Mapokezi ya Rais wa Bank ya Afrika ni zaidi ya Rais wa Nchi

Thanda

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,915
596
Haya ..niko Arusha,Mkutano wa Bank ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank) kwa hapa umekuwa hosted na Wizara ya Mkulo(nakumbuka tulikaa vikao vingi sana kuhakikisha mkutano huu unafanyika Afrika Mashariki, Mkulo akapiga debe kwamba "Tanzania Tunaweza Bila Kuwezeshwa"kweli ukaja Arusha... lugha tunayoitumia ni Kiingereza na Kifaransa....wafaransa wa kizungu na wa kiafrika...kiswahili NO, mimi naongea kiswahili,. nakutana na mmoja wa waandaaji wa mkutano huu wa kimataifa wa wachumi."votre nom siil vous plait?=Your name please? najitambulisha,naye pia anajitambulisha kwangu, ana uraia wa nchi mbili Ghana na Ufaransa, ni dada mcheshi, mzungu, na ni mara yake ya kwanza kuja Tanzania, tunasalimiana, lakini ghafla Magavana wanaanza kuingia, mnisamehe sijapiga picha..waandishi wa habari usiseme.

Msafara wa rais wa bank ya maendeleo ya Afrika anakaribia kuingia hapa...maafisa usalama kama kawaida.Askari wamejipanga kwa ajili ya kutoa heshima kwa Rais, wote wana silaha...wanapokea maelekezo. mkutano haufanyiki hapa hotelini, ni eneo la AICC(Arusha International Conference Center) hapa ni kula na kulala tu...na vikao vingine vidogovidogo(billateral meetings, working conferences na Launching of AGF, Mabenki yote yana uwakilishi hapa.Wawakilishi wa bank mbalimbali wako hapa, makampuni ya simu pia, TANAPA wanaongoza kwa kuutangaza utalii.

Naiona red carpet kutoka mlangoni hadi kwenye kambarau (lift)ya hotel....

Pikipiki za polisi ziko nne, zinaingia kwa mbwembwe, askari wa usalama barabarani wako hadi ndani ya hotel wanaelekeza magari kila mahali..haya zinaingia gari za polisi kama nne, Field Force Unit, Ambulance ya polisi, Magari aina ya PRADO hayana idadi...yote yana nembo ya kampuni ya ANGONI. Magari madogo madogo na yale ya kukodi hayana idadi. La mheshimiwa silioni,..huyu hapa anashuka, ni mtu wa makamu kidogo, amevaa shati la rangi ya kijivu, suruali nyeusi, na miwani ya jua,. tunampokea anatupa mikono mmoja baada ya mwingine..anasema jambo karibu Tanzania, no anaongea kiswahili, jamani anaongea kiswahili safi...(nimerudi nyumbani,,,,anasema) ni mwafrika kutoka Africa ya...aaaaaaaaaaaaahh, kumbe ni Mheshimiwa Donald Kaberuka, Mnyarwanda anayeitumikia Bank hiyo kwa kipindi cha pili(Miaka Mitano).Anaelekezwa kwenda katika kambarau (lift)..anaingia...end of story. tuliobaki nje, raia na maafande wa usalama wote tunaelekea maeneo yetu muhimu.

Amesoma hapahapa Tanzania na Uingereza na Mwaka 1997 alikuwa waziri wa fedha wa Rwanda...Si tu anapewa salamu za ki-protokali, bali pia nimeangalia wingi wa askari eneo hili na aina ya ulinzi kwa mtu ambaye kwangu naona bora angepokewa kawaida kama viongozi wengine na sio mapokezi zaidi ya yale ya rais wa nchi...haya ngoja tuone mapokezi ya Kikwete kesho hapahapa katika hotel ya Mount Meru, Arusha
 
So, What? Is this really supposed to be here? a Tanzanian Critical Political Issue?

HELP !!!! where is our MODS??? Sometimes we do fail to deliver a political news
 
Jana imebidi nikimbie toka Arusha niende kuishi Babati manake Arusha hakuna Hotel zote ziko full booked kwa ajili ya mkutano wa AfDB! Hii si ndio tuliambiwa kwamba zimenunuliwa laptops kwa kila mshiriki kama sikosei? Isije ikawa hasara nyingine kama ya Sulvan.
 
Una mmana mkutano wa Sulvan uliitia hasara nchi yetu? Kiasi gani (US $ ngapi)?
 
Habari ni habari, nini maana ya forum?...ni kujuzana yanayojiri, unataka kusema kuwa hoja hii haipaswi kufahamika kwa wadau? Au huwa hausafiri na kujifunza mambo?, USHAURI WA BURE: Tembea na ujifunze kwa watu, ili kujua wenzako wanafanya nini, kwanini, wapi na lini..hiyo itakusaidia sana.

Karibu Arusha, Mkutano ni wa delegates zaidi ya 3000, hakuna pa kulala kama sio mwenyeji wa Arusha labda uwe ulifanya booking mwezi uliopita( Mwezi April)
 
Ni kweli, nafasi hakuna...zote zenye majina haya zimejaa pia ( INNS, RESORTS, GUEST HOUSES, MOTELS, DELUXES)nakwambia zote zimejaa. mkutano unaanza kesho, AICC, Simba Hall. Pia Kumbi za Mbayuwayu,Tausi,Mbuni na Manyara ziko booked hadi mkutano uishe.
 
Asante sana Mr Dash, Ila naomba nisikukaribishe Arusha kama uko mkoa mwingine, hadi Mkutano huu uishe kwani nina uhakika unaweza kosa pa kulala.Kama huamini muulize Kimbunga kwanini ameamua kwenda kulala Babati.
 
Mimi hapa sina comment kuhusu hasara, ila Mama Mdogo, C.E.O wa Sullivan, Ambassador Carl Masters, ambaye ndiye mume wa Hope Sullivan na mmiliki wa mlolongo wa makampuni kwa ajili ya kuwawezesha waafrika,aliingia jana jioni toka Marekani, akaonana na Mh. Rais, na leo hii yuko Arusha. Sasa kama unaweza mtafuta ili kumuuliza hilo, fine! Mimi sina haki ya kutoa namba zake za simu ingawa ninazo. Ila yuko, na hivi ninavyoongea na wewe amevaa shati jeupe na suruali ya light blue, viatu vyeusi. Leo anaonekana smart bila suti, amekaa upande wa mwisho kwenye kona anakunywa ginger beer (soda aina ya tangawizi ya kopo) kinywaji maarufu kwao Jamaica.

Anaweza akatusaidia kama mkutano aliouleta Arusha Mwaka 2008 ulikuwa na faida zipi ( Mimi nilikuwa mshiriki namba 2115 katika Mkutano huo)na hadi leo vile vitambulisho ninavyo.
 
Habari ni habari, nini maana ya forum?...ni kujuzana yanayojiri, unataka kusema kuwa hoja hii haipaswi kufahamika kwa wadau? Au huwa hausafiri na kujifunza mambo?, USHAURI WA BURE: Tembea na ujifunze kwa watu, ili kujua wenzako wanafanya nini, kwanini, wapi na lini..hiyo itakusaidia sana.

Karibu Arusha, Mkutano ni wa delegates zaidi ya 3000, hakuna pa kulala kama sio mwenyeji wa Arusha labda uwe ulifanya booking mwezi uliopita( Mwezi April)

Kwangu mimi, UAFRIKA ni zaidi ya mambo yote chini ya jua. Mwakilishi wa Afrika, huwezi kumfananisha na mtu wa kanchi kamoja, kasicho na hata dira. Alistahili zaidi ya aliyotendewa, labda tu awe mamluki. Ila African Bank ni bonge la hatua, kama tunaitakia mema Afrika yetu. AfrikaKwanza! AfrikaMoja! AfrikaSana!
Mungu wetu yu tayari kutushindia, anaita sasa!
 
Tanzania / Africa tunaweza kuendelea tukitokomeza uongozi wa aina ya mkweree na chama chake cha magamba kwani hawana vision!!
 
So, What? Is this really supposed to be here? a Tanzanian Critical Political Issue?

HELP !!!! where is our MODS??? Sometimes we do fail to deliver a political news

kiongozi unajua kuna aina ngapi za uandishi au za kufikisha habari?
 
Acha jamaa atupe story, unajua hata bia zote ni bure kwa courtesy ya ndugu yetu Kaberuka....:happy:
 
Jana imebidi nikimbie toka Arusha niende kuishi Babati manake Arusha hakuna Hotel zote ziko full booked kwa ajili ya mkutano wa AfDB! Hii si ndio tuliambiwa kwamba zimenunuliwa laptops kwa kila mshiriki kama sikosei? Isije ikawa hasara nyingine kama ya Sulvan.

Mkuu unatazamiwa kutumia 12bn !
 
Tangu Lema apigwe chini mikutano Arusha imeongezeka sijui watawala wameamua wanatufundisha nini.Wamiliki wa mahotels wanacheka jinsi hotels zilivyojaaa.
 
Pamoja na mambo mengine theme Tanzania ni mwanachama na tunachangia pesa lukuki about 20bn USD lakini hatukopi uhsusani sector binafsi na mikopo yao si chini ya 10m USD, kidogo serikali imekopa kupitia kilimo kwanza lakini wabongo hatuna bankable business plan ya kuvuta mkwanja huko. Mkutano huu unaweza kuwashawishi restructuring ya mikopo yao nasi tuvute.
 
Kwa Taarifa yako ni kwamba Dr.Donald Kebaruka ni Mnyarwanda wa asili ya Tanzania.Amesoma shule ya Msingi Murongo ipo Wilayani Karagwe ,mkonia Kagera mpakani mwa Uganda na Tanzania na kumaliza shule ya msingi mwaka 1954.Shule hiyo ya msingi ndiyo pia amesoma mdada maarufu mjini Dar Madame Ritta Paulsen,shule hiyo iko kijijini kwao na Rita.Donald amekulia Tz na kufanya kazi hadi wakati wa uongozi wa Kagame ndio aliomba wanyarwanda waliopo nje ya nchi warudi Rwanda kujenga nchi yao na wengi hasa waliosoma na kukulia Tanzania walirudi na kupewa vyeo vya juu akiwemo Dr Donald.Hadi anapata kazi ya uraisi wa AfDB Rais Mkapa ndiye alikuwa champion wake kumpendekeza.
 
Secondary kasomea Tabora boys....ni moja ya vichwa vya kinyarwanda wazazi wao walikimbia zamani wakati wa vurugu za kwanza kati ya wahutu na watusi. Kuna mwingine professor rwakabamba naye alisomea tanzania.

Katika record zake bunge la budget la rwanda baada ya Genocide alipo present budget ya wizara ya fedha haikueleweka kabisa...kwa most of MP's wa wakati huo ambao walipewa vyeo tu kwa ajiri ya either kupambana na vita vinginevyo..ilibidi afungue darasa bungeni...na project na writting board kwa ajiri ya kueleza budget nzima...na maana yake....
 
Ulinzi wote huo wanaogopa peoplezzzz powerr hakuna lingine

Mie nadhani ni woga wa Al shabab; ujue Arusha na hapa Kenya si mbali na hawa jamaa ni tishio, sidhani kama wanaeza kuwa wanawaogopa CDM kwani CDM si chama cha magaidi wala wahuni na wapenda vurugu"
 
Back
Top Bottom