Maprograma wa Tanzania mupooo?

mazd

Senior Member
Apr 3, 2011
187
32
Jamani, kwanini tunakua nyuma kiteknolojia kiasi hichi Watanzania?..Kutwaa mabegi na vibahasha eti tunasoma IT !!!...Ebu waliosoma waungane angalau na sisi tuambiwe tumetengeneza Software fulani--tusiishie kutengeneza vidatabase uchwara tukajiita maprograma wa ukweli--go open source---Na serikali yetu itujali, wasiwe madili ya software wanawapelekea mzungu na south Africa, wanatuona sisi matobwe?--Tuaamke tushikane. :mmph:

................................
Said,
Hermitscorp-Nokia Qt ambassador
Hermitscorp Laboratory
 
Tanzania bado. Matatizo mawili hapa. Moja, tunajifunza kile kilichosemwa darasani tu, matokeo yake wengi tuna basic knowledge. Wanakuja wahindi, wakenya na wasauzi wanatupiga bao. Kuna pesa nyingi sana zinaenda nje. Mbili, tunaridhika kwa kitu kidogo tukidhani ni kikubwa. Mtu anaweza kuwa anafahamu kutengeneza website basi anadhani yeye ndiyo yeye kwa sababu anazungukwa na kundi kubwa lisilo na uelewa.

Zaidi, tunaangushwa na exposure. Ni watu wachache katika medani ya sayansi wanadhani wanaweza wakafanya kazi ya thamani ya milioni 200. Na zaidi tunajikatisha tamaa kwamba, "Ah, nikompliketi kazi zenyewe ziko wapi?"

Tanzania bado. Bado sana. Ngoja Wahindi (wa India, sizungumzii rangi) waendelee kwanza.
 
@3D
Unathani Tanzania inaweza kua taayari kama sisi wenyewe hatujawa tayari?---mi nahisi ni uzalendo kulishikia bendera hili. Myself nimeshaonesha mfano katika web yangu na manufaa nimeshayaona (sio kazi ya kutuoa time bila mafanikio kama wengi wanavyodhani).
 
Safari bado ndefu bongo hata uwe unajua nini hauwezi pata chance yakutumika unakaa na mautaalam yako mpaka basi, mfano mm nilitengeneza website hii Y.D.C.P mwaka 2006 nikiwa imepita miaka 3 tangu nitoke form 4, and nilipo maliza chuo tu nkatengeneza MWANZA | TANZANIA | Mwanza City Directory
na hii ilikuwa bonge la project coz niliweka mpaka navigator ya maeneo muhimu ya mwanza. Ila sasa unakutana na pingamizi la kimazingira unaingia fani ingine.
Tanzania watalaam wapo bana basi 2.
 
Tatizo ni hilo kwamba wapo lakini kila mtu kivyake---kwa hapo hapana atake jua kua fulani anaelewa nini, but together we can.
 
Maprogramer na IT proffesional wapo kuna aina mbili za matatizo lakini comon ni lile la upande wwetu sisi IT profesional wengi tatizo amablo hata wahasibu, maengeneer ,wanasheria wa tanzania wanalo.

  • Tumejiset kutumwa na kuagizwa. Mtu kama mtaalama wa kompyuta aliyemalaiza chuo. hajawai kuandika wala kupropose any change kwa wakuu wake. tunasubiri tu kuambiwa fanya hivi fanaya vile. We dont relate mazingira yetu ya kazi na taaluma yetu kutafuta opprtunities. Mfano hili huwa nalisema sana .Pale wizaraya elimu kuna computer professionals. Je wamewai kupropose kwa wakubwa wao watafutwe walimu zitengenzwe video za masomo au practical . Hili wala haliitaji programmer. matokeo yake unakuta kuna project nyingi za It kwenye mawizara na idara but hazina manufaa zaidi ya kusaidia administration tu. Not so many ICT projects zinalenga kugusa maisha ya watu. Sasa kama wizaraya elimu ina prject 5 za IT na hakuna hata mmoja inayomguza mwanafunzi moja kwa moja inaonyesha hatuna priority. Hivi kutafutamwalimu mzuri wa hysics akarekodiwa kwenye DVD mbona haiitaji kujua java wala CISCO wala haitaji kuwepo kwa mkonga.

  • Maofisini tumejiset kussoprt na kutumika na sio kudevelop na kushauri .Kuna watu theoretically tunajua vitu vingi tu lakini ikija practical application output yetu ndogo.

  • Programmer na watu wa technical hawapendi documentation. hili nimelishuhudia kwenye example project nilitaka kujaribu kufanya na wana JF. https://www.jamiiforums.com/technology-and-science-forum/106152-it-project-kwa-vitendo.html .Watu wanataka ku rush kwenda kwenye coding. Na hivi ndio mprogramer na watu wa ICT wengi wanafanya kazi zao hata maofisini. Ukmuuliza project document or objective, hana. Muulize Requirement specification hana.. This It tell kwa nini unakuta sometime hata department za computer zinaongozwa na watu wasio na backgroung ya IT.
Nadhani imefika wakati watu walio maofisini tufanye kazi ki official . Tusibaki kulaumu wakati hatujawai kuandika memo au ku propose jambo lolote la fani yetu officialy in wrting. We are part of the problem and part of the solution .Wengi huwa tuna tabia yakujiona sisi ni part ya solution na sio problem. We need to change

Mlolongo wa matatio hayo mzizi wake ni kwenye elimu ambapo tumefundishwa kupokea tu.kuchallnege mwalimu ilikuwa kosa. Tumekuwa hivyo hivyo hata maofisini.hatujaelimishwa na kutayarishwa kuwa innovative . Ni kasumba mbaya kudhani kila kitu lazima kianzie kwa manager.
 
Mtazamaji, yaani nilikuwa natafuta ile post yako ili nkushtue kuhusu huyu jamaa aliyetengeneza mwanzadirectory hapo juu (mkuu Thinkpad). Hebu pitia, naona kama alichokifanya ni kile unachokitaka vile?
 
yah kazi yake nzuri but nadhani aangaliwe uwezekano wa kufanya yafuatayo

Yeye mwenyewe au watu wake kuingiza number ya key institutions na office kama

  • Public office na official contact za ofisi kama za RC, DC, Wabunge, Madiwani, RPC vitu vya polisi, etc
  • Taasisi muhimu kama kama shule, hospitali, Ustawi wa jamii, etc
  • Mashirika muhimu kama Tanesco, reli, Maji
Vile vile sijui how well amejaribu kufanya kazi yake ijulikne na watu wa kawaida kama madereva taxi, walimu wa sekondary na na primary, wauza samaki, madakatri ili wasajili mawasilino yao. Kazi yake nzuri but it still lack something. kama ni free kusajili basi he need to take it to the next step wakati akiiboresha . Next step yenyewe ni public awareness wajue faida ya kazi yake.

Kuna walimu hwajui kutumia net lakini wanapenda taarifa za ualimu wao zijulikane ili wapate wanfunzi wa kuwafundisha.. Anawasaidiaje hawa?
 
Safari bado ndefu bongo hata uwe unajua nini hauwezi pata chance yakutumika unakaa na mautaalam yako mpaka basi, mfano mm nilitengeneza website hii Y.D.C.P mwaka 2006 nikiwa imepita miaka 3 tangu nitoke form 4, and nilipo maliza chuo tu nkatengeneza MWANZA | TANZANIA | Mwanza City Directory
na hii ilikuwa bonge la project coz niliweka mpaka navigator ya maeneo muhimu ya mwanza. Ila sasa unakutana na pingamizi la kimazingira unaingia fani ingine.
Tanzania watalaam wapo bana basi 2.

mzee congz,nimeguswa na creativity yako
 
@3D
Unathani Tanzania inaweza kua taayari kama sisi wenyewe hatujawa tayari?---mi nahisi ni uzalendo kulishikia bendera hili. Myself nimeshaonesha mfano katika web yangu na manufaa nimeshayaona (sio kazi ya kutuoa time bila mafanikio kama wengi wanavyodhani).
Mkuu website yako inaitwaje na mie niitembelee
 
Kwanza TZ hatuna mfumo wa kuvumbua vipaji vya IT kutoka wakiwa wadogo....

Sio vipaji vya IT tu, Tanzania haina nia, mipango wala mawazo ya kuvumbua vipaji vya aina yeyote; labda kucheza kiduku! (hii ya kiduku 'inahimizwa' kwenye harusi, sendofu na besdei, huko utaona wanalazimisha watoto wa chekechea kukata mauno wimbo wa alaji halafu wanawapa soda)
 
Thanks mkuu, Unajua hii kazi niliifanya nilivyotoka chuo kabla sijapata kazi, sasa niko job na nature ya kazi nilio pata duh! website utaziskia tu kwa mbali na data base,
Ila hiyo project ilikuwa niiendeleze sana ,maana hata hapo kwenye map kama umena kuna vitu vingi vina miss yaani ilitakiwa maeneo yote ya muhimu yawe humo.
Sasa hapo nikama ina jiendesha lkn kwa kampuni kujiunga hapo walikuwa wanatoa pesa tena kwa muitikio mkubwa sana ila kutokana na kazi kunibana sasahivi hapa BMTL sina jinsi inabidi niwe mpole tu! nikipata mtu wa kuiendesha naweza kumkabidhi account akafanya kazi.
 
Kuna makosa makubwa sana yanayofanyika Yaani ile hali ya Serikali kuangalia vipaji vya watu tangu wakiwa wadogo,
Coz mfano mimi nilikuwa mzuri sana kwenye electronics circuit na ningefanya vizuri kuliko ktk IT lkn sasa wapi ukasome na wapi utapiga kazi ya electronics kama ilivyo. hakuna
 
Tatizo ni siasa nyingi nchi hii hawajaweka vipaumbele au kama vipo basi hawavifanyii kazi zaidi ya kukaaa maofisini na kula hela za wafadhili.Ni vijana wangapi wanao onyesha vipaji vyao katika technology ila hawapati support(Iko wapi DIT,Arusha tech ,etc).
Wenzetu nchi za jirani wako mbali katika haya maswala mfano uganda Uganda Linux User Group .naona na arusha nao wameanzisha group yao ALC | Arusha Linux Community so vitu kama hivi vikianzishwa kila mahali hata katika vyuo vinavyo fundisha ICT kuwepo na department ambayo wanafunzi wanaweza kuendeleza idea zao ingekua jambo la busara.ni mtazamo tu!!!
 
Kweli mkuu hapo ni changa moto....mimi nilishaskia jamaa anatengeneza helcopter hapo dar lkn sijui aliishia wapi sijui alikosa support. serikali ingemfadhiri naamini angetengeneza.
 
Kweli mkuu hapo ni changa moto....mimi nilishaskia jamaa anatengeneza helcopter hapo dar lkn sijui aliishia wapi sijui alikosa support. serikali ingemfadhiri naamini angetengeneza.

seriously i hate the use of the word 'serikali', hata sekta binafsi haina mwamko wa ku-finance start-ups. nobody is ready.... just nobody!
 
Back
Top Bottom