Mapungufu haya ya JK yamenibowa

walonge

Member
Aug 1, 2010
25
3
Jamani naomba aliyekaribu na JK amjulishe kuwa sikufurahishwa na haya yafuatayo na ndio sababu namuhukumu kama alisema hivyo ila atatenda sivyo.

1) wakati wa kusherehekea kupewa kwake urais mbele ya NEC, yeye mwenyewe alikiri kuwa yapo mambo mazuri ambayo wenzake yaani vyama vingine vya siasa vimeyasema na aka ahidi kuyafanyia kazi. Sasa namuuliza je ni yapo hayo mazuri yaliomvutia? na ikiwa ana dhamira ya kweli basi si vibaya akataja mambo hayo ili aondolewe adhabu ya kuitwa alitamka hivyo ila hatatenda hivyo kwakuwa sitaki kumuita mna.....fiki!

2) Nalazimika kuamini hatatenda hivyo kwa kuwa nilitumainia katika hotuba yake ya kufunguwa bunge ange yazungumzia hayo mema ya wapinzani kwa kuwa pale alitumia nafasi ile kuonyesha vipaumbele vyake. Swali kwake je Jk amesha sahau kuwa amesema atafanyia kazi na sera za wapinzani? mbona sijaona akisema chochote?

Naamini Jk atajisafisha vyema kwa wananchi wake pale atakapokuwa jasiri wa kuweka wazi haya na hakika kw akufanya hivyo atarudisha heshima na uaminifu wangu kwake.
 
Kwa kifupi mambo yaliyomvutia ni ya CUF tu.
Jamani hata mseme nini JK hawezi kwenda kinyume na ccm ya Lowasa na Rostam Azizi, mnajisumbua bure tu.
 
Huyu jamaa siku zote ni usanii tu. Hakuna cha maana. Kumfuatilia ni kujisumbua na kupoteza muda wako bure tu.
 
yaani huyu dno bure kabisa ..nchi hii haijawahi kuwa na utawala wa hovyo kama kipindi hiki
 
Kipindi cha upongozi wa JK ni hasara na maumivu kwa wananchi wa TZ kama yale waloyopata wana wa Israel walipokuwa utumwani Misri.Sijui ataondoka lini tuanze upya.
 
Back
Top Bottom