Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,268
- 33,040
Mapishi ya pilipili mboga na ngisi
Mahitaji
Pilipili mboga gramu 250, ngisi gramu 250, chumvi kijiko kimoja, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, maji ya wanga vijiko vitatu, chembechembe za kukoleza ladha kijiko kimoja, kiasi kidogo cha vitunguu maji na tangawizi Njia 1. kata pilipili mboga ziwe vipande, kata ngisi awe vipande. 2. chemsha maji, halafu tia slesi ya pilipili mboga kwenye maji, korogakoroga, ipakue. Na tia vipande vya ngisi kwenye maji korogakoroga, ipakue. 3. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi korogakoroga, tia vipande vya pilipili mboga na ngisi, korogakoroga, halafu tia chumvi, chembechembe za kukoleza ladha, mvinyo wa kupikia, maji ya wanga, korogakoroga, halafu mimina mafuta ya ufuta, korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa. Mapishi ya kuku na limao
|
Mapishi ya kamba-mwakaje na uyoga
Mahitaji Kamba-mwakaje gramu 400, mafuta gramu 30, uyoga gramu 70, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, ute wa yai, mvinyo wa kupikia vijiko viwili, chumvi kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, pilipili hoho moja, wanga vijiko viwili, chembachembe za kukoleza ladha nusu ya kijiko. Njia 1. osha kamba-mwakaje, koroga pamoja na ute wa yai, mvinyo wa kupikia, chumvi na wanga. Kata pilipili hoho iwe vipande. Kata uyoga uwe vipande. 2. washa moto, tia mafuta kwenye sufuria, tia kamba-mwakaje kwenye sufuria korogakoroga, tia vipande vya uyoga, pilipili hoho, halafu tia chumvi, sukari, chembechembe za kukoleza ladha, korogakoroga, mimina maji ya wanga, korogakoroga, ipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.
Mapishi ya kuchemsha doufu kwa mvuke ndani ya majani ya yungiyungi
|