule nyuma, tuliishia kutukanwa!.

Pia nawapongeza wana Chadema kwa yote, they are growing up for the better! This time hawajatukana!.

Amini msiamini, critique ndio inayojenga chama imara kuliko pongezi za sifa na mapambio!.

Pasco.
Mkuu Pasco, ulipata nafasi ya kuhudhuria mazishi ya marehemu Kyaruzi?
 
Arusha kawaida mkutano kama huo ukiisha maandamano yanakuwepo viongozi huamua kuingia mount meru hotel , na ndio unakuwa mwisho wa maandamano ...waandamanaji wakiisha kutawanyika na viongozi nao hutawanyika lakini mostly tunakutana pale cet garden(kwa mrefu) kwa mengineyo
 
Ha ha ha haaaaaaaaa....point ya mwisho.....MC huenda alikuwa na kazi ya harusi baadaye!!!
 
Jana nilikuwa mmoja wa wahudhuriaji wa mkutano pale Jagwani wa M4C, ukiacha kasoro chache lakini umati wa watu hasa vijana ulikuwa na mkubwa sana, pia nilipata fursa ya kutembea kwa mąndamano kuwasindikiza viongozi kwenye ofisi za chama toka viwanja vya Jagwani (CDM SQUARE) mpaka makao makuu ya chama pale kinondoni, lengo langu la kushiriki maandamano hayo nilitaka kujua je umati hatima yao itakuwa nini na je wakifika pale Makao makuu ya chama watafanya nini vijana wamekuwa na hamasa kuu hivi?

Hayo ndiyo mambo ambayonilitaka kupata majibu yake na kwa jibu moja ni kwamba watu hasa vijana wanataka mabadiliko na wapotayari kwa mabadiliko huwezi amini kila kijana niliona anachukuwa no. ya viongozi zilizotangazwa kwa wanaotaka kufungua matawi nilifurahi kuona watu wameliitikia kwa hamasa.

Lakini pamoja na hayo kunamapungufu muhimu sana ambayo nimeyaona na CDM wanatakiwa kuyafanyia kazi, nitayataja machache hapa:

1. Pamoja na muda ulikuwa finyu wa viongozi kuzungumza lakini kuna mambo ambayo hayakupangwa kwa utaratibu uliopangiliwa vema mathalani ni pale Dr. Slaa alipomtaka na kumsihi mwenyekiti kama Kiongozi wa upinzani Bungeni na kama waziri mkuu kivuli pamoja na kabineti mambo ambayo wanatakiwa wayafanyie kazi wakiwa Bungeni kwani yamekuwa kero kwa wananchi mathalani Slaa alimtaka Mbowe ashughulikie suala la watu kunyanyaswa na polisi binafsi sikusikia Mbowe akisema amesikia na atayafanyia kazi kuyafanyia kazi.

2. Nilitegemea kupitia tungepewa tadhini japo kidogo juu ya kampeni hii M4C na vua gamba vaa gwanda imekuwa na mafakio kiasi gani, nilitegemea hata kupata tąrifa fupi ya viongozi wa Dar. tathini ya Chama hapa dar. mathalani tuna matawi mangapi, wanachama wangapi nini mahitaji yetu na kadhalika.

3. Nilitegeme kupata hata salamu toka kwa wageni wa vyama rafiki angalau mmoja angepewa nafai ya kuzungumza akatupa hata exposure za wenzetu hapo niliona mmekuwa so conservative.

4. Mc alifanya kazi nzuri sana ya uhamasishaji sijajua jina lake lakini alivaa ovyo sana sawa inawekana ni msanii lakini angalau angevaa sare za chama au kwa njia nyingine nadhifu lakini alionekana kama aliitwa tu kuja kufanya kazi ya u-mc tu.

Ni hayo tu.

Mawazo ya mdau ni mazuri sana. Its really constructive ideas. huyu ni mzalendo wa chama, maana mtu anapokuambia mapungufu yako anakupenda na kukuthamini. Tusimbughudhi wadau-angekuwa anaponda tungejua la kumwambia maana wadau tuko macho.

M4C-forever
 
At least kukosoana wenyewe kwa wenyewe bila kutukanana wala kuonekana wasaliti ni jambo la msingi sana na litaipa pia JF Heshima.....sio kuunga mkono hata pale unapodhani panahitaji kunyoshwa kidogo.....Pamoja sana wakuu......Uhuru wa maoni muhimu ukizingatia hata jina la chama linaashiria demokrasia sasa itakuwa ni ajabu sana kuwa wakwanza kuifinyanga demokrasia...

Hatuwezi kuwaza sawa sawa siku zote as if viongozi wa chama ni Malaika...Ukiona hivyo ni dalili ya kukiua chama...
 
Back
Top Bottom