Mapungufu niliyoyaona pale Jangwani - muhimu CHADEMA kuyafanyia kazi

Ni vizuri kufanyia kazi changamoto... Wengi wetu tumeshindwa kujikosoa.
 
jamani si kila mtu anayekosoa ana nia mbaya..kuna namna ya kuboresha kulingana na mtizamo wake..upande wangu nimeona kuna point fulan aliposema au kudai tathimini..ni lugha tu aliyotumia cha msingi naona alilenga kitu kinaitwa baseline survey..hii hufanyika unapotaka kufanya jambo anatakiwa kuwa na data za wakati huo hii itakusaidia kufanya ufuatiliaji(monitoring) na baadae tathimini(evaluation) yote haya kukuwezesha kujua kama upo katika mstari sahihi na mwisho je umefanikiwa?
 
Mkuu Kurunzi, hongera kwa kuwa bold na kuleta ukosoaji wa CDM in a constructive criticism. Sisi tuliofanya hivyo kule nyuma, tuliishia kutukanwa!.

Pia nawapongeza wana Chadema kwa yote, they are growing up for the better! This time hawajatukana!.

Amini msiamini, critique ndio inayojenga chama imara kuliko pongezi za sifa na mapambio!.

Pasco.

Ni kweli Pasco, tupo CDM kukijenga hata mahali nilipo nakijenga kwakukosoa na kupongeza lakini kwa sasa tunelekekea kuchukua nchi ni lazima tujipange vema ili tusiwape maadui pakusemea.
 
Nafikiri mtoa mada uko sahihi kabisa umetoa very simple but important constructive critisism.

Binafsi tathmin yangu ni kwamba mkutano huo ulikuwa more of a PR event kitu nnachokubaliana nacho kabisa kutokana na hali halisi ya chama kinavokua, hivo hayo uliyoyasema yalitakiwa kuzingatiwa.

Nafikiri wahusika wameyasikia na watayafanyia kazi

Binafsi natamani kuona umakini kwa vyama vyote au vingi vyao maana vyama vitakapokuwa makini sera zetu kama nchi zitakuwa bora na maisha yetu yataboreka sana

Niachie hapa kwa leo.
 
uko sahihi kamanda. mimi pia napenda wawe wanatangaza hela zinazopatikana wakipitisha mchango. ni hela ya umma hiyo,wapenda mageuz.

Sio jambo rahisi kufanyika majumuisho na kutangaziwa mapato hapo hapo. Taarifa inatolewa baadaye kadri taarifa sahihi zinavyokuwa zimekusanywa.
 
Nadhani jambo zuri kuwa na more critics kuliko kupongeza ili wahusika warekebishe na kufanya bora zaidi Mikoa mingine,,

Tumeshakuwa watu wazima lazima tukubali chałages ndani na nje ya chama.
 
Hakuna haja ya kutaja idadi ya wanachama, kimbunga kitaonekana mwaka 2015. Leo nimemsikia MzeePeter kisumo ambaye ni mwenyekiti wa baraza la wadhamini la ccm kwamba ccm ina wanachama milioni 5 lakini wamesahau kuwa tangu operation ya vua gamba vaa gwanda ianze wanaccm wengi wamehamia cdm.
 
jamani si kila mtu anayekosoa ana nia mbaya..kuna namna ya kuboresha kulingana na mtizamo wake..upande wangu nimeona kuna point fulan aliposema au kudai tathimini..ni lugha tu aliyotumia cha msingi naona alilenga kitu kinaitwa baseline survey..hii hufanyika unapotaka kufanya jambo anatakiwa kuwa na data za wakati huo hii itakusaidia kufanya ufuatiliaji(monitoring) na baadae tathimini(evaluation) yote haya kukuwezesha kujua kama upo katika mstari sahihi na mwisho je umefanikiwa?

Naamini tathimini hiyo itapelekea mimi nma we tujue ni wapi tunapaswa kuongeza nguvu.
 
mkuu samahan, ninawiwa kusema hoja zako nyepesi kuliko uji wa futari
 
Hakuna haja ya kutaja idadi ya wanachama, kimbunga kitaonekana mwaka 2015. Leo nimemsikia MzeePeter kisumo ambaye ni mwenyekiti wa baraza la wadhamini la ccm kwamba ccm ina wanachama milioni 5 lakini wamesahau kuwa tangu operation ya vua gamba vaa gwanda ianze wanaccm wengi wamehamia cdm.

Hapana records na takwimu nimuhimu kwani mapambano yetu haihitaji kificho kwani ni dhairi na
 
Kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri uliyofanya, Ninyi ndio tunawahitaji.

Hapa tupo watu wa tabaka mbalimbali, maono mbalimbali, viwango vya kufikiri na kuona mbalimbali, uwezo wa kujenga hoja kwa viwango mbalimbali, uchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii mbalimbali. Kwa aliye msomi au mzoefu wa kusoma tukio na yaliyojilia kisha kutoa hitimisho atakuwa amekuelewa fika. Kuna wanaochangamkia mipasho na kuna wanaopenda uchambuzi yakinifu.

Kasoro ulizoziainisha ni za msingi, wahusika wanatakiwa kuzifanyia kazi. Ipo siku wakishika dola hawatakiwi kufanya kazi kwa propaganda. Wananchi wanahitaji kujua hatu ambazo chama kimefikia katika jitihada zake za kuiamsha jamii, na ni mategemeo ya takwimu hata za matukio na takwimu za matarajio siku zijazo zina umuhimu wa kujenga kujiamini na kuamsha zaidi ari ya watu kuitikia na kufikia malengo.

Wawapo jukwaani kawaida yao kila mmoja huwa na yake ya kuongea, na katu hawaweki kumbukumbu ya aliyemtangulia ameongea nini kwa minajili ya kama anatakiwa kutolea ufafanuzi, au kupokea pendekezo, hayo ni mambo muhimu, kwani ukiwa kiongozi unapotoa hotuba inabidi ijibu yale yaliyoongelewa na viogozi wa chini yako ambao wamekutangulia kutoa hotuba za utangulizi.

Jambo moja ambalo nimekubali wameshalifanyia kazi ni ila hamaki ya kujibu hoja jukwaani na kuzitolea maamuzi. Mkutano wa pale Jangwani ambapo wamepabatiza jina la Chadema Square pamoja na shinkizo la watu wengi licha ya vyombo vya habari, matamko yaliyotangulia na baadaye kusukumwa na wahudhuriaji wa mkutano ule kutolea tamko kuhusu Shibuda, busara ilitawala na kuongelea kwa mbali sana bila kuonyesha kuligusa moja kwa moja na kuhitimisha kwamba vikao vitalifanyia kazi. Hiyo ndiyo busara inayotakiwa na ndio ukomavu wa kuongoza nchi. Papara husababisha mwanya wa mipasuko.

Nataraji ushauri wako umesikika na wameusikia, nategemea wataufanyia kazi, kwani kujenga nyumba si kazi ya siku moja, na ni mambo mengi yanayofanya nyumba ikamilike. Wengine wanamaliza kujenga nyumba kwa miezi na wengine kwa miaka hata hivyo kuna baadhi wanaishi ndani ya nyumba ambayo baadhi yatakamilika kwa muda wanapoishi. Bado wana nafasi ya kuyafanyia kazi nataraji nafasi nyingine tutaona mabadiliko ya kuziba mapungufu yaliyojitokeza.
 
4. Mc alifanya kazi nzuri sana ya uhamasishaji sijajua jina lake lakini alivaa ovyo sana sawa inawekana ni msanii lakini angalau angevaa sare za chama au kwa njia nyingine nadhifu lakini alionekana kama aliitwa tu kuja kufanya kazi ya u-mc tu.

Ni hayo tu.

Kama sijakosea, MC anaitwa JOHN MREMA, mkurugenzi bunge na halmashauri chadema, pia 2010 aligombea ubunge jimbo la vunjo na augustine mrema. Ni jembe la ukweli, labda mkuu ulipendelea avae sare but for me namkubali sana kamanda kama makamanda wengine licha ya alivyokua amevaa.

BTW; thanx for constructive critism, WATAYAFANYIA KAZI coz huwa wanapita huku.
 
Tunapokosolewa tukubali usimwangalie ni nani anayekukosoa hii itatufanya tujenge kilicho bora zaidi
 
Siku CHADEMA itaacha kufanya makosa madogo madogo itakuwa sio chama cha siasa tena bali mwakilishi wa mungu duniani; Ni lazima makoso madogo madogo yatokea kibinadamu.

Tunachokataa CCM ni kufanya makosa makubwa makubwa mfululizo bila hata haya, tunakufa na umaskini wakati wanasema maisha bora, tunashiriki ubepari wakati wanasema siasa za ujamaa. Kama huamini moja ya makosa makubwa ya CCM ni katiba ya zanz, ambayo wao ndo waliingia mwafaka na CUF, wakajipoendekeza kwa kusema zanz ni nchi; wanawadanganya watanzania kwa umaarufu wa muda mfupi, kama zanz ni nchi basi CCM & CUF ndo walivunja muungano tangu siku hiyo. Inachofanya Tanganyika ni kutoa ulinzi kwa Znz kama USA kwa Afghanistan etc, Makosa mengine ni Bilal kuwa Makamu wa rais wa Tanganyika wakati ni Mzanzibar, zanz si ni nchi??? inamaana Tanzania ndo Tanganyika, Zanz ni Zanz.

Kosa jingine la CCM vyeo kwa upendeleo, mtu yuko masomoni anapewe cheo, Mbunge anakuwa RC au DC tumelalamika sana tangu 2006 au 7 huko Ukerewe mtoto wa primaty school alimuuliza Lowassa inakuwaje ktk upungufu wa ajira mtu mmoja napewa vyeo lukuki??? Hili nalo linajirudia bila huruma kwa Mtanzania.

EPA, Richmond yanajirudia kila siku huku wahusika wakila bata. na mengine mengi unayoyajua.
 
Ni mawazo mazuri yafanyiwe kazi nia ni kuchukua Serikali 2015 na tusisite kukosoa ndipo tutaimalika zaidi peoplessss power.
 
Back
Top Bottom