Mapungufu katika Wimbo wa Taifa la Tanzania

Unaishi dunia gani vile???Hao wananchi unaoongelea ambao bado hawajaumia ni wapi??

umeona yaliyotokea 'Kenya' baada ya uchaguzi?, ni kiongozi gani aliyeathirika?, ni raia wangapi walioathirika?. Think twice.
 
Naomba nisikujibu..sio kwa kukosa chakusema bali wa kumwambia!Peace!
 
huna wa kumwambia?!, kwani uko chumbani kwangu?!, naomba nikukumbushe kuwa hapa uko janvini na maelfu kwa maelfu ya wasilizaji/watazamaji na wachangiaji wanakusubiri utoe huja.
 
Kaaazi kweli kweli!Habari ya chumbani kwako inahusikaje hapa??Hao maelfu wanajua ambacho ningesema maana tumeshakiongelea sana!
 
Salamaleko wanajamvi,
Wimbo wa Taifa ni mojawapo ya alama za Taifa husika zikiwemo pia fedha, bendera nk. Kwa maana hiyo alama hizi ni vitu vya kuheshimika sana na si jambo la utani hata kidogo. Ndugu zetu wa CDM wamekuwa wakiimba wimbo huu wa Taifa na kubadilisha,, yaani pale panapotamkwa Tanzania,, wao huweka CHADEMA,,, Mfano "Tubariki CHADEMA na watu wake" Ukitazama hata ule mkanda wa maandamano ya Arusha on you tube utaona ninachosema. Kinachonipa kichomi ni pale ambapo viongozi wakuu Dr. Slaa, Mbowe na wengine wanaliachia tu jambo hili pasina kulitolea tamko kwa wafuasi wao kwamba wanapotosha na kuudhalilisha wimbo wa Taifa. Sasa unapoimba "CHADEMA na watu wake" katika wimbo wa Taifa,, ina maana CHADEMA ni Taifa? na lina watu wake?
Kwanini wasitunge tu nyimbo zao zenye kusifia CDM kadri wapendavyo badala ya kuudhalilisha wimbo wetu wa Taifa? Nasema ni kuudhalilisha kwa sababu mababu zetu waliopigania uhuru na kwa hali na mali na hatimaye kutuwekea wimbo huu wa Taifa, hawatafurahii mambo ya namna hii, na ni kutowatendea haki na kuwadharau kama si kuwadhalilisha. Mwalimu Nyerere huyu huyu ambaye CDM wanamtumia sana wanapotaka kulinganisha na viongozi wa leo wa CCM,, je angekuwa hai angefurahia tendo hili la kuuchafua wimbo wa Taifa kwa mithili hii??
Wenzao CCM wana nyimbo zao wenyewe lukuki za kusifia chama chao na kamwe miaka yote sijasikia wakiimba "CCM na watu wake".
Hata watoto wetu wanaokua leo,, wakiendelea kusikia hivyo,, ni picha gani wanaijenga? Shuleni wanaimba wimbo wa Taifa wenye maneno tofauti mtaani wanakutana na upotoshaji, tunakwenda wapi? Tofauti za kiitikadi zisifike mahali pa kudhalilisha Taifa, tuweke uzalendo mbele. Isije baadaye ikaonekana kama vile CDM ni chama cha fujo, vurugu na hata kuudhalilisha wimbo na Taifa Tanzania.
Nashauri Dr. Slaa na Mwenyekiti Mbowe,, wakiwa kama watanzania na wazalendo wa kweli,, walipinge na kulikemea kwa nguvu pindi wafuasi wao wanapotaka kuudhalisha wimbo na Taifa kwa ujumla. Hili mimi nalipinga kwa nguvu,,.Tanzania imekuwepo kwa muda mreefu na itaendelea kuwepo hata sisi tukifa,, kuuchezea wimbo wa Taifa kwa kubadilisha maneno ni jambo baya kabisa. Vipi kama kila chama TLP, UDP, CUF nk wakiimba hivyo? Wimbo huu utakuwa wa heshima kweli?
Angalizo: Wimbo wa Taifa siyo Bongo Fleva, ni alama ya nchi Tanzania na unatakiwa kupewa heshima stahili. Siamini kama Mbowe naSlaa wanawaambia wafuasi waimbe hivyo, na siamini kama wanafurahia.
Na kama wanafurahia,, Basi,, Leave me alone!!
 
Kwakweli japokua mimi ni mwanademokrasia sijapata kusikia wimbo huu wa taifa ukiimbwa halafu wanachama hawa wenzetu wakachomekea neno Chadema badala ya Tanzania kwenye ubeti huo! Kama ni kweli basi itakua ni mandumila kuwili wasio kitakia chama hiki mema, ni kweli tunaheshimu sana wimbo huu wa taifa na wala hatuna nia ya kuipotosha jamii kwa kufanya hivyo hii itakua ni sawa na kubadilisha bendera ya taifa na kupandisha bendera yenye nembo nyingine! hata mimi napiga vita kuhusiana na tabia hiyo kama ipo au imeshajitokeza. Alunta Continue!
 
Mkuu, hilo ni kweli na inasikitisha kama hali hii isipotolewa tamko au karipio kali kwa wafuasi wa CDM. Bado nasisitiza kwamba sidhani kama Slaa na Mbowe wanashabikia hili. Nawaomba watoe karipio kali .
 
Kwakweli japokua mimi ni mwanademokrasia sijapata kusikia wimbo huu wa taifa ukiimbwa halafu wanachama hawa wenzetu wakachomekea neno Chadema badala ya Tanzania kwenye ubeti huo! Kama ni kweli basi itakua ni mandumila kuwili wasio kitakia chama hiki mema, ni kweli tunaheshimu sana wimbo huu wa taifa na wala hatuna nia ya kuipotosha jamii kwa kufanya hivyo hii itakua ni sawa na kubadilisha bendera ya taifa na kupandisha bendera yenye nembo nyingine! hata mimi napiga vita kuhusiana na tabia hiyo kama ipo au imeshajitokeza. Alunta Continue!

Ni kweli kabisa....mimi pia ilinishangaza sana kwenye wimbo wa taifa ulipoimbwa wakati wa mkutano wa tarehe 5 january,uliozua vurugu arusha. Si sawa japo ilionyesha waliofanya hivyo si viongozi,ni wafuasi waliokuwa mkutanoni. Yabidi viongozi wakemee hilo.
 
Taifa gani halina utaifa?kungekuwepo taifa hata vitambulisho vya utaifa vingetolewa.Sasa hivi CHADEMA ndo inatunganisha
 
Naamini Dr.Slaa anaposoma maoni ya mtu kama wewe,, atakuwa anatamani kujificha. Inaonekana wewe hujui hata maana ya wimbo wa Taifa. Vitambulisho vya Taifa vinaingizje hapa? Na kama hakuna Taifa, wewe unaishi wapi mwenzetu? Mimi kwa jambo hili napenda kuona masilahi ya Taifa yanawekwa mbele,, uzalendo uje kwanza ndugu zangu wa CCM na CDM. Sote ni watanzania,, leo Rais anaweza kuwa yeyote lakini wimbo wa Taifa utabaki kuwa ule ule. Siyo leo Rais akiwa Slaa,, CCM wabadilishe wimbo wa Taifa, au akiwa Rais wa CUF CDM ibadilishe,, huu ni uhuni,,,Hatuwezi kuachia hali hii na kuichekeacheka,, ni hatari sana,, baadaye hatutakuwa na wimbo wa Taifa,, watu kama huyu figganigga ni wa kuogopwa kama ukoma na uzalendo wa nchi hana huyu. Naipenda Tanzania
 
Salamaleko wanajamvi,
Wimbo wa Taifa ni mojawapo ya alama za Taifa husika zikiwemo pia fedha, bendera nk. Kwa maana hiyo alama hizi ni vitu vya kuheshimika sana na si jambo la utani hata kidogo. Ndugu zetu wa CDM wamekuwa wakiimba wimbo huu wa Taifa na kubadilisha,, yaani pale panapotamkwa Tanzania,, wao huweka CHADEMA,,, Mfano "Tubariki CHADEMA na watu wake" Ukitazama hata ule mkanda wa maandamano ya Arusha on you tube utaona ninachosema. Kinachonipa kichomi ni pale ambapo viongozi wakuu Dr. Slaa, Mbowe na wengine wanaliachia tu jambo hili pasina kulitolea tamko kwa wafuasi wao kwamba wanapotosha na kuudhalilisha wimbo wa Taifa. Sasa unapoimba "CHADEMA na watu wake" katika wimbo wa Taifa,, ina maana CHADEMA ni Taifa? na lina watu wake?
Kwanini wasitunge tu nyimbo zao zenye kusifia CDM kadri wapendavyo badala ya kuudhalilisha wimbo wetu wa Taifa? Nasema ni kuudhalilisha kwa sababu mababu zetu waliopigania uhuru na kwa hali na mali na hatimaye kutuwekea wimbo huu wa Taifa, hawatafurahii mambo ya namna hii, na ni kutowatendea haki na kuwadharau kama si kuwadhalilisha. Mwalimu Nyerere huyu huyu ambaye CDM wanamtumia sana wanapotaka kulinganisha na viongozi wa leo wa CCM,, je angekuwa hai angefurahia tendo hili la kuuchafua wimbo wa Taifa kwa mithili hii??
Wenzao CCM wana nyimbo zao wenyewe lukuki za kusifia chama chao na kamwe miaka yote sijasikia wakiimba "CCM na watu wake".
Hata watoto wetu wanaokua leo,, wakiendelea kusikia hivyo,, ni picha gani wanaijenga? Shuleni wanaimba wimbo wa Taifa wenye maneno tofauti mtaani wanakutana na upotoshaji, tunakwenda wapi? Tofauti za kiitikadi zisifike mahali pa kudhalilisha Taifa, tuweke uzalendo mbele. Isije baadaye ikaonekana kama vile CDM ni chama cha fujo, vurugu na hata kuudhalilisha wimbo na Taifa Tanzania.
Nashauri Dr. Slaa na Mwenyekiti Mbowe,, wakiwa kama watanzania na wazalendo wa kweli,, walipinge na kulikemea kwa nguvu pindi wafuasi wao wanapotaka kuudhalisha wimbo na Taifa kwa ujumla. Hili mimi nalipinga kwa nguvu,,.Tanzania imekuwepo kwa muda mreefu na itaendelea kuwepo hata sisi tukifa,, kuuchezea wimbo wa Taifa kwa kubadilisha maneno ni jambo baya kabisa. Vipi kama kila chama TLP, UDP, CUF nk wakiimba hivyo? Wimbo huu utakuwa wa heshima kweli?
Angalizo: Wimbo wa Taifa siyo Bongo Fleva, ni alama ya nchi Tanzania na unatakiwa kupewa heshima stahili. Siamini kama Mbowe naSlaa wanawaambia wafuasi waimbe hivyo, na siamini kama wanafurahia.
Na kama wanafurahia,, Basi,, Leave me alone!!

wanacheza na Dola hawa. Ok si yetu macho cha msingi amani yetu tutailinda vilivyo hatutaacha watu waichezee.
 
Naamini Dr.Slaa anaposoma maoni ya mtu kama wewe,, atakuwa anatamani kujificha. Inaonekana wewe hujui hata maana ya wimbo wa Taifa. Vitambulisho vya Taifa vinaingizje hapa? Na kama hakuna Taifa, wewe unaishi wapi mwenzetu? Mimi kwa jambo hili napenda kuona masilahi ya Taifa yanawekwa mbele,, uzalendo uje kwanza ndugu zangu wa CCM na CDM. Sote ni watanzania,, leo Rais anaweza kuwa yeyote lakini wimbo wa Taifa utabaki kuwa ule ule. Siyo leo Rais akiwa Slaa,, CCM wabadilishe wimbo wa Taifa, au akiwa Rais wa CUF CDM ibadilishe,, huu ni uhuni,,,Hatuwezi kuachia hali hii na kuichekeacheka,, ni hatari sana,, baadaye hatutakuwa na wimbo wa Taifa,, watu kama huyu figganigga ni wa kuogopwa kama ukoma na uzalendo wa nchi hana huyu. Naipenda Tanzania

Well said! Salimia nakubaliana na wewe, ila nahisi huyu ni mtoto mdogo hivyo asamehewe bure tu. akikua atajua utaifa ni nini. As of now hajui kabisaaa mana ya utaifa na sidhani ana msaada kwa CDM kwa muda huu na asipobadilika hatakua na msaada wowote!
 
Taifa lenyewe liko wapi?..Nchi yenyewe iko wapi?...:shock:
Mnasemea nchi hii ya Al-Adawi na Rostam?..:shock:
Mnapenda nyimbo, wakati nchi inauzwa?...you are not serious..not at all!:shock:
Mnalilia beti za nyimbo, wakati mikataba ya hovyo inasainiwa MAHOTELINI!:shock:
Mnaongelea beti, wakati Mama Salma anaondoka kutalii na ndege ya Serikali!:shock:
Mnataka mapambio, wakati wake zenu hamjawaachia sukari nyumbani!:shock:
Mnatamani rap, wakati viwanda vinakufa kwa kukosa umeme!:shock:
My godness!!:shock:
Hivi tunawaza kweli?...tunaitakia mema nchi hii?..are we serious?...my hairs!
:shock:

Najua mkimaliza wimbo mtakuja na hoja ya MWENGE!...
Hoja dhaifu tupu...viroja!

Na kuna vijana wenzenu wanaanza maandamano ya nchi nzima leo kuunga mkono HOTUBA YA KIKWETE! , na bado mnaongelea wimbo!
I better quit earlier!
 
Nakubaliana na wewe mkuu hata mimi nimeliona hili na siyo wanachadema tu bali mashuleni, vyuoni na kadhalika wengi wamekuwa wakiongeza maneno yao wenyewe kwenye wimbo wa taifa .
Jambo la kujiuliza kwanini watu wengi hasa vijana amefikia hatua ya kutoheshemu nyimbo ya taifa je wamekosa uzalendo au wanaona kuna maana gani ya kuheshimu nyimbo ya taifa wakati hata wanaowaongoza hawaheshimu haki na misingi ya utawala bora? . Mimi nafikiri tuliangalie kwa mapana yake kuliko kuwa na fikira mgando wa kuichafulia CDM taswira yake.
 
Wanaofanya hivyo wanafanya makosa.Mi nafikiri waelimishwe tu bila jazba.Tanzania inayoimbwa kwenye wimbo huu ni hiihii inayojumuisha tanzania nne(Rejea makala ya Samsoni Mwigamba Tanzania daima Jumatano iliyopita uk.14).Ingawa wapigania haki wote na wazalendo ambao wanaamini taifa limefika hapa lilipo kwa sababu ya ombwe la utawala wa ccm wapo Tanzania ya nne,haifai kujitenga na taifa kwa kutumia wimbo wa taifa.Tupiganie kuwaöndoa hawa watawala watuachie Tanzania yetu ikiwa ni moja.
 
Taifa lenyewe liko wapi?..Nchi yenyewe iko wapi?...:shock:
Mnasemea nchi hii ya Al-Adawi na Rostam?..:shock:
Mnapenda nyimbo, wakati nchi inauzwa?...you are not serious..not at all!:shock:
Mnalilia beti za nyimbo, wakati mikataba ya hovyo inasainiwa MAHOTELINI!:shock:
Mnaongelea beti, wakati Mama Salma anaondoka kutalii na ndege ya Serikali!:shock:
Mnataka mapambio, wakati wake zenu hamjawaachia sukari nyumbani!:shock:
Mnatamani rap, wakati viwanda vinakufa kwa kukosa umeme!:shock:
My godness!!:shock:
Hivi tunawaza kweli?...tunaitakia mema nchi hii?..are we serious?...my hairs!
:shock:

Najua mkimaliza wimbo mtakuja na hoja ya MWENGE!...
Hoja dhaifu tupu...viroja!

Na kuna vijana wenzenu wanaanza maandamano ya nchi nzima leo kuunga mkono HOTUBA YA KIKWETE! , na bado mnaongelea wimbo!
I better quit earlier!

mkuu PJ yani kama tumelogwa vile.. watu wanaangalia vitu vya kipuuzi puuzi tu mambo ya msingi hamna mtu anaongea wanakaa ndani tu wakiugulia, sasa watu kuimba wimbo kwa maneno yao kwenye maandamano wanaona big deal..! this is so low of us

sijui tutabadilika lini
 
Nadhani tujiulize ni kwanini watu hao wanapenda kuongeza cdm badala ya Africa au Tanzania? Inawezekana wanaithamini zaidi cdm zaidi ya Tanzania na tujiulize kuwa ni kwanini waithamini cdm zaidi ta tz?, inawezekana wanapata faraja kwa kuwa WANACHADEMA badala ya kuwa WATANZANIA na ni kwanini faraja yao itokane na kuwa wanacdm badala ya kuwa watz?, inawezekana maumivu yao yanaisha kwa kuona LABDA ukombozi wao uko ndani ya CHADEMA badala ya kuwa ndani ya TANZANIA. Yawezekana pia wamechoka na kuitwa Watz wenye umoja wakati nchi yao LABDA inaliwa na wachache.

Kubwa zaidi tudeal na cause/ chanzo na si effect/ madhara au matokeo ndo tutaweza kutibu ugonjwa (kama upo)
 
Taifa lenyewe liko wapi?..Nchi yenyewe iko wapi?...:shock:
Mnasemea nchi hii ya Al-Adawi na Rostam?..:shock:
Mnapenda nyimbo, wakati nchi inauzwa?...you are not serious..not at all!:shock:
Mnalilia beti za nyimbo, wakati mikataba ya hovyo inasainiwa MAHOTELINI!:shock:
Mnaongelea beti, wakati Mama Salma anaondoka kutalii na ndege ya Serikali!:shock:
Mnataka mapambio, wakati wake zenu hamjawaachia sukari nyumbani!:shock:
Mnatamani rap, wakati viwanda vinakufa kwa kukosa umeme!:shock:
My godness!!:shock:
Hivi tunawaza kweli?...tunaitakia mema nchi hii?..are we serious?...my hairs!
:shock:

Najua mkimaliza wimbo mtakuja na hoja ya MWENGE!...
Hoja dhaifu tupu...viroja!

Na kuna vijana wenzenu wanaanza maandamano ya nchi nzima leo kuunga mkono HOTUBA YA KIKWETE! , na bado mnaongelea wimbo!
I better quit earlier!
[/QUOTE]

Mkuu PK utadhani hao wanaondamana ugumu wa maisha hauwagusi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom