Mapungufu niliyoyaona pale Jangwani - muhimu CHADEMA kuyafanyia kazi

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,271
9,900
Jana nilikuwa mmoja wa wahudhuriaji wa mkutano pale Jagwani wa M4C, ukiacha kasoro chache lakini umati wa watu hasa vijana ulikuwa na mkubwa sana, pia nilipata fursa ya kutembea kwa mąndamano kuwasindikiza viongozi kwenye ofisi za chama toka viwanja vya Jagwani (CDM SQUARE) mpaka makao makuu ya chama pale kinondoni, lengo langu la kushiriki maandamano hayo nilitaka kujua je umati hatima yao itakuwa nini na je wakifika pale Makao makuu ya chama watafanya nini vijana wamekuwa na hamasa kuu hivi?

Hayo ndiyo mambo ambayonilitaka kupata majibu yake na kwa jibu moja ni kwamba watu hasa vijana wanataka mabadiliko na wapotayari kwa mabadiliko huwezi amini kila kijana niliona anachukuwa no. ya viongozi zilizotangazwa kwa wanaotaka kufungua matawi nilifurahi kuona watu wameliitikia kwa hamasa.

Lakini pamoja na hayo kunamapungufu muhimu sana ambayo nimeyaona na CDM wanatakiwa kuyafanyia kazi, nitayataja machache hapa:

1. Pamoja na muda ulikuwa finyu wa viongozi kuzungumza lakini kuna mambo ambayo hayakupangwa kwa utaratibu uliopangiliwa vema mathalani ni pale Dr. Slaa alipomtaka na kumsihi mwenyekiti kama Kiongozi wa upinzani Bungeni na kama waziri mkuu kivuli pamoja na kabineti mambo ambayo wanatakiwa wayafanyie kazi wakiwa Bungeni kwani yamekuwa kero kwa wananchi mathalani Slaa alimtaka Mbowe ashughulikie suala la watu kunyanyaswa na polisi binafsi sikusikia Mbowe akisema amesikia na atayafanyia kazi kuyafanyia kazi.

2. Nilitegemea kupitia tungepewa tadhini japo kidogo juu ya kampeni hii M4C na vua gamba vaa gwanda imekuwa na mafakio kiasi gani, nilitegemea hata kupata tąrifa fupi ya viongozi wa Dar. tathini ya Chama hapa dar. mathalani tuna matawi mangapi, wanachama wangapi nini mahitaji yetu na kadhalika.

3. Nilitegeme kupata hata salamu toka kwa wageni wa vyama rafiki angalau mmoja angepewa nafai ya kuzungumza akatupa hata exposure za wenzetu hapo niliona mmekuwa so conservative.

4. Mc alifanya kazi nzuri sana ya uhamasishaji sijajua jina lake lakini alivaa ovyo sana sawa inawekana ni msanii lakini angalau angevaa sare za chama au kwa njia nyingine nadhifu lakini alionekana kama aliitwa tu kuja kufanya kazi ya u-mc tu.

Ni hayo tu.
 
Uliosema wataweza kuyafanyia kazi.
Je walipotanga mkutano wa jangwani walisema watazungumzia M4C na katiba mpya au tathimini ya M4C?. Kumbuka tangu izinduliwe Arusha, D.S.M ndio mkoa wa pili sasa tathimini yanini wakati hata robo au nusu ya mikoa hawajafika?.

Labda nikuulize kwanini unafikiri Mh. Tundu lisu alikuwa mzungumzaji wa kwanza, Dr. Slaa akafuata na baadae Mh. Mbowe? Na hukumuona Mbowe alikuwa anaandika wakatia Dr. Slaa anazungumza?..,
 
mbona unazungumzia hitimisho wakati M4C ndio kwanza ipo kwenye introduction?....subiria majumuisho,kuhusu wagen kupewa muda pale walikua wanacheza na time na polisiccm walikua wanakula timing ikizidi hata dk 5 tu,wanatia timu ingawaje wasingeweza muzic
 
Kuhusu wagen kupewa muda pale walikua wanacheza na time na polisiccm walikua wanakula timing ikizidi hata dk 5 tu,wanatia timu ingawaje wasingeweza muzic
Lakini Mkutano ulianza saa nane.
 
Uliosema wataweza kuyafanyia kazi.
Je walipotanga mkutano wa jangwani walisema watazungumzia M4C na katiba mpya au tathimini ya M4C?. Kumbuka tangu izinduliwe Arusha, D.S.M ndio mkoa wa pili sasa tathimini yanini wakati hata robo au nusu ya mikoa hawajafika?.

Labda nikuulize kwanini unafikiri Mh. Tundu lisu alikuwa mzungumzaji wa kwanza, Dr. Slaa akafuata na baadae Mh. Mbowe? Na hukumuona Mbowe alikuwa anaandika wakatia Dr. Slaa anazungumza?..,

Japo angeseama atayafanyia kazi na ametake note kwani si wote waliona anatakenote.
 
unajua kiukweli hauwezi fanya kitu na kukava sehemu zote izo ni dosari ndogo sana kaka tupo katika mapambano mambo ya dosari ambazo hazina tija haina haja ya kuyazungumzia cha muhimu tuzungumzie ni jinsi gani tutaikomboa nchi yetu ya tanzania kutoka katika mikono ya wazungu weusi wa kikoloni kwa mtu mwenye akili na mwenye busara atazingatia haya ila kama una kichwa cha kuku subiri kukatwa 2015
 
Mkuu bila kusahau vyombo vya music na vipaza sauti tafadhali vilekebishwe vilisumbua sana!
 
Mkuu Kurunzi, hongera kwa kuwa bold na kuleta ukosoaji wa CDM in a constructive criticism. Sisi tuliofanya hivyo kule nyuma, tuliishia kutukanwa!.

Pia nawapongeza wana Chadema kwa yote, they are growing up for the better! This time hawajatukana!.

Amini msiamini, critique ndio inayojenga chama imara kuliko pongezi za sifa na mapambio!.

Pasco.
 
yaa nakubaliana na moja la mc kuwa ovyo,kiukweli mi sikuamini kama yule ni mc.
 
Lakini Mkutano ulianza saa nane.

Uanze saa nane au saa mbili, nyie hamna uwezo wa kutupangia ratiba. Kwanza hivyo mnavyoviita vyama rafiki ndio vipi?

Yale ni mapambano sio protokali za kutambulishana na kupigiana makofi, kwani Mbatia si kafanya mkutano wake kule Mtwara juzi, mbona hamkuhoji kwa nini hakutambulisha wapinzani wengine (as if Mbatia naye ni mpinzani).

Sema shida yenu ni kwamba lazima mpekue pekue weeee mpk mpate jambo la kukosoa kwa jinsi msivyo na haya. Tafuteni mengine, haya mliyoorodhesha hapa ni utumbo mpana.
 
No 4 ndio ya kufanyia kazi hayo mengine hayana mshiko m4c ndio inaanza na matawi ndio kwanza tathimini ya nini?
 
Kurunzi na Pasco,
Nyumba yenu imeoza Bati hadi mvua inawanyea, sasa mnapata wapi kiburi cha kumkosea mwenzenu aliyeezeka kwa Vigae vya Afrika Kusini kwamba anatakiwa apandishe Gebo ili upepo na wadudu wasiingie ndani? Au mnatafuta msaada wa kuezekewa?

TUMBIRI,

tumbiri@jamiiforums.com
 
uko sahihi kamanda. mimi pia napenda wawe wanatangaza hela zinazopatikana wakipitisha mchango. ni hela ya umma hiyo,wapenda mageuz.
 
Back
Top Bottom